Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Saturday, September 4, 2010

Ajinyonga Baada ya Kunyimwa Mkopo



Mwanaume mmoja wa nchini Uturuki amejinyonga kwenye mlango wa kuingia kwenye sehemu aliyokuwa akifanya kazi baada ya kunyimwa mkopo na kampuni yake.
Mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la Isa Uguten mwenye umri wa miaka 45, alijinyonga kwenye mlango wa kuingia kwenye uwanja wa klabu ya farasi ya mjini Adana ambako alikuwa akifanya kazi kama mtunza bustani.

Taarifa iliyotolewa ilisema kuwa kutokana na matatizo ya kifedha yaliyokuwa yakimkabili, Isa aliamua kuomba mkopo wa fedha toka kwa kampuni yake ambayo amekuwa akiifanyia kazi kwa miaka 15 sasa.

Hata hivyo kampuni yake ilikataa kumkopesha.

Baada ya kuambiwa hivyo, juzi usiku, Isa aliamua kujinyonga kwenye mlango wa kuingia kwenye viwanja vya klabu hiyo.

Mwili wake uligundulika jana asubuhi ukiwa unaning'ia kwenye mlango.

Polisi waliushusha chini mwili wake na aliposachiwa ilikutwa barua kwenye mfuko wake wa suruali akielezea sababu ya kujinyonga huku akiushushia lawama uongozi wa klabu hiyo.

Mwili wa Isa ulikabidhiwa kwa ndugu zake baada ya kukamilika kwa taratibu za uchunguzi wa maiti.


The Islamic Brotherhood is not based on economic interests, race, or color. It is based on something infinitely superior: Rejection of falsehood and acceptance of the Truth as revealed by the One True God.


When giving commands regarding the Islamic Brotherhood, the Qur'an uses a beautiful style with a profound message. Instead of saying, "greet each other" it says, "greet yourself." [An-Nur 24:61]. Instead of saying, "do not defame each other," it says, "do not defame yourself." [Al-Hujurat 49:11]. Instead of saying, "do not kill each other," it says, "do not kill yourself." [An-Nisaa 4:29]. The message is clear: Whatever is happening to others in the Brotherhood, is actually happening to yourself. Any aggression against any part of the Brotherhood is an aggression against all of it.




Sisi sote ni wa MOLA na kwake tutarejea. Inasikitisha sana.Haya yote ni bcs WAAJIRI WENGI hawafikiri kuwa w'kazi ni binaadamu kama wao, na kwamba hawaishi maisha HALISI "REALY LIFE" Kiasi cha kutofikiria kuwa w'KAZI wanatanzwa na matatizo magumu hata kuliko wao. HATA KUFIKIA HATUA YA KUJINYONGA INAELEKEA JAMAA ALIJIELEZA VYA KUTOSHA LKN ALIKUWA ANAMPIGIA MBUZI GITAA. MOLA AMSAMEHE NA AMUWEKE PEPONI.


Mtoa Maoni:

Wengi wanaojinyonga mara nyingi ni kufikia hatua ya kutokufikiria tena....Hakika haya yanasababishwa na kutegemea kitu ambacho unaweza kupata au kukosa.

Kuwa na malengo ndio ndio uchukue uamuzi sio unalala kesho ukiamka unataka kupata kitu fulani kwa lazima na ukikosa ndio kuiba au kujinyonga.
Mkopo si lazima na ijulikane kuwa si wafanyakazi wote wanaweza kupewa mikopo kwani wengine si watu wa malengo wanpewa mikopo lakini baadae wanakuwa mizigo wa muajili wake."MKOPO SI LAZIMA"


Mtoa Maoni:

Hatua ya kujinyonga si sahihi! angetafuta njia mbadala ya kufikisha ujumbe! Usimsusie Nguruwe shamba, utavuna makapi matupu! Hii ni darubin Bw. UBUGUVU.


Mtoa Maoni:

hivi hawa wanaojinyonga hawaoni utamu wa ugali?


Mtoa Maoni:

Kukimbia ukuonako,na kukimbilia kusikoonekana ni hatua moja ya htr sana aichukuayo mwanadamu.
Hivyo kwa uhakaika gani unayafupisha maisha uliyonayo na kujianzishia maisha ambayo, kwa karibu au mbali utakujaishi?
Ni kweli wa kulaumika huyu?
Wataalamu wa nafsi hawaoni ni kimbilio sahihi la kujiua kwa kuwa,iwapo umejiua kwa kukosa utakacho, hivyo baada ya kifo chako,je utakipata ukitafutacho?
Maamuzi mengine ni htr sn,athari zake ni kubwa sn.
Mungu wasamehe waja kwani hawajui watendalo

No comments:

Post a Comment