Dini ni mfumo wa maishani
Wednesday, August 4, 2010
Mchakato wa katiba mpya Kenya
Katika muda wa chini ya wiki moja Wakenya watapiga kura ya maoni tarehe 4 Agosti 2010,watapiga kura kukubali au kukataa katiba inayopendekezwa. Kura hii ya maoni ni kilele cha miongo miwili ya harakati za kutafuta katiba mpya.
Yafuatayo ni maswali na majibu kuhusu baadhi ya maswala muhimu katika mchakato huo:
b)Dini
Kama ilivyo sasa, katiba inayopendekezwa pia itakuwa na mahakama za waislamu maarufu kama mahakama za kadhi. Mahakama hizo zimekuwepo tangu wakati wa kupata uhuru lakini baadhi ya makanisa yalitaka mahakama hizi ziondolewe wakidai kuwa kuziweka katika katiba ni kupendelea dini moja. Mahakama hizo zinatatua kesi za kijamii na ndoa miongoni mwa waislamu.
c)Haki ya msingi:Utoaji mimba
Moja ya maswala ambayo yameleta utata kati ya viongozi wa dini na wanasiasa ni kipengele ambacho baadhi ya viongozi wa dini wanadai kinaandaa mazingira kwa watu kutoa mimba, lakini je kipengele hicho kinaruhusu utoaji mimba?
· Haki za msingi sehemu ya 2 kifungu 26(4) inasema:
‘Utoaji mimba hauruhusiwi, ila tu iwapo mtaalamu wa afya atabaini kuwa maisha ya mama mjamzito yako hatarini,au kulingana na mwongozo utakaotolewa na sheria zengine.’
Wanasema kuwa hali hii inatoa mwanya kwa watu kutoa mimba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment