Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Friday, March 11, 2011

Watano wafariki wakifuata dawa kwa babu


Watu watano wamefariki dunia na wengine wakijeruhiwa kufuatia ajali ya magari mawili ambayo yalibeba watu waliofuata dawa za babu mchungaji mstaafu Ambilikile Mwasapile ambazo zinadaiwa kutibu magojwa sugu.
Ajali hiyo mbaya ilitokea kwenye wilaya ya Monduli ambapo magari mawili yaliyobeba wagonjwa waliofuata tiba toka kwa babu Ambilikile yaligongana uso kwa uso.

Gari moja lilikuwa limebeba wagonjwa waliokuwa wakirudi makwao baada ya kupata tiba toka kwa babu huku gari jingine lilikuwa limebeba wagonjwa waliokuwa wakienda kupatiwa tiba za babu.

Watu wanne walifariki hapo hapo kwenye eneo la ajali wakati mwingine alifariki hospitalini.

Kamanda wa polisi wa Arusha, Akili Mpwapwa alisema kuwa watu 14 walijeruhiwa katika ajali hiyo na waliwahishwa katika hospitali ya wilaya ya Monduli kwa matibabu zaidi.

Waliofariki walitajwa kuwa ni Raphael Kiboa (65) na mkewe wote toka Lushoto, Tanga, Beatus Moris (36) wa Arusha.

Wengine ni Zakayo Ole Memiri Laizer (45) wa Miserani, Arusha na Ismail Ngozi Mohamed (38) mkazi wa Tabora.

Miili ya waliofariki imehifadhiwa katika hospitali za wilaya ya Monduli na hospitali ya mkoa ya Mlima Meru.






Tahadhari ya mionzi Japan





Japan


Serikali ya Japan imesema, mionzi kutoka kwenye mtambo wa nyuklia wa Fukushima Daiichi uliokumbwa na tetemeko kubwa la ardhi umefikia kiwango cha kuleta madhara.

Onyo hilo lilitolewa baada ya mtambo huo kutikiswa na mlipuko wa tatu, unaoonekana kuharibu mfumo wa kuhifadhi kinu kimojawapo kwa mara ya kwanza.

Iwapo itakuwa imepata ufa, kuna wasiwasi wa kuvuja kwa mionzi zaidi.

Maafisa wameongeza umbali wa eneo la hatari, wakionya wakazi walio ndani ya kilomita 30 kuondoka au kubaki ndani ya nyumba zao.

Baadae serikali ilisema viwango vya mionzi katika lango kuu la mtambo huo vimeshuka.

Mtikisiko huo umechochewa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 9.0 lililotokea Ijumaa iliyopita na tsunami kaskazini-mashariki mwa Japan.

Siku ya Jumanne, kinu nambari 2 kilikuwa cha tatu kulipuka katika kipindi cha siku nne kwenye mtambo huo wa Fukushima Daiichi.

Moto nao ulizuka ghafla katika kinu nambari 4, na kuaminiwa kusababisha kuvuja kwa mionzi.

Kinu nambari 4 kilifungwa hata kabla ya tetemeko hilo kwa ajili ya matengenezo, lakini vyuma vya kinyuklia vya mafuta vilivyotumika bado vimehifadhiwa kwenye eneo hilo.

Katibu wa baraza la mawaziri Yukio Edano alikuwa akingalia kwa makini vinu viwili viliyobaki kwenye mtambo nambari tano na sita, kwani vilianza kupata joto kiasi.

Alisema maji ya bahari ya kupooza yamekuwa yakitiwa kwenye kinu nambari moja na tatu- ambavyo vimekuwa vikirudi katika hali yake ya kawaida- na pia kwenye kinu nambari 2, ambacho hakitabiriki.

Kiwango cha mionzi kwenye mji mkuu wa Japan- umbali wa kilomita 250- kimeripotiwa kuongezeka kuliko kawaida, lakini maafisa wamesema hakuna hatari zozote za kiafya zinazoweza kutokea.

Wakazi wa Tokyo wamekuwa wakikusanya vifaa, huku maduka mengine yakiishiwa na bidhaa kama vile chakula, maji, barakoa na mishumaa.










Mapambano Brega, Libya





Mapigano kati ya jeshi la Libya na waasi yameshika kasi huko mjini Brega.





Waasi mjini Brega, Libya


Wakati mmoja pande zote mbili zilidai kuwa zimedhibiti mji huo.

Magharibi mwa nchi hiyo jeshi la libya lilisogea karibu na mji wa Zuwara na pia kulishambulia mji wa Misrata.

Jumuiya ya nchi nane tajiri duniani G8 imetoa wito kuchukuliwa hatua dhidi ya Kanali Muammar Gaddafi lakini hawakutaja marufuku ya ndege kutopaa katika anga ya Libya.

Afisa mmoja kutoka Umoja wa Mataifa ametoa wa kukomesha mashambulio dhidi ya waandamanaji na kuzingatia kuwepo na uwezo wa kutoa huduma za kibinaadamu.

Ndege za serikali zimekuwa zikiyashambulia kwa mabomu maeneo ya mipakani ya mji wa Ajdabiya.

Kulingana na taarifa kutoka AFP, milio ya miripuko yalisikika yakiongezeka mjini humo na huduma za dharura za kuwaondo majeruhi mjini humo na kuwapeleka hospitalini zimeongezeka.








Waziri ajiuzulu nchini Uganda









Waziri Buturo alihama chama twala NRM baada kushindwa kwenye kura za mchujo
Aliyekuwa waziri wa maadili nchini Uganda, Dr Nsaba Buturo amejiuzulu wadhfa wake kufuatia uamuzi wa mahakama ya kikatiba nchini humo.

Mahakama hiyo imeamuru kuwa wanasiasa wanaohama vyama vyao vya kisiasa na kujiunga na vingine wakiwa bado wanahudumu kama wabunge wafutwe kazi.

Katiba ya sasa nchini Uganda inasema kuwa mbunge yeyote akitaka kuhama CHAMA chake na kujiunga na kingine ni sharti ajiuzulu kwanza wadhfa wake na uchaguzi mdogo kuandaliwa.

Dr Buturo alisema, "kilichobakia kwangu kilikuwa kuondoka afisini na heshima yangu yote."

Chini ya sheria mpya, ambayo ingawa ipo-haijatekelezwa, zaidi ya Wabunge 70, kukiwemo Mawaziri tisa wanapaswa kujiuzulu, sio tu Uwaziri lakini pia viti vyao vya Bunge.

Wanasiasa hao wakitaka kurejea tena Bungeni watagombea upya viti vyao kupitia vyama vyao vipya.









Maharamia wahukumiwa Marekani



Maharamia wahukumiwa kifungo cha maisha katika mahakama ya marekani.

Mharamia wa kisomali


Wasomali watano wamehukumiwa kifungo cha maisha kwa kuishambulia manuwari ya jeshi la wanamaji la Marekani waliodhani ni manuwari ya bidhaa.

Wanaume hawo watano walipatikana na hatia mwezi Novemba kwa kujaribu kuiteka nyara manuwari ya USS Nicholas iliyokuwa katika operesheni ya kudhibiti tatizo la maharamia.




Mawakili wa upande wa utetezi wamedai kuwa watu hao walikuwa mateka na walilazimishwa kufyatua risasi wakati waliposhambuliwa mwezi Aprili.

Waendesha mashtaka walisema hii ni mara ya kwanza watu kuhukumiwa katika kesi ya maharamia na jopo la mahakama la marekani tangu mwaka 1820.












Issoufou ashinda uchaguzi wa urais Niger


Tume ya uchaguzi nchini Niger imetangaza kuwa kiongozi wa upinzani nchini Niger Mahamadou Issoufou ameshinda uchaguzi wa urais kwa asilimia 58 ya kura

Mahamadou Issoufou


Bw Issoufou aliwahi kushindwa na aliyekuwa rais, Mamadou Tandja, mara mbili katika uchaguzi za hapo awali.

Seini Oumarou mgombea wa kiti cha urais kutoka chama cha MNSD ambacho ni chama cha Bw Tandja, alipata kura aslimia 42.

Uchaguzi huo inatazamiwa kurudisha hali ya utawala wa raia katika nchi hiyo.





Wafuasi wa Gbagbo washambuliwa


Wafuasi wa Alassane Outtara wamewashambulia wafuasi wa rais Laurent Gbagbo katika mji mkuu wa Abidjan nchini Ivory Coast.


Mfuasi wa Ouattara


Milio ya risasi zilisikika Jumatatu tarehe 14 jioni katika wilaya mbili zilizoko karibu na kambi la jeshi.

Mwandishi wetu wa BBC, John James, aliripoti kuwa tukio hilo litachochea mzozo unaoendelea nchini humo bila kuipelekea nchi hiyo kuingia katika hali ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Rais Gbagbo amekataa kuachia madaraka ilhali Bw Ouattara anatambuliwa na wengi kuwa ndiye aliyeshinda uchaguzi wa urais mwaka jana.

Hii ni mara ya kwanza ya kuzuka mapigano katika kitongoji cha Yopougon ambacho kinamuunga mkono Bw Gbagbo, na kile cha Adjame cha wafuasi wa Bw Ouattara.

Mwandishi wetu alisema hakuna uhakika kama wafuasi wa Ouattara wamepiga hatua au wamekuwa tu wakitekeza mashambulio katika maeneo ambayo wana uashawishi mkubwa

No comments:

Post a Comment