Dini ni mfumo wa maishani
Friday, August 20, 2010
Waziri wa Afya wa Afrika Kusini ameonya wahudumu wa sekta hiyo kuwa watakapothubutu kukwaza shughuli nyeti za afya watakumbwa na kesi za mauaji
Waziri wa Afya wa Afrika Kusini ameonya wahudumu wa sekta hiyo kuwa watakapothubutu kukwaza shughuli nyeti za afya watakumbwa na kesi za mauaji.
Aaron Motsoaledi, ambaye ni daktari alisema kuwa alishangazwa na mbinu zinazotumiwa na waandamanaji. Takriban wafanyakazi milioni moja walianza mgomo wa kazi siku ya Jumatano wakidai nyongeza ya mshahara.
Takriban wafanyakazi milioni moja walianza mgomo wa kazi siku ya Jumatano wakidai nyongeza ya mshahara.
Askari wa jeshi la nchi ndiyo wanatoa huduma katika hospitali za nchi kujaza nafasi zilizoachwa na waandamanaji ambao miongoni mwao ni wauguzi.
Hakuna dalili yoyote kuhusu kama mazungumzo kuhusu nyongeza ya mishahara kati ya serikali na mashirika ya wafanyakazi yenye uhusianoa na shirika la COSATU yatafanyika.
Serikali imekariri msimamo wake kwa waandamanaji kuwa haina uwezo wa kutimiza matakwa yao yanayokadiriwa kuwa mara mbili ya kiwango cha kushuka kwa kiwango cha uchumi. Imesema kuwa hata hicho kiwango kidogo cha asilimia 700 ilichojitolea itasuasua kukitimiza kwa malipo ya polisi, waalimu madaktari na wauguzi.
''Wagonjwa warudishwa nyumbani''
Athari za mgomo
Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg anasema kuwa kunako siku ya tatu ya mgomo hospitali nyingi zimebana wagonjwa wanaohitaji kuingia huku vyumba vya wagonjwa vikisimamiwa na msaada wa watu waliojitolea kwa kuwasaidia wagonjwa, kupika na kubadili shuka.
Serikali inaendelea kuwataka watu zaidi wa kujitolea katika hospitali na shule.
Waziri mwenyewe Dr Motsoaledi ameshiriki shughuli akiwa kwenye hospitali ya Chris Hani Bragwanath huko Soweto, ambako polisi iliwafyatulia waandamanaji risasi za mpira na maji waliojaribu kuwazuia watu wasingie hospitali hiyo.
Rais Jacob Zuma amesema kuwa wanachama wa mashirika ya wafanyakazi wana haki ya kuandamana ila akawataka wakomeshe ghasia na uvunjaji sheria
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment