Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Friday, September 17, 2010

Ufaransa kuendelea na bomoabomoa





BRUSSELS

Ufaransa itaendelea na mpango wake wa kuzibomoa kambi za Waroma zisizokuwa halali nchini humo. Akizungumza katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels, Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ameutetea uamuzi wa serikali yake wa kuwafurusha Waroma kwani ni suala la usalama. Hata hivyo kauli za kuifananisha hatua hiyo na yaliyowasibu Waroma na Wayahudi wakati wa vita vya pili vya dunia zilimshtua. Siku ya Jumanne wiki hii, Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayehusika na masuala ya sheria Viviane Reding, aliikosoa Ufaransa kwa sababu ya kuwafurusha Waroma na akalifananisha hilo na yale yaliyotokea wakati wa vita vikuu vya dunia. Kwa sasa Bibi Reding tayari ameiomba radhi Ufaransa. Duru zinaeleza kuwa Rais Sarkozy wa Ufaransa na Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso walirushiana maneno makali kuhusu suala hilo wakati wa mlo wa mchana. Kamisheni hiyo imetangaza kuwa ina mpango wa kuichukulia Ufaransa hatua za kisheria kwani kuna uwezekano kuwa imekiuka sheria za Umoja huo zinazowapa raia wa mataifa wanachama uhuru wa kusafiri

No comments:

Post a Comment