Dini ni mfumo wa maishani
Wednesday, September 8, 2010
HAKIKA , UCHUNGUZI WA HISTORIA YA MTUME WA WAISLAMU , MUHAMAD (S.A.W) ; UTAKUTA KINACHOELEKEZA UKWELI WA UTUME WAKE KWA MAMBO MATATU
1- KWANZA:
HISTORIA YAKE MAARUFU INAYOTAMBULIKANA IMEDHIHIRI KWA KILA UPANDE WA MAISHA YAKE . KWAHAKIKA ALITAMBULIKA MUHAMAD (S.A.W) , KWA TABIA YAKE TUKUFU, AKAJULIKANA KWA UKWELI NA UAMINIFU WAKE IKAFIKA HADI WATU WA MAKA WALIMWAMINI KWA MALI YENYE THAMANI WALIOMILIKI .
NA ALIKIWA BI KHADIJA BINT KHUWELED (mmoja wa matajiri wa Maka ) AKIMWAKILISHA KWENYE BIASHARA ZAKE KWA AJILIYA UAMINIFU NA MIPANGO YAKE MIZURI, NA MAPENZI YAWATU KWAKE.
ALIKUWA MASHUHURI MBELE YA WATU KWA AJILI YA AKILI NA UADILIFU WAKE. AKAWA NDIYE ALIYEUNGANISHA WATU WA MAKA KWA RAI YAKE MAARUFU KATIKA MAS"ALA YA TOFAUTI ILIYOTOKEA KATI YA MAKABILA YA MAQURESHI PINDI WALIPOIJENGA AL-KAABA
( NYUMBA YAMWENYEZI MUNGU ) WAKAHITALIFIANA KWA NI NANI ATAKAEWEKA JIWE JEUSI MAHALA PAKE .
AKAWA NDIYE ATAKAETOA RAI YAKE YA SAWA ; IKAWA NDIYO SABABU YA KUZIMISHA MOTO WA FITNA BAINA YA WATU WA MAKA.
NA WAMEKUBALIANA WANAHISTORIA KWAMBA HAIKUTHUBUTU KWA MTU YEYOTE WA MAKA WALIOISHI WAKATE WAKE , BALI HATA WALE WAPINZANI WA UTUME WAKE NA KUMTUHUMU KWA KUSEMA URONGO AU KHIANA AU MWENDA WAZIMU.
BALI WALIKUWA MAJIBU YAO ALIPOWAKUTANISHA KATIKA SAFU MWANZO WA UTUME WAKE, TIMAMU WA AKILI NA AFIYA .
UMASHURI WA UKWELIWAKE :
"AKAWAAMBIA" : "MWAONAJE NIKIWAAMBIA KUNA MAADUI WAPANDA FARASI WANAKUJA KUWAVAMIA . JE MUTANIAMINI? SAUTI ZOTE KWA PAMOJA.
"NDIO !!! HATUJAKUSIKIA UKISEMA URONGO"
AMA MAISHA YAKE BAADA YA KUPEWA UTUME NA DALILI YA UMAARUFU WAKE MZURI :
ALIISHI MKARIMU NA TABIA NJEMA ; MASAHABA WAKE WAKAMPENDA SANA.
WALIKUWA WAKJITOLEA KWA MALI NA NAFSI ZAO. ALIISHI MAISHI YASAHALI MNO.
IKAWA WAKATI HUO KUNA DALILI YA WAZI KWA KILA ANAYEMJUA KWA UKWELI NA IMANI YA UTUME KUTOKA KWA MOLA WAKE.
2- PILI:
LENGO LAKE NI KULINGANIA WATU KWA ALOKUJANAYO. MWANZO WA KULINGANIA. KWAKE, WATU WAKE WALIMTUNUKU AWE KIONGOZI WAO, WAKAMTUNUKU MALI MENGI, WAKAMPA NA MKE ALIYEKUWA MZURI KULIKO WANAWAKE WOTE WAKIARABU.
AKAKATAA!!
AKAWAHAKIKISHIA KWAMBA:
LENGO LAKE NI KUFIKISHA DINI YA KIISLAMU KWA WATU WOTE , IKAWA MWENENDO WA MAISHA YAKE NI KUTIMIZA LENGO LAKE .
IKAWA TABIA NA ANAVYOISHI NA WATU ANAPOWALINGANIA, NA BAADA YA MWENYEZI MUNGU KUMBAINISHA DINI YAKE KATIKA MAKA NA MADINA NA SEHEMU ZA BARARABU NI DALILI KWAMBA HAKUWA NA TAMAA YA KUPATA URAIS AU UFALME.
BALI YEYE NI MTUME ALIUELETWA NA MOLA WAKE.KWA HIVYO BW. ADEI BIN HATEM, MMOJA WA VIONGOZI WA KABILA LA TEJA AMBAYE ALIKUWA MNASARA; AELEZA TABIA YA MTUME (S.A.W) ALPOKUTANA NAE KWA MARA YA KWANZA.
AKASEMA : NIKAONDOKA KWENDA NYUMBANI KWAKE.
WALLAHI NIKAMKUTA MTU MMOJA MREFU ANAONGEA NAE. ASEMA NIKAJIAMBIA NAFSI YANGU WALLAHI NI MALAIKA. KISHA HISTORIA HAIKUSAHAU WALIOMKADHIBISHA KATIKA WATU WA MAKA AMBAO WALIM"UDHI WAKAWADHIBU SAHABA ZAKE BALI WALIJARIBU KUM"UWA NA KUMPIGA VITA, WAKAMFUKUZA,WAKAWAUA WENGI WA SAHABA ZAKE.
NA HAIKUWA SIKU WAALIPOKOMBOA MAKA ILA ALIWATENDA MEMA.
WAKASEMA NDUGU MKARIMU NA MWANA WA NDUGU MKARIMU.
AKATAMKA KWA TABIA YA UTUME MKARIMU "NENDENI NYIE MUKO HURU" AKAWASAMEHE.
3- TATU :
IMEBAKI TUANGALIE KWA YALE ALOKUJA NAYO:
TUANGALIE QURANI: IMETEREMKA KWAKE QURAN AMBAYO ILIYOKUA NA MIUJIZA MIKUBWA.
NI MIUJIZA ILIYOJE KATIKA QURAN? IMETEREMKA QURANI NA MIUJIZA KILA UPANDE.
A - KWA UPANDE WA FASAHA YA LUGUA ; KWA UPANDE WA NIDHAM; KWA NJIA YA KUFIKIZA KWA DALILI ZA UTAMSHI WA MAANA.
HIVYO INATUARIFU YA KWAMBA-JUU YA KWAMBA HAKUNA KATI YAO ALOTIA SHAKA QURANI PAMOJA NA UADUWI WALOKUA NAO.
NA VIPI TUTAKAPOMJUWA MTUME (S.A.W) ALIYEKUWA HAJUI KUSOMA WALA KUANDIKA; KASHA INATEREMKA KITABU YENYE SIFA ZA MIUJIZA NI KWAMBA JAMBO HILI LINATUPA DALILI MUHIMU YA KWAMBA YEYE NI MTUME ALIYELETWA NA MOLA WAKE.
NA KATIKA MIUJIZA MIKUBWA KATIKA QURANI INAYOPAMBANA NA MA-QURESHI NA WAARABU; BALI KWA WATU WOTE HADI SIKU YA MWISHO; KWAMBA WALETE MFANO WA QURANI AU SEHEMU YAKE.
HADI TAREHE YA LEO YA KARNE YA KUMI NA NNE ZIMEPITA, HAJAPATIKANA MTU , ANGALAU SENTENSI MOJA PEKEE INAYOFANANA NA QURANI .
HATOPATIKANA HADI SIKU YA MWISHO.
PAMBANO HILI LINAEADELEA KWA JINSI YOTE..
B - NA KATIKA HABARI ZILIZOPITA ; HAZIKUWA ZIKUJULIKANA. IMEELEZA VISA VYA MITUME, REHMA NA AMANI ZIWAFIKIE WOTE PAMOJA NA MTUME WETU.
NA WALIKUWA MAYAHUDI; NAO, NI WATU WALOTEREMSHIWA KITABU, WALIKUWA WAKISIKILILZA HII QURANI NA WAKISIKILISA KISA CHA MTUME WAO MUSA (AMANI ZIMFIKIE) ; NA JUU YA HIVYO ; HAKUTOKEA HATA MYAHUDI MMOJA ALIYEKADHIBISHA YALIYOMO NDANI YA QURANI.NA KUMBUKA MUHAMAD (S.A.W) NI MTU ASIYEJUA .KUSOMA WALAKUANDIKA..
MWENYEZI MUNGU ASEMA KATIKA QURANI:
(وَمَا كُنتَ تَتْلُو مِن قَبْلِهِ مِن كِتَابٍ وَلَا تَخُطُّهُ بِيَمِينِكَ إِذاً لَّارْتَابَ الْمُبْطِلُونَ) (العنكبوت : 48 )
NA HAKUWA MWENYE KUSOMA KITABU CHOCHOTE KABLA YA HIKI, WALAHUKUKIANDIKA KWA MKONO WAKO WAKO WA KUUME(INGEKUWA HIVYO) WANGEFANYA SHAKA WALE WANAOTAKA KUBADILISHA HAKI). (ALANKABUT AYA:48).)
( هُوَ الَّذِي بَعَثَ فِي الْأُمِّيِّينَ رَسُولاً مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ) (الجمعة : 2 (
YEYE NDIYE ALIYEMLETA MTUME KATIKA WATU WASIOJUA KUSOMA, ANAYETOKANA NA WAO, AWASOMEE AYA ZAKE NA KUWATAKASA NA KUWAFUNZA KITABU NA HIKIMA (ILIMU NYINGINEZO) NA KABLA YA HAYA WALIKUWA KATIKA UPOTOFU (ILIMU NYINGINEZO) ULIO DHAHIRI.(AL-JUMUA AYA:2) NA MTUME (S. A.W) ALIKUWA NI MKAZI WA MAKA WALA HAJATOKA NJE YA WATU WAKE, WALA HAJASAFIRI ISIPOKUWA SAFARI MBILI PEKEE YA KWENDA SHAM.
ALITOKA NA AMI YAKE ALIPOKUWA KIJANA MDOGO KABLA HAJABALEGHE; BILA YA KUMUEPUKA. NA MARA YA PILI ALIKWENDA NA MAISARA (MFANYI KAZI WA BI KHADIJA) KATIKA BIASHARA, AKIWA NA UMRI WA KUZIDI ISHIRINI HIVI.
NA WALIKUWA WAKIMJUWA VIZURI HALI YAKE. WALA HAJAKUTANA NA MWANACHUONI YEYOTE KATI YA MAYAHUDI NA MANASARA NA WENGINEO. BAHIRA (MWANACHUONI WAKIYAHUDI) ALIPOMUONA MTUME(S.A.W) ALIMTAMBUA KWA SIFA ZAKE NA UTAJO WAKE.
AKAWAMBIA WATU WAKE WAMUHIFADHI NA MAYAHUDI.
WALA WASIMWACHE KUONGEA NAO KWA UREFU. NA MWENYEZI MUNGU NDIYE ALHEKUWA AKIMLUNDA MTUME WAKE (S. A.W) KAMA ILIVYO KATIKA KITABU CHAKE; JUU YA KWAMBA ANAFUNDISHWA NA KIUMBE MWENGINE MWENYEZI MUNGU ASEMA KATIKA QURANI:
(وَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّهُمْ يَقُولُونَ إِنَّمَا يُعَلِّمُهُ بَشَرٌ لِّسَانُ الَّذِي يُلْحِدُونَ إِلَيْهِ أَعْجَمِيٌّ وَهَـذَا لِسَانٌ عَرَبِيٌّ مُّبِينٌ) (النحل : 103 )
NA BILA SHAKA TUNAJUA KWAMBA WANASEMA: YUKO MTU ANAYEMFUNDISHA. (LAKINI) LUGHA YA YULE WANAYEMUELEKEZEA (KUWA ANAMFUNDISHA MTUME) NI YA KIGENI, NA HII (LUGHA INAYOTUMIKA KATIKA QURANI) NI LUGHA YA KIARABU BULBUL. (AL- NAHL:AYA 153).
KATIKA AYA HII INAWAKADHIBISHA KWANI LUGHA WALIONASIBISHA KUMJUA MTUME (S. A.W) NI MGENI, HANA FASAHA YA LUGHA, NA QURANI IMETEREMKA KWA LUGHA YA KIARABU ILO WAZI NA KUBAINIKA Juu ya kwamba katika qurani kuna majibu kwa wale walopewa kitabu kwa baadhi waliozua kwamba ""mtume Issa (amani zimfikie) amesulubiwa .
na kwamba wengine wasema ni Mungu,na wengine wasema ni mchawi .na kauli yao ya kumsingizia mtume Suleiman (amani zimfikie),alikuwa ni mchawi, na mfano wa hayo.
Na katika qurani visa vya mitume, rehma na amani ziwafikie pamoja na mtume wetu Muhamad(s.a.w). haipatikani katika vitabu vya torati na injili mfano wa visa vya Mitume Hud, Saleh,Shueib na wengineo.
Na katika qurani ukumbusho wa akhera na maelezo yake.
na sifa za pepo na moto, furaha na adhabu;haya hayapatikani katika torati wala injili.
ama kwa yalofichika, yajayo mbeleni:
tumearifiwa kwamba Aba-lahab ami yake Mtume (s.a.w) hatoamini na atakufa akiwa kafiri. na bwana huyu alikuwa hai wakati wa kuteremka aya hizi na akazisikia na juu ya hivyo hakuamini. na hakuwa nimwenye kuamini hata kukawa na shaka ya ukweli wa qurani.
Na ushahidi mwingine ni kwamba qurani iliwapasha habari kwamba wa-Roma, baada ya kushindwa na ma- Fursi, watawashinda ma-Fursi na watanusurika.
Na walikuwa wafuasi wa mtume Muhamad (s.a.w) walikuwa wakishindana na watu wa Maka kwa yaliyotokea.Na imani yao kwa ukweli wa utume wa Muhamad (s.a.w).
Yakatokea yale waloambiwa na qurani, kwa kunusurika wa-Roma kutokana na ma-Fursi ukadhihiri ukweli wa quran.
C - na katika miujiza ya qurani ni kwamba maajabu makubwa katika umma wa qurani kwa kufuata nakutenda kwa malengo muhimu; mafundisho ya busara ya hali ya juu kabisa kwa umma waqurani:kuongea, kufahamu na kulingania hata ukafika kilele katika ibada, adabu na heshima; hata wakaweza kutanda ulimwenguni. Ambapo kabla ya hapo walikuwa wametengana, wamepotea, wasiojua kusoma wala kuandika; wakabaki mwisho wa mataifa menigine
d - na katika miujiza mikubwa ya qurani ni kuthibiti mambo yaliyofichika kwa kumwamini mwenyezi mungu na kuamini siku ya mwisho na mitume na vitabu....,kwa dalili inayofahamika, haiwezikani ila mtu atakubaliana nayo.
Ama inayohusu sharia, ambayo mwanadamu anaitiwa kwayo, qurani imekuja na sheria ilosifika kama inavyofuata:
1- uadilifu na usawa. uislamu umeamrisha uadilifu na kukatza dhulma. na umeanza kwa kumkataza mwanadamu kudhulumu nafsi yake!!na kwa jumla hukukataza kudhulumu hata hayawani!!
2- ikaja sheria ya kiislamu kuhifadhi haki za mwanadamu na kuhakikisha usalama wa nafsi zao na damu yao na wanachomiliki pamoja na jamii zao, na akili zao na uhuru wao.
3- na imetambulika kwamba, ni sheria kamilifu kwa maisha ya mwanadamu. na sahali mno mwanadamu kuandama. Ina rehema na mapenzi na udugu. na inampeleka mwanadamu kujipamba na tabia njema, kupenda watu na wao kumpenda; na kuishi na wao maisha mazuri.
4 - na katika kuhakikisha kurehemeana baina ya watu. Tajiri anamrehemu fakiri ambaye anahitaji katika mali; akampatia sehemu ya mali yake.na wazazi haki kwa watoto wao.na kwa jirani haki kwa jirani yake kwa uzuri. na kuunganisha kizazi kwa njia nzuri.
5 - hakika mizani bora ya uislamu ni katika kumcha Mwenyezi Mungu. na hii inamfanya kuwa na maisha mema mbele za watu. Ukarimu wa mwanadamu ni katika uchaji wa mwenyezi mungu. na mchango wake katika dini yake ina athari kubwa katika maisha yake na maisha ya wengine pamoja nae, wakishirikiana wote tajiri na fakiri..
6 - sharia ya kiislamu inamwita mtu awe na maisha mazuri, na kumuelekza katika kutafuta elimu na kufanya kazi na kuwapendelea watu analolipendelea nafsi yake.
7 - na kwamba inaleta utulivu katika nafsi za wanadamu. inahuisha akili yake na mwenendo wake na kiwiliwili chake kwenye malengo mamoja ya kumridhisha mola wake aliyetukuka. kwa hivyo utakuta sheria ya kiislam ina vipimo vya maajabu kwa viumbe, na hivi ndivyo anavyobainisha mwanadamu mwema muislamu.
na utakuta katika sababu za kuingia watu katika dini ya kiislamu na imani yao kwa Mtume Muhamad(s.a.w)ambaye ni mjumbe alotumwa kwa watu wote hasa waarabu ambao wengi wao hawakua na elimu ya waja waliotajwa katika vitabu vya mbinguni kuhusu utume wake
utakuta wengi wao waliamini baada ya kubainika miujiza na dalili ya ukweli wa utume wake muhamad (s.a.w).
bali wengi katika waarabu na wengineo, walimfuata Mtume (s.a.w.) baada ya kufariki kwake; juu ya kwamba wengi wao hawakuwa na elimu yu malaika wala mitume. kwa hivyo walipoona uadilifu, na rehema na sheria njema alokujanao, wakamfuata.
walipokuta wema na athari ya ulinganizi wake na tabia njema na baada ya kuwasilisha dalili na thibitisho ya ukweli wa utume wa Muhamad (s.a.w)ya kwamba mwanadamu afanye haraka ya kufuata haki nakumwamini mwisho wa mitume, rehma na amani zimfikie pamoja na mitume wengine wote. ili iweze kupatikana furaha ya dunia na akhera.
Mwenyezi Mungu aseme katika qurani:
(يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءكُمُ الرَّسُولُ بِالْحَقِّ مِن رَّبِّكُمْ فَآمِنُواْ خَيْراً لَّكُمْ وَإِن تَكْفُرُواْ فَإِنَّ لِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ وَكَانَ اللّهُ عَلِيماً حَكِيماً) (النساء : 170 )
" Enyi watu ! mtume amekufikieni kwa haki kutoka kwa mola wenu. basi aminini; itakuwa bora kwenu.
na kama mtakataa basi ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote vilivyomo mbinguni na ardhini mjuzi (na) mnenye hikima.(surat nisaa aya:170).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment