Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Tuesday, August 17, 2010

Kesi ya UKIMWI: 'Naomba radhi'



Mwimbaji wa kundi moja la muziki nchini Ujerumani lijulikanalo kama No Angels, amekiri kosa la kufanya mapenzi bila kinga na wanaume kadhaa bila kuwaonya kuwa ana virusi vya HIV.


Nadja Benaissa

Nadja Benaissa

Mwanamuziki huyo Nadja Binaissa mwenye umri wa miaka 28,



alikuwa akizungumza katika ufunguzi wa kesi yake katika mji wa Darmstadt nchini Ujerumani.
Ninaomba radhi


"Ninaomba sana radhi", Bi. Benaissa ameiambia mahakama. Hata hivyo amekanusha kuambukiza mtu yeyote kwa makusudi.

Anakabiliwa na mashitaka ya kudhuru mwili kwa kutuhumiwa kumuambukiza mtu mmoja virusi.

Aidha, ameshitakiwa kwa tuhuma za kutaka kudhuru mwili wa mtu kwa kutuhumiwa kufanya mpenzi na wanaume wawili ambao hata hivyo hawakuambukizwa.

Iwapo atakutwa na hatia, Bi. Benaissa huenda akakabiliwa na kifungo cha kati ya miezi sita hadi miaka 10.
Mapenzi bila kinga

Baada ya kesi kufunguliwa, shirika la habari la Ujerumani DAPD liliandika taarifa kutoka kwa mwanasheria wa Bi. Benaissa, ikisema mwanamuziki huyo hakuweza kushughulikia vyema suala la kuishi na virusi vya HIV, na pia kukiri kufanya mapenzi bila kutumia kinga.

Lakini mwimbaji huyo alisema: " Hata mara moja sikutaka mpenzi wangu kuambukizwa."

Bi. Benaissa alikamatwa mjini Frankfurt mwaka jana, muda mfupi kabla ya kufanya onyesho lake la muziki, na aliwekwa rumande kwa siku 10.
Uhalifu wa maambukizi

Wanaharakati wa masuala ya UKIMWI wameshutumu mamlaka za huko kwa jinsi walivyolishughulikia suala la kukamatwa kwa msanii huyo, na kuonya dhidi ya kuharakisha suala la uhalifu wa maambukizi ya virusi vya HIV.






Kwa mujibu wa waendesha mashitaka, Bi. Benaissa alijijua kuwa na virusi vya HIV tangu mwaka 1999.

Mpenzi wake wa zamani, ambaye ana virusi vya HIV, anasema mwimbaji huyo alimuambukiza mwaka 2004, na anatazamiwa kufika mahakamani mjini Darmstadt kama mlalamikaji.

Mwezi Novemba mwaka jana, Bi. Benaissa katika tamasha la UKIMWI mjini Berlin, alijitokeza na kusema hadharani : "Jina langu ni Nadja Benaissa, nina miaka 27, nina mtoto wa kike na ninaishi na virusi vya HIV."
Mafanikio

Kundi la waimbaji la No Angels liliundwa mwaka 2000 katika kipindi cha televisheni cha waimbaji wa kimataifa, na baadaye kurekodi vibao vilivyovuma na hatimaye kuwa kundi la kina dada lenye mafanikio zaidi nchini humo.

Mwaka 2007, waimbaji hao waliungana tena na kushiriki katika mshindano ya wimbo bora wa Eurovision, na kushika nafasi ya 23.

Kesi ya Bi. Benaissa inatarajiwa kumalizika mwisho wa mwezi huu.

No comments:

Post a Comment