Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Monday, August 16, 2010

'Dunia Amkeni' UPENDO UNAPUNGUA MAISHANI!?


Katibu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon ameyaita mafuriko ya Pakistan maafa makubwa sana ambayo hajawahi kuyaona katika maisha yake. Ameyataka mataifa ya magharibi yaamke na kuanza kutoa msaada kwa Pakistan kama yalivyoisaidia Haiti. Watu 1600 wameishafariki hadi sasa.
Umoja wa mataifa umezitaka nchi wanachama kuamka na kuanza kutoa msaada kwa wahanga wa mafuriko ya Pakistan ambayo yamepelekea vifo vya watu 1600 na watu milioni 20 kukosa makazi.

Hali iliyopo nchini Pakistan inasikitisha sana kiasi cha kwamba katibu wa Umoja wa mataifa, Ban Ki-moon alisema kuwa mafuriko ya Pakistan ndiyo maafa makubwa sana aliyowahi kuyaona katika maisha yake.

Nchi za magharibi ambazo zilitoa msaada mkubwa kwa wahanga wa tetemeko la ardhi nchini Haiti, zimeamua kukaa kimya wakati Wahanga wa Pakistan wakilia kuomba msaada.

Umoja wa Mataifa ulizitaka nchi wafadhili kuchanga dola milioni 459 ili kuisaidia Pakistan lakini hadi sasa ni asilimia 25 tu ya pesa hizo zimepatikana.

"Katika miaka ya nyuma nimewahi kuona maafa mbalimbali yanayotokana na nguvu za asili katika sehemu mbalimbali duniani, lakini sijawahi kuona maafa kama haya", alisema Ban Ki-moon.

Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha nchini humo, maelfu ya watu walizikimbia nyumba zao mwishoni mwa wiki baada ya mto Indus kufurika.

Kumekuwa na taarifa za watu kupigana wenyewe kwa wenyewe wakigombania chakula.

Ziara ya Ban Ki-moon nchini Pakistan inatarajiwa kuzifanya nchi za magharibi ziongeze kasi yao ya kutoa msaada kwa Pakistan.

Chini ni VIDEO mbili za maafa ya Pakistan na jinsi wahanga wa mafuriko wanavyopigania chakula cha msaada

No comments:

Post a Comment