Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Wednesday, August 4, 2010

Avaa Gauni la Spinachi Kupinga Watu Kula Nyama


Mwanamama wa nchini Kenya ambaye anapigania watu waache kula nyama na badala yake wawe wanakula mboga za majani, alikuwa kivutio mitaani alipovaa gauni lililotengenezwa kwa majani ya spinachi.
Michelle Odhiambo alivaa gauni refu lililotengenezwa kwa majani ya spinachi na kupita kwenye mitaa ya Nairobi akipiga kampeni ya kuwahamasisha watu waache kula nyama choma.

Michelle ambaye ni mwanaharakati wa shirika la kutetea haki za wanyama alisema kuwa aliacha kula nyama za aina zote miaka minane iliyopita.

Michelle aliwahimiza wamiliki wa mahoteli waache kupika vyakula vyenye nyama na badala yake watumie mboga za majani.

Hata hivyo kampeni yake ya kupinga ulaji wa nyama inakabiliwa na upinzani mkubwa hasa kwa kuzingatia kuwa mapishi bila nyama huhusishwa na umaskini nchini Kenya. Watu wenye pesa hupenda kujionyesha kwa kula nyama katika vyakula vyao.

Michelle alisema kuwa chakula ambacho hutumiwa kulisha wanyama wanaochinjwa kinaweza kutumiwa kulisha watu wengi.

Michelle pia alihoji tabia ya watu kuwahasi wanyama na kuwachinja bila ya kutumia dawa za kupunguza maumivu.

"Hii ni haki kweli?", aliuliza Michelle.

No comments:

Post a Comment