Mashabiki wa mpira Bamako, Mali
Maelfu ya raia wa Mali walijitokeza kuishangilia timu ya Libya katika kufuzu kwa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwenye mji mkuu wa Mali.
Mashindano hayo yalifanyika Bamako kutokana na sababu za kiusalama nchini Libya.
Takriban raia 20,000 wa Mali walijitokeza kushuhudia shindano hilo, wengi wakiwa wamebeba mabango wakipinga uvamizi unaofanywa na nchi za magharibi nchini Libya.
Kapteni Tariq Ibrahim al-Tayib aliiambia BBC baada ya kuichapa Comoro mabao 3-0, "Tumeguswa sana na watazamaji wa Mali"
Mwandishi wa habari aliyopo Bamako Martin Vogl alisema serikali ya Mali ina uhusiano wa karibu na kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi na huungwa mkono sana nchini humo.
Baada ya kila goli katika shindano hilo lililofanyika siku ya Jumatatu jioni, mashabiki hao walikuwa wakiita: "Gaddafi! Gaddafi!," alisema.
Bw Tayib alisema wachezaji wengi hawakuweza kucheza kwasababu walikuwa wanaishi Benghazi, mji ulioshikiliwa na majeshi yanayopambana na Kanali Gaddafi.
Lakini alisema hakuna mgawanyiko wowote wa kisiasa upande wa timu ya soka ya taifa.
Alisema, "Timu nzima inamwuunga mkono Muammar Gaddafi".
Siku ya Ijumaa, maelfu ya Walibya walipita mitaa ya Bamako kuonyesha nia yao ya kumwuunga mkono kiongozi huyo wa Libya- wakiandamana kuelekea kwenye mabalozi ya Ufaransa na Marekani kupinga nchi hizo kujihusisha katika harakati za kijeshi dhidi ya Kanali Gaddafi.
Majeshi ya Gaddafi yawazidi nguvu waasi
Askari wanaomtii Kanali Gaddafi mjini Misrata
Majeshi yanayoiunga mkono serikali yamezidi kuwashambulia waasi nchini Libya, nahivyo kuwalazimu kurejea nyuma katika mji wa Bin Jawad.
Mapigano hayo mapya yameibuka baada ya wajumbe kutoka nchi mbalimbali kukutana mjini London kwenye mkutano wa kujadili mipango ya usoni ya Libya.
Awali Rais wa Marekani Obama alijitetea kwa kufanya uamuzi wa kuidhinisha harakati za kijeshi kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani, akisistiza Marekani imejihusisha kwa kiwango kidogo.
Lakini pia alisema kumwondoa Kanali Gaddafi kwa nguvu ni kosa.
Majeshi yanayompinga Kanali Gaddafi yamesogea sana upande wa magharibi kutoka kwenye ngome yao ya Benghazi katika siku za hivi karibuni- wakisaidiwa sana na mashambulio ya anga ya kimataifa- yakiteka idadi kadhaa za jamii za kipwani na mitambo muhimu ya mafuta, ikiwemo Ras Lanuf, Brega, Uqayla na Bin Jawad.
Obama atetea uamuzi wa kumshambulia Gaddafi
Rais Barack Obama.
Obama atetea uamuzi wa kumshambulia Gaddafi ili kuepusha mauaji halaiki
Obama asema utawala wake umechukua hatua za kijeshi ili kuepusha maangamizi ya raia nchini Libya
Rais Obama ameutetea uamuzi wa utawala wake wa kumshambulia Kanali Gaddafi. Amesema hatua hiyo ilikuwa ya lazima ili kuzuia mauaji halaiki.
Wakati huo huo wajumbe kutoka nchi zaidi ya 40 leo wanakutana mjini London kujadili njia za kuutatua mgogoro wa Libya
Rais Obama amewaambia wananchi wake kwamba Marekani imezuia mauaji halaki nchini Libya. Rais Obama alieleza hayo katika hotuba aliyoitoa kwenye Chuo Kikuu cha kijeshi mjini Washington na kutangazwa moja kwa moja na televisheni. Amesema laiti jumuiya ya kimataifa inengelisuasua kwa siku hatamoja zaidi tu , pangelitokea mauaji halaiki katika mji wa Benghazi.
Amesema endapo Marekani ingeendelea kusubiri mauaji halaiki yangelitokea katika mji huo na kuliathiri eneo lote, na yangelizisakama nafsi za watu duniani kote.Amesema kuacha mauaji yatokee kusingelingana na maslahi ya Marekani.
Rais Obama ameeleza kwua kama Rais wa Marekani, hakutaka kusubiri kuona picha za maangamizi na makaburi ya jumuiya bila ya kuchukua hatua.
Hata hivyo Rais huyo ameonya vikali dhidi ya kujaribu kumwondoa Gaddafi kwa kutumia nguvu. Amesema kufanya hivyo kutakuwa kurudia mauaji yaliyotokea nchini Iraq.Obama ameeleza kuwa mnamo muda wa mwezi mmoja tu, Marekani imeshirikiana na washirika wake wa kimataifa katika kujenga mfungamano mkubwa na kuweza kupewa jukumu na jumuiya ya kimataifa la kuwalinda raia nchini Libya.
Lakini amesisitiza kwamba lingekuwa kosa kulitelekeza jukumu hilo kwa lengo la kuleta mabadiliko ya utawala nchini Libya.Ameeleza kuwa kuzipanuza operesheni za kijeshi ili kumwangusha Gaddafi kungelikuwa kosa
Wakati huo huo wajumbe kutoka nchi zaidi ya 40 wanakutakana mjini London leo kujadili njia za kuutatua mgogoro wa Libya.Mkutano huo utahudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki -Moon, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kuihami ya NATO Anders Fogh Rasmussen na wajumbe wa Umoja wa nchi za Kiarabu.
Muda mfupi kabla mkutano huo kuanza, Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa waliwasilisha mada inayotoa mwito wa mwanzo mpya nchini Libya.Sarkozy na Cameron wametoa mwito kwa wafuasi wa Gaddafi kuwataka watengane na kiongozi huyo.
Hata hivyo mkutano wa mjini London unafanyika bila ya Urusi ambayo haikualikwa.Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Sergei Lavrov hatahudhuria mkutano huo kwa sababu nchi yake siyo sehemu ya mfungamano
wa kimataifa unaochukua hatua za kijeshi dhidi ya Kanali Gaddafi.
Hapo awali waziri Lavrov aliyakosoa mataifa yanayoishambulia Libya kwa kuvuka mipaka ya yale yaliyopitishwa katika azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Waasi nchini LibyaTaarifa kutoka Libya zinasema waasi wamevisambaaratisha Vikosi vinavyomuunga mkono,Kiongozi wa Libya Muammer Gaddafi pamoja na vifaru.
Taarifa za sasa zinasema zaidi ya watu 142 wamepoteza maisha na wengine zadi ya 1400 kujieruhiwa wakiwemo wengine 90 wakiwa katika hali mbaya.
Hivi sasa vikosi vya wanajeshi wanaomtii kanali Gaddafi vimeweka kambi katika eneo moja mjini Misrata lililopo mashariki mwa mji wa Tripoli.
Akizungumza kwa masharti ya kutotajwa jila lake muasi mmoja anasema, vikosi hivyo kwa hivi sasa vinajiandaa kufanya mashambulizi dhidi yao.
Amedai hivi sasa Misrata ipo katika tishio la kutokea mauwaji ya haraiki na kuongeza kwamba kile kilichozuiwa Benghazi na vikosi vya muungao kitarajiwe kutokea eneo hilo.
Mtu mwingine ambae ni daktari,amesema katika mapigano yaliyotokea leo mjini Misrata watu wanne wamepoteza maisha.
File:US Navy 051206-N-3488C-021 Fire Controlmen stabilize a RIM-7 NATO Sea Sparrow missile container as it is lifted to the flight deck aboard the conventionally powered aircraft carrier USS Kitty Hawk (CV 63).jpg
Waasi wa Libya wakishangiliaKutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya majeruhi hivi sasa kuna matarajio kwa meli Kituruki kwenda kuchukua majeruhi takribani 50 katika eneo hilo kwa matibabu zaidi.
Awali msemaji wa Waasi,Shamsidin Abdulmolah amesema meli hiyo,ambayo ina hospitali ndani yake, inayosindikizwa na vikosi vya NATO itachelwa kuwasili mjini Misrata.
Kuwasili kwa meli hii kulitanguliwa na meli nyingine kubwa iliyobeba misaada ya vyakula, maziwa na vitu vingine muhimu kwa binadamu.
Katika hatua nyingine, serikali ya Libya leo iliwapeleka Waandishi wa habari kwenda kujionea mambo yalivyo katika eneo hilo,tukio ambalo lilioneshwa moja kwa moja na televisheni ya taifa ya nchi hiyo.
Hata hivyo, baadhi ya Waandishi, wamesema hawakupelekwa eneo la kati la mji ambako kulionekana dhahiri mapigano yanaendelea kutokana na kutanda kwa moshi mzito.
Waasi wanadai vikosi vinavyomtii,Gaddafi vimesababisha kaya zaidi ya elfu tano bila ya makazi na kuongeza kuwa hivi sasa vinashikilia eneo la kaskazini la Misrata.
Kauli zinapishana katia ya Waasi na Serikali ya Libya ambapo serikali inasema vikosi vyake vimesimamisha mashambulizi mjini humo na kwamba hivi mji upo mikononi mwao na umekuwa shwari kabisa.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Shirika la Habari la Libya, inadai kikosi cha kupambana na ugaidi kimesitisha mashambulizi dhidi ya raia yaliyokuwa yakifanywa na magaidi.
Katika tukio lingine televishen ya Taifa ya Libya, iliyokuwa ikitangaza moja kwa moja katia makazi ya Gaddafi mjini Tripoli mapema,imemuonesha mtoto wa kiongozi huyo Hamis ambae ilitangazwa kuwa amefariki baada ya kujeruhiwa na makombora ya majeshi ya Muungano.
Majeshi ya Muungano yalianza operesheni za kuzuia ndege kuruka nchini Libya machi 19 kwa shabaha ya kuwanusuri wananchi na mashambulizi ya serikali ya nchi hiyo ambayo hata hivyo yametoa fursa kwa Waasi kusonga mbele.
1I/AAAAAAAAMnM/e5FimWzXbro/s320/NATO_Sea_Sparrow_missile_container_as_it_is_lifted_to_the_flight_deck_aboard_the_conventionally_powered_aircraft_carrier_USS_Kitty_Hawk_%2528CV_63%2529.jpg" />
No comments:
Post a Comment