Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Friday, September 17, 2010

Marekani kuishirikisha Syria kusaka amani ya Mashariki ya Kati






AMMAN

Marekani ina mpango wa kuzishirikisha Syria na Lebanon kuzungumza pamoja na Israel kama hatua muhimu ya kuisaka amani ya kudumu ya Mashariki ya Kati kama ilivyoelezwa kwenye makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2002. Kulingana na hati hiyo iliyozinduliwa kwenye kikao cha kilele cha mataifa ya Kiarabu mjini Beirut, Israel itatambuliwa na mataifa yote ya Kiarabu endapo itaondoka kwenye maeneo iliyoyateka nyara mwaka 1967 wakati wa vita vya Mashariki ya Kati ikiwemo Jerusalem Mashariki.

Kauli hizo zimetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton akiwa mjini Amman, baada ya kukutana na Mfalme Abdulla wa Pili wa Jordan. Kwa mujibu wa Bibi Clinton, viongozi hao wamejitolea na wana nia ya kuyatafutia suluhu mambo mazito yanayowakabili.

Akizungumza na waandishi wa habari na mwenzake wa Jordan Nasser Judeh, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton, alisema anaamini kuwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, na Rais wa Mamlaka ya ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas, wanaweza kufanikiwa kutafuta suluhu ya mzozo huo

No comments:

Post a Comment