Waziri wa Sheria na rafiki wa karibu wa Mfalme Mswati wa Swaziland ametupwa jela na anakabiliwa na adhabu ya kifo baada ya kumla uroda mmoja wa wake wa mfalme Mswati.
Chini ya amri ya mfalme Mswati, waziri wa sheria na rafiki wa karibu wa Mfalme Mswati, Ndumiso Mamba ametupwa jela baada ya kukamatwa kitandani hotelini akimla uroda malkia wake, Nothando Dube, ambaye ni mke wa 12 wa mfalme huyo wa Swaziland.
Malkia Nothando Dube mwenye umri wa miaka 22 amewekwa ya chini ulinzi mkali nyumbani kwa mama mkwe wake huku waziri huyo mkware akiendelea kunyea debe jela.
Waziri Mamba alikamatwa na polisi kitandani akijivinjari na malkia wake kwenye hoteli ya Royal Villas mjini Mbabane.
Wadadisi wa masuala ya kisiasa nchini Swaziland walidai kwamba uhusiano wa kimapenzi kati ya malkia na waziri huyo ulikuwa ukijulikana sana kilichobaki watu walikuwa wakisubiri ushahidi.
Mamba huenda akahukumiwa adhabu ya kifo iwapo atapatikana na hatia.
Mfalme Mswati yuko nchini Taiwan kwa ziara ya kiserikali.
Dube ambaye amezaa watoto wawili na mfalme Mswati aliolewa na Mfalme Mswati akiwa na umri wa miaka 16 baada ya kuonekana kwenye dansi maalumu la kila mwaka la wasichana bikira ambapo wasichana hupita wakiwa wameacha matiti yao nje huku mfalme akijichagulia yupi amuongeze kwenye himaya zake.
Dube huenda akafukuzwa toka kwenye himaya za kifalme iwapo atapatikana na hatia.
No comments:
Post a Comment