Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Wednesday, September 1, 2010

Blair amuita Brown "mwehushaji"





Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair amemuita mrithi wake Gordon Brown "mwehushaji", wakati akizungumzia mvutano wao katika kitabu chake kuhusu maisha yake.





Amemuelezea Bw. Brown kama waziri wa fedha "mwenye uwezo na mchapa kazi" lakini ameongeza kuwa alikuwa akimweka chini ya "shinikizo kali".
Mtu wa ajabu

Bw. Brown alikuwa "mtu wa ajabu" na chama cha Labour kilipoteza katika uchaguzi wa hivi karibuni kwa sababu kilijiweka mbali na mabadiliko zaidi, amesema Bw. Blair.

Lakini mmoja wa vigogo wa Labour Diane Abbott amemtuhumu Bw. Blair kwa "kumchinja" mrithi wake.




Katika kitabu chake, waziri mkuu huyo wa zamani pia ameelezea "masikitiko" yake juu ya vifo vya wanajeshi wa Uingereza walioko Iraq, lakini ametetea uamuzi wake wa uvamizi wa Iraq ulioongozwa na Marekani mwaka 2003.

Hii ni mara ya kwanza Bw. Blair amezungumzia kinaganaga kuhusu uhusiano wake na Bw. Brown wakati yeye akiwa waziri mkuu na Bw. Brown akiwa waziri wa fedha. Mhariri wa masuala ya kisiasa wa BBC Nick Robinson amesema inaonekana mambo yalikuwa mabaya zaidi kati ya wawili hao, kuliko ilivyokuwa ikiripotiwa na vyombo vya habari wakati huo.
Brown

Brown na Blair

Katika kitabu hicho, Bw. Blair anamuelezea Bw. Brown, ambaye alimrithi uwaziri mkuu mwaka 2007, kama "mtu wa ajabu" na kusema wakati wake kama waziri mkuu "kamwe usingefanikiwa". Lakini pia ameandika kuwa ingekuwa "vigumu mno" kumzuia kuchukua nafasi hiyo, kutokana na msingi wa nguvu yake ndani ya chama na vyombo vya habari.




Uhusiano mgumu

"Alikuwa mtu asiyewezekana, wakati mwingine kama anakutia wehu. Lakini alikuwa shupavu, mwenye uwezo na mchapa kazi, na hizo ndio sifa ambazo daima nitamheshimu" amesema Bw. Blair.
Kitabu

Kitabu cha Tony Blair

Bw. Blair amesema iwapo angemfukuza kazi au kumshusha cheo Bw. Brown "chama na serikali ingeparaganyika na hali hiyo huenda ingechochea zaidi yeye kuingia madarakani kwa haraka zaidi".

Katika mahojiano na BBC ambayo yameambatana na kuzinduliwa kwa kitabu hicho, Bw. Blair amesema uhusiano wake na Bw. Brown ulikuwa "mgumu, na usiowezekana" lakini kwa "kipindi kikubwa wakati tukiwa madarakani, alikuwa ngome ya uimara".

Ameongeza kuwa, wakati Bw. Brown akiwa waziri wa fedha, "watu labda walikadiria juu sana uwezo wake kuwa waziri mkuu" lakini tena "katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita wakati akiwa waziri mkuu, watu labda walikadiria chini uwezo wake".



Hatari zaidi
Blair

Blair akiwa Iraq

Kuhusu vita vya Iraq, Bw. Blair pia amesisitiza kuwa kumuacha Saddam Hussein kukaa madarakani kungekuwa na "hatari zaidi" kwa usalama, kuliko kumuondoa madarakani.

Amekiri "kuwa hatukutazamia nafasi ya al-Qaeda au Iran" katika kupanga kitakachotokea baada ya vita, na pia amezungumzia "kusikitishwa" kwake na vita hivyo.

No comments:

Post a Comment