Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Tuesday, August 17, 2010

Albino anusuruka kuuzwa -Mwanza


RAIA wa Kenya, Nathan Mtei [28] anashikiliwa na pollisi mkoani Mwanza kwa tuhuma za kumsafirisha albino toka nchini humo kwa lengo la kuja kumuuza kwa shilingi million 400 akiwa mzima
Albino aliyenusurika kuuzwa ni Robson Mkwana Mnyoti (20) raia wa nchini Kenya alisafirishwa na mtuhumiwa huyo hadi mkoani Mwanza bila kujitambua kuwa kuwa yeye ni biashara kwa kuahidiwa ajira.

Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoani Mwanza, Bw. Simon Sirro, alisema wamemkamata mtuhumiwa huyo kwa kupata taarifa kutoka kwa raia wema na kuunda timu ya askari .

Kamanda Sirro alisema, askari polisi walipopata taarifa kuwa kijana huyo anahusika na uuzaji wa viungo vya albino, askari hao walijifanya kuwa wanahitaji viungo hivyo wakampigia simu kuwa wanahitaji viungo hivyo kwa kupewa namba na raia wema na mtuhumiwa huyo aliwaahidi askari hao kuwa atawapatia mzigo huo Agosti 13 mwaka huu.

Hivyo ilipofika siku hiyo aliwapigia askari hao simu kuwa mzigo waliuokuwa wanauhitaji uko tayari na askari hao walipofika katika hoteli aliyofikia na albino huyo iliyopo maeneo Nyakato aliwaonyesha albino huyo na kuwataka askari hao wampe shilingi milioni 400 na anamuuza albino huyo akiwa mzima.

Hivyo mtuhumiwa huyo alipewa mtego kwa kupewa pesa hivyo na kuwataka askari hao waende nae na watashughulika wenyewe maswala mengine na ndipo mtuhumiwa huyo alipokamatwa.

Kamanda Sirro alisema kuwa, mtuhumiwa huyo katika kibano cha polisi alikiri ni kweli anahusika na biashara hiyo kwa muda mrefu na alimrubuni albino huyo kuwa anakuja kumatafutia kazi y a udereva nchini.

No comments:

Post a Comment