Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Wednesday, September 1, 2010

'Osama Bin Laden ni Kibaraka wa Marekani' - Fidel Castro




Osama bin Laden ni kibaraka wa Marekani ambaye anatumiwa na serikali ya Marekani kama njia ya kutoa vitisho vyake, hayo yalisemwa na rais mstaafu wa Cuba, Fidel Castro.
Rais mstaafu wa Cuba, Fidel Castro amesema kuwa Osama bin Laden anafanya kazi CIA na alikuwa akitumiwa na rais wa zamani wa Marekani, George Bush kutangaza vitisho vyake duniani.

Castro alisema kuwa wakati wowote ambao Bush alitaka kutoa vitisho kwa nchi yoyote alimtumia Osama bin Laden kama sababu.

Castro alisema kuwa amejua hayo kwakuwa ameona ushahidi wa maandiko uliotolewa na taasisi ya WikiLeaks ambayo imejipatia umaarufu duniani kwa kutoa taarifa za mambo yaliyofanywa siri.

Castro aliyasema hayo wakati akiongea na mwandishi wa habari wa Lithuania, Daniel Estulin, ambaye anajulikana kwa kuzifanyia uchunguzi taarifa zenye utata.

"Osama anafanya kazi chini ya ikulu ya Marekani, Bush alikuwa na sapoti ya Osama wakati wote", alisema Castro.

"Wakati wowote ambao Bush alitaka kutoa vitisho duniani, alitoa hotuba kuhusiana na Bin Laden akimtaja kuwa anafanya mipango kufanya matukio ya kigaidi".

Castro alisema kuwa maelfu ya kurasa za WikiLeaks zimeweka wazi Al-Qaida wanamfanyia nani kazi.

"Aliyetuthibitishia kuwa Bin Laden ni kibaraka wa CIA ni WikiLeaks, wametoa nyaraka za kuthibitisha hivyo", alisema Castro bila ya kutoa maelezo zaidi kuhusiana na madai yake hayo.







Mtoa Maoni: Ubuguvu Tuesday, August 31, 2010 11:03:29

Osama anachokifanya hakikubaliki kidimi lkn kinakubalika na utawala wa bushi inasikitisha kuona baadhi ya watu wanamshabikia osama kiasi kwamba kama nabii alietumwa na mungu. Osama ndiyo mtu aliouchafulia jina uisilam kwa kushirikiana na media za magharibi kwa masirai ya marekani wakati kuna makundi makubwa ya kujilipu kama Tamils tigers, pkk hayo ndo makundi makubwa duniani ktk secula rists sio al-qaida na hata hivyo suicide haitokani na motivated by religirn


Mtoa Maoni: Red neck Tuesday, August 31, 2010 11:48:34

Kiama kiko karibuni?embu angalieni Pakstain,N
Niger ,Indonesia maji yamejaa kila mahali
Na yanazidi .Indonesia mlima unalipuka watu
Hawana mahali pa kuishi


Mtoa Maoni: JOSE Tuesday, August 31, 2010 11:59:38

Yasemwayo daima yaweza kuwa na ukweli kuwa huyu Osama ni kibaraka wa USA ngoja niwaachie akina UBUGUVU hapa Na MOMS016.

Red Neck tumekupata mzee na baadhi ya hizo web site tunasoma pia ili kupata habari mbalimbali.


Mtoa Maoni: MINA Tuesday, August 31, 2010 13:16:47

SEMY wakilisha hapo mwanawane




Mtoa Maoni: Mangilile Tuesday, August 31, 2010 14:16:52

Osama kamwe hatokuwa kibaraka wa Bush wala CIA. Kila mtu na imani yake, wala hakuna mtu katika Uislamu mwenye haki na uwezo wa kuamua kuwa yeye ndiye mwislamu safi na Osama anaharibu Uislam! Uislam kamwe hauharibiki kwa Mtu au watu! Jambo la msingi ni kusikilizana na Osama na sio kutaka kumkandamiza kwani naye mtu na anao uwezo wa kujitetea! Mara ngapi tumesikia magaidi wameuliwa? ila wakiua wao ndio nongwa? Osama anatetea IMANI yake, na kama humuungi mkono it`s up to u!

No comments:

Post a Comment