Dini ni mfumo wa maishani
Thursday, March 10, 2011
Congo ya ruhusu uchimbaji wa madini
Waasi mashariki mwa nchi hiyo wanatumia faida ya madini kufadhili shughuli zao
Utawala wa Rais Joseph Kabila umeruhusu tena shughuli za kuchimba madini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo baada ya kipindi cha miezi sita.
Rais Kabila aliweka marufuku hiyo ili kudhibiti biashara ya magendo ambayo imesababisha serikali kukosa kipato kutoka utajiri wake wa madini.
Uchimbaji na mauzo haramu ya madini hayo pia umekuwa ukichochea utovu wa usalama katika mikoa ya Kivu kaskazini na Kusini.
Waziri wa madini nchini humo, Martin Kabwelulu amesema kuwa harakati za kuwadhibiti waasi katika eneo hilo na mikakati ya serikali ya kuimarisha usimamizi wa shughuli za kuchimba madini ndio zimechangia marufuku hiyo kuondolewa.
Viongozi katika maeneo husika wameshirikishwa katika mikakati hiyo kuhakikisha kuwa utawala wa mikoa pia unafaidi kutoka kwa wawekezaji watakao sajiliwa kuchimba madini nchini humo.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inautajiri mkubwa wa madini yakiwemo, dhahabu, almasi na Kobalti yenye thamani kubwa kwenye soko la kimataifa.
Wiki iliopita Rais Kabila na mwenzake wa Kenya Mwai Kibaki walizindua tume ya pamoja itakayo endesha harakati za kudhibiti biashara ya magendo ya dhahabu.
Uchunguzi umeonyesha kuwa mtandao wa biashara hiyo ya magendo unaendesha shughuli zake nchini Kenya.
Mauzo ya bidhaa nje ya Ujerumani yaongezeka
Mauzo ya bidhaa nje za Ujerumani yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 24 mwezi Januari mwaka huu ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka mmoja uliopita. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na ofisi ya kitaifa ya takwimu hapo jana, kuna dalili ya kuendelea kuimarika kwa uchumi wa Ujerumani. Thamani ya mauzo ya bidhaa nje ya nchi ya mwezi Januari ilipanda hadi kufikia Euro bilioni 78.5, huku bidhaa zilizoagizwa kutoka nje zikiongezeka kwa asilimia kama hiyo hadi kufikia Euro bilioni 68.
Ujumbe wa Gbabo wakataa pendezo la Umoja wa Afrika
Ujumbe wa kiongozi anayeng'nga'nia madaraka nchini Cite d'Ivoire, Laurent Gbagbo, umelikataa pendekzo la jopo la Umoja wa Afrika kuutanzua mzozo wa kisiasa unaoikabili nchi hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Addis Ababa leo baada ya kikao maalumu cha marais watano wa Afrika cha kumfahamisha uamuzi wake kiongozi anayetambulika kimatiafa kama mshindi wa uchaguzi wa Novemba 28 mwaka jana, msemaji wa ujumbe huo, waziri mkuu wa zamani wa Cote d'Ivoire, Pascal Affi, N'Guessan, amesema ikiwa pendekezo hilo halitazaa matunda, basi Umoja wa Afrika kwa njia moja au nyengine utakuwa unachangia kukamilisha mapinduzi yaliyoanza mnamo mwaka 2002 yaliyogeuka mapinduzi ya kura kupitia uchaguzi wa mwaka jana. Ouattara, anahudhuria mkutano wa Addis Ababa lakini rais Gbagbo amebaki Abidjan, badala yake kutuma ujumbe wake.
China yatoa tamko kuhusu Dalai Lama kujiuzulu
China imesema leo kwamba kiongozi wa kiroho wa Tibet, Dalai Lama, anafanya ujanja kwa kutangaza atajiuzulu kama kiongozi wa kisiasa wa serikali ya Tibet iliyo uhamishoni. Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa China, Jiang Yu, amewaambia waandishi wa habari mjini Beijing kuwa kiongozi huyo amekuwa akilizungumzia suala hilo katika miaka michache iliyopita na anadhani ni ujanja wa kuihadaa jumuiya ya kimataifa. Msemaji huyo amesisitiza kuwa serikali ya Tibet iliyo uhamishoni ni kundi haramu la kisiasa na hakuna nhci inayolitambua. Katika hotuba yake leo kwenye maadhimisho ya kushindwa kwa mapinduzi dhidi ya utawala wa China mnamo mwaka 1959, Dalai Lama amesema atataka kufanyike mageuzi ya kisheria kumruhusu ajiuzulu kutoka kwa majukumu yake ya kisiasa wakati wa kipindi kijacho cha bunge la Tibet baadaye mwezi huu. ODalai Lama hata hivyo ataendelea kubakia kiongozi wa kiroho wa Tibet.
Vikosi vya Ujerumani lawamani kwa kumuua mwanamke wa Afghanistan
Wanajeshi wa Ujerumani Afghanistan
wa
Polisi wa mkoa wa Kunduz kaskazini mwa Afghanistan wamevishutumu vikosi vya Ujerumani kwa kumuua kwa bahati mbaya mwanamke mmoja n akumjeruhi mwengine kwenye mapamgano ya risasi katika eneo hilo. Kwa mujibu wa mkuu wa jeshi la polisi mkoani humo, tukio hilo lilitokea jana wakati kikosi cha doria cha Ujerumani kiliposhambuliwa katika wilaya ya Chahar Dara, na kikajibu shambulizi hilo kwa kufyatua risasi. Msemaji wa vikosi vya Ujerumani huko Kunduz, luteni kanali Klaus Geier, amesema hawezi kuthibitisha kifo cha mwanamke huyo raia wa Afghansitan. Amesema mama huyo aliyekuwa na jeraha kichwani, baadaye alikabidhiwa kwa madaktari wa Kijerumani, lakini akaaga dunai hospitalini. Msemaji huyo aidha amesema jeraha la mwanamke huyo halikusababishwa na risasi. Tukio hilo kwa sasa linachunguzwa.
NATO na Umoja wa Ulaya zaijadili Libya
Mawaziri wa ulinzi wa Jumuiya ya kujihami ya NATO wamekutana leo mjini russels Ugbelgiji kujadili hatua za kuchukua ndani na nje ya Libya, huku maafisa wakisema muungano huo unaweza kutumika tu kwa kuungwa mkono na jumuiya ya kimataifa. Viongozi wa NATO na wa Umoja wa Ulaya leo wameanza mazungumzo ya siku mbili kuhusu Libya. Mkutano huo unafanyika huku mapigano makali yakiendelea nchini humo kati ya waasi na vikosi vinavyomtii kiongozi wa Libya, kanali Moammar Gaddafi. Ripoti kutoka Libya zinaashiria kwamba vikosi vya serikali vimesonga mbele na kuyateka maeneo yaliyokuwa yakidhibitiwa na waasi, ikiwemo miji ya Ras Lanuf, Bin Jawad na Zawiyah. Makundi ya waasi hayana silaha madhubuti kuweza kujilinda kutokana na mashambulizi ya angani yanayofanywa na ndege za Gaddafi, ambazo jana zilikishambulia kituo kikubwa cha mafuta.
Ujerumani yafunga akaunti za benki za Libya
Ujerumani imezifunga akaunti za benki zinazomilikiwa na benki kuu ya Libya na mfuko wa mali za taifa hilo. Wizara ya uchumi imesema hatua hiyo inaziathiri akaunti 193 katika benki 14 za Ujerumani, ikiwemo benki kuu ya Ujerumani, zenye thamani ya zaidi ya Euro bilioni 50. Akizungumza juu ya uamuzi huo, waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani, Guido Westerwelle, amesema:
Hatua ya kuzifunga akaunti hizo imechukuliwa kabla kufanyika mkutano wa kilele wa mawaziri wa mambo ya nchi za kigeni wa Umoja wa Ulaya, unaotarajiwa kumtaka kiongozi wa Libya, kanali Moammar Gadafi ajiuzulu. Kwenye taarifa yao ya pamoja mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Bi Cathrene Ashton, waziri wa kigeni wa Uingereza na wa Ujerumani wameutaka Ulaya kutoshirikiana na Gadafi na wamtake ajiuzulu.
Mapenzi na Mganga Yasababisha Moto Uliolitekeza Ghorofa Marekani
Moto uliolitekeza ghorofa moja nchini Marekani na kupelekea kifo cha mtu mmoja na watu wengine 100 kukosa makazi ulisababishwa na mwanamke aliyekuwa kwenye tamasha la ngono na mganga.
Mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina lake wa Brooklyn, New York nchini Marekani alimlipa mganga dola 300 ili amuondolee matatizo yanayomkabili.
Mganga huyo naye katika mojawapo ya masharti yake alimtaka mwanamke huyo wafanye mapenzi kwenye kitanda kilichozungukwa na mishumaa, limeripoti gazeti la New York Post.
"Alimwaga pombe iliyotengenezwa kwa miwa kwenye sakafu eneo la mlangoni ili kuzuia mapepo wabaya kuingia ndani, na ili dawa za uganga zifanye kazi, mganga alimtaka mwanamke huyo wafanye mapenzi", liliambiwa gazeti la New York Post.
Huku malavi davi yakiwa yamenoga, kukuru kakara za malavi davi zilipelekea baadhi ya mishumaa kudondoka chini na matokeo yake kuzusha moto mkubwa.
Mganga alijaribu bila mafanikio kuuzima moto huo kwa kutumia maji toka bafuni lakini moto huo ulipozidi kupamba moto mganga na mwanamke huyo walikimbia toka kwenye chumba chao kilichokuwa ghorofa ya nne na kuuacha mlango wazi.
Upepo uliokuwa ukivuma kwa spidi ya kilomita 65 kwa saa uliufanya moto huo uzidi kuwa mkubwa na kuenea kwenye vyumba vingine.
Moto huo uliziteketeza pia vyumba vya ghorofa ya nne na tano na kupelekea paa la jengo hilo kuporomoka.
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 62, aliyekuwa akiishi ghorofa ya sita alifariki kutokana na moto huo.
Jumla ya wafanyakazi 200 wa mashirika 44 tofauti ya zimamoto walishiriki kuuzima moto huo na kuuzuia usifike kwenye majengo ya jirani.
Wafanyakazi 25 wa zimamoto walijeruhiwa katika harakati za kuuzima moto huo
Gaddafi asema Walibya wako tayari kufa kumlinda
Gaddafi (kushoto)akisalimiana na Christiane Amanpour wa kituo cha habari cha ABC, mjini TripoliMatamshi yake yamekosolewa vikali na balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa akisema Gaddafi yuko mbali mno na ukweli halisi wa mambo nchini Libya
Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi amesisitiza kuwa raia wake wote wanampenda, hivyo kupuuza shinikizo la kimataifa linalozidi kumtaka aondoke madarakani na pengine akimbilie uhamishoni baada ya kuiongoza nchi hiyo kwa miongo minne. Katika mahojiano yake hapo jana na televisheni ya ABC, BBC na gazeti la The Times la jijini London, Gaddafi amesema Walibya wako tayari kufa kwa ajili ya kumlinda na kusisitiza hakuna anayempinga. Gaddafi amedai hakuna maandamano yoyote mabarabarani.
Matamshi ya kiongozi huyo yamelaaniwa vikali na balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan Rice.
Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan Rice
Akizungumza katika ikulu ya Marekani mjini Washington, Bi Rice amesema matamashi hayo yanadhihirisha kwamba Gaddafi hafai kuongoza na amejitenga na ukweli halisi wa mambo. Wakati huo huo, Marekani imeanza jana kupeleka meli zake za kivita na ndege karibu na Libya. Marekani pia imezuilia mali za Libya za thamani ya dola bilioni 30 kumshinikiza Gaddafi aondoke madarakani.
Hatma ya Ivory Coast itajulikana leo
visa vya ghasia kati ya wafuasi wa viongozi hawa wawili vinaongezeka mjini Abidjan
Baraza la usalama la Umoja wa Afrika linakutana mjini Addis Ababa, Ethiopia kujadili hatua za kuchukuliwa baada ya juhudi za upatanishi nchini Ivory Coast kushindikana kwa mara nyingine.
Bw Alassane Outarra ambaye anatambulika kama mshindi wa uchaguzi uliofanyika Novemba mwaka jana, kwa mara ya kwanza amesafiri kutoka nchini humo kuhudhuria mkutano huo.
Lakini Rais Laurent Gbagbo ameususia na badala yake amemtuma kiongozi wa chama chake Bw Pascal Affi N'Guessan.
Baraza hilo litajadili ripoti ya jopo la viongozi watano walioteuliwa na Umoja huo kuongoza duru hii ya upatanishi kabla ya kutoa uamuzi wa hatua za kuchukuliwa kusuluhisha mzozo huo.
Jopo hilo linaongogzwa na Rais wa Mauritania Mohammed Ould Abdel Aziz. Wengine ni Jakaya Kikwete wa Tanzania, Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Idriss Deby wa Chad na Blaise Compaore wa Burkina Faso.
Awali Umoja wa Afrika,ulitishia kutumia nguvu za kijeshi kumondoa Bw Gbagbo ambaye amekataa kuachia wadhifa wa urais.
Athari za vikwazo vya kiuchumi vilivyowekewa utawala wa Gbagbo zimeanza kusikika. Duru zinasema serikali sasa imeshindwa kulipa mishahara ya watumishi wa umma wakiwemo wanajeshi.
Kesi ya Taylor ni 'ukoloni mamboleo'
Bw Charles Taylor
Wakili wa aliyekuwa Rais wa Liberia Charles Taylor alisema upande wa mashtaka umegeuza kesi yake ya uhalifu wa kivita katika " mfumo wa ukoloni mamboleo wa karne ya 21."
Courtenay Griffiths aliyasema hayo katika hitimisho ya utetezi wake kwenye mahakama maalum ya umoja wa mataifa ya Sierra Leone huko the Hague.
Bw Taylor ni aliyekuwa kiongozi wa kwanza barani Afrika kukabiliwa na kesi kama hii ya kimataifa.
Amekana kuhusishwa na mashtaka 11, ikiwemo mauaji, ubakaji, na kutumia watoto kuwa maaskari wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe Sierra Leone.
Anatuhumiwa kwa kuwapa silaha na kuwaongoza waasi wa Revolutionary United Front (RUF) wakati wa harakati za ugaidi kwa kipindi cha miaka 10 uliofanywa kwa kiwango kikubwa dhidi ya raia.
RUF ilivuma kwa sifa zake mbaya za kukata viungo vya mwili vya raia, na kutumia ubakaji na mauaji kutishia watu.
'Kwanini siyo Gaddafi?'
Katika hitimisho la upande wa utetezi, Bw Griffiths aliwaambia majaji kuwa wote watendewe haki sawa.
Aliuliza kwanini kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi hayumo kwenye mahakama hiyo.
Alisema ni kwasababu serikali ya Uingereza iliyoongozwa na aliyekuwa waziri mkuu Tony Blair alitaka kufanikisha azma zake za kiuchumi na Libya.
Naomi Campbell
Wakili huyo wa utetezi pia alisema kwamba hakuna aliyeshughulikia kesi hiyo mpaka mwanamitindo maarufu Naomi Campbell na muigizaji wa Hollywood walipojitokeza, na tangu wakati huo ikabadilika kuwa kama haipo tena.
Bi Campbell na muigizaji Mia Farrow waliitwa kutoa ushahidi katika kesi hiyo mwezi Agosti.
Upande wa mashtaka ulikuwa ukijaribu kuweka uhusiano baina ya Bw Taylor na almasi ambazo hazikukatwa ambapo Bi Campbell alisema aligaiwa alipokuwa Afrika Kusini mwaka 1997.
Bw Taylor anatuhumiwa kuuza "almasi haramu zinazotumika kugharamia vita " kwa ajili ya waasi, ili na wao wapate silaha.
Upande wa utetezi ulisema Bw Taylor alijaribu kuleta amani Sierra Leone baada ya kuombwa na nchi jirani.
Kesi hiyo, inayofikia hatua za mwisho, ilicheleweshwa kwa wiki kadhaa kutokana na tofauti za kisheria, lakini wiki iliyopita upande wa utetezi ulishinda rufaa yake ili kutoa hitimisho.
Mwisho ilikuwa iwe Januari kwasababu ulisema ushahidi mpya uliibuka.
Mahakama maalum ya umoja wa mataifa ya Sierra Leone the Hague imesikiliza maelezo kutoka kwa zaidi ya mashahidi 100.
Kesi hiyo tayari imedumu kwa zaidi ya miaka mitatu na majaji wanatarajiwa kutoa uamuzi baadae mwaka huu.
Kama atakutwa na hatia, Bw Taylor atatumikia kifungo chake gerezani nchini Uingereza.
Huyu Naye ni Gaidi
Mwanamgambo mmoja wa kundi la Taliban nchini Afghanistan amekuwa maarufu ghafla duniani baada ya video yake kuingia kwenye mitandao dunini, mgambo huyo ni mfupi sana kiasi cha kwamba bunduki aliyoibeba inamzidi urefu, amebatizwa jina la 'Mini Osama bin Laden'.
Akiranda randa kwenye mojawapo ya kambi ya Taliban huku akiwa ameibeba bunduki aina ya kalashnikov, mgambo huyo amekuwa gumzo kwenye mitandao duniani.
Kutokana na ufupi wake huenda hata bunduki aliyoibeba ikawa imemzidi urefu.
Mgambo huyo ambaye jina lake halijapatikana amebatizwa jina la kiongozi wa Al- Qaeda, Osama bin Laden ambapo amekuwa akiitwa "Mini Osama bin Laden".
Gaddafi azidisha mashambulizi dhidi ya waasi
Kiongozi wa Libya, Muammar GaddafiVikosi vitiifu kwa kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi, vikiyashambuliwa maeneo yanayoshikiliwa na waasi, huku Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO), ikiondoa uwezekano wa kuivamia nchi hiyo kijeshi kwa sasa.
Moshi mzito mweusi uliochanganyika na miale ya moto umeonekana kutanda katika anga la mji wenye mitambo ya mafuta wa Es Sider ulio mashariki mwa Libya leo hii (Jumatano 09.02.2011).
Bado hakuna chanzo huru cha habari kilichothibitisha nani aliyefanya mashambulizi hayo, lakini inafahamika kuwa, Es Sider ni miongoni mwa miji inayoshikiliwa na waasi, na ambapo vikosi vitiifu kwa Muammar Gaddafi, vimekuwa vikipigana kuirudisha mikononi mwa serikali.
Mpiganaji wa upande wa waasi, Abdel Salam Mohammed, ameliambia shirika hilo na hapa namnukuu: "Hapa tulipo tumesimama kwenye muelekeo wa Es Sider. Yalikuwa na mashambulizi makali ya mabomu dhidi yetu na kisha yakapiga matangi ya kuhifadhia mafuta."
Mpambe wa Gaddafi atua Cairo
Mripuko katika mji wa Mashariki wa Libya Wakati hali ikiendelea hivyo ndani ya Libya, huko nchini Misri kuna ripoti kuwa mmoja wa watu wa karibu wa Gaddafi, Abdelrahman al-Zawi, amewasili uwanja wa ndege wa Cairo, huku mkutano wa mawaziri wa nje wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, ukitarajiwa kukutana mjini humo, kujadili uwezekano wa kuiwekea Libya vikwazo vya anga.
Bado haijulikani dhamira ya al-Zawi kutua ghafla nchini Misri, lakini huenda ni kuwasilisha ujumbe wa Gaddafi, ambaye hapo jana alionya kuwa, hatua yoyote ya kulifunga anga la Libya, itachukuliwa kuwa ni vita ambavyo nchi yake itavijibu inavyostahiki.
Hatua hiyo, ambayo pia inapigiwa chapuo na Uingereza, Ufaransa na Marekani, inatazamiwa kuzuia mashambulizi ya vikosi vya Gaddafi dhidi ya wapinzani wake, lakini haitoshi kuzuia umwagikaji damu unaoendelea nchini humo.
Katibu Mkuu wa NATO, Fogh RasmussenKwa upande mwengine, Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi, NATO, imesema kwamba haitarajii kuivamia Libya kijeshi, ingawa haikuondoa uwezekano wa hatua nyengine kutumika dhidi ya utawala wa Gaddafi.
Akizungumza na kituo cha habari cha Sky News cha Uingereza leo hii, Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Fogh Rasmussen, amesema kwamba jumuiya yake haikusudii kujiingiza kijeshi nchini Libya, lakini iko tayari kuchukua hatua yoyote itakayostahiki, kama dharura ya kufanya hivyo itajitokeza.
"Ikiwa tutaombwa na ikihitajika, tunaweza kupatikana katika dharura hata ya muda mfupi. Kuna mambo mengi mazito katika eneo hili kuhusiana na uwezekano wa uingiliaji kati wa majeshi ya kigeni." Amesema Rasmussen
Ujerumani yaamini vikwazo vya anga si njia pekee
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Thomas de Maiziere Naye Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Thomas de Maiziere ametaka mjadala wa kuwekwa marufuku ya ndege kuruka kwenye anga ya Libya kuchukuliwa kwa tahadhari, akisema kwamba hiyo ni moja tu kati ya hatua nyingi ambazo zinaweza kuchukuliwa, na wala sio hatua pekee.
Katika miaka ya 1990, jeshi la anga la Ujerumani lilikuwa sehemu ya operesheni inayolinda anga la Serbia dhidi ya ndege za kijeshi za Yugoslavia, hatua ambayo ilipingwa na watu wa Yugoslavia kama uingiliaji kati wa kigeni katika ardhi yao.
Akihofia hatima ya hatua hiyo, de Maiziere ameonya kwamba hatua zozote za kijeshi ni lazima zijadiliwe na viongozi wanaohusika na masuala ya usalama na sio kuwa mijadala ya wazi kwenye vyombo vya habari.
Gaddafi ayashutumu mataifa ya Magharibi kwa uasi
Gaddafi awataka Walibya wawashinde waasi
Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Muammar GaddafiHuku mapambano makali yakiendelea kati ya vikosi vitiifu kwa kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi, na waasi, kiongozi huyo amejitokeza akisema kwamba uasi unaoendelea dhidi yake umetayarishwa na nchi za Magharibi.
Katika mahojiano yaliyotangazwa leo kwenye televisheni ya taifa ya Libya, Muammar Gaddafi ameyashutumu waziwazi mataifa ya Magharibi kwamba ndiyo yaliyo nyuma ya uasi unaondelea sasa dhidi ya utawala wake na kuwaita Walibya wanaoshiriki kwenye uasi huu kuwa ni waasi.
"Mataifa ya kikoloni wanapanga njama za kuwadhalilisha watu wa Libya, kuwafanya watumwa na kuchukua mafuta yao." Amesema Gaddafi.
Katika mahojiano mengine mbali aliyofanya na kituo cha televisheni cha LCI cha Ufaransa, Gaddafi aliitaja kwa jina nchi ya Ufaransa kwamba iko kwenye mpango huo.
Ufaransa na Uingereza zimekuwa zikitoa wito wa kuwepo marufuku ya kuruka ndege kwenye anga ya Libya, ili kuzuwia vikosi vya Gaddafi visiwashambulie wapinzani kupitia angani. Hatua hii inaungwa mkono na Marekani, lakini kwa sharti la kuungwa mkono na kupitishwa na Umoja wa Mataifa.
Muasi wa Libya na mzinga wa kutungulia ndegeKatika hatua nyengine, kituo cha televisheni ya taifa cha Libya, kimemuonesha Gaddafi akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika mji wa Zintan, ulio umbali wa meli 75 kusini magharibi ya mji mkuu wa Tripoli, ambapo amewataka Walibya kuikomboa miji ya mashariki iliyochukuliwa na waasi.
Kwa mara nyengine, amelitaja kundi la Al-qaida, ambalo amesema linafanya kazi zake katika nchi za Misri, Algeria, Afghanistan na Mamlaka ya palestina kuwa ndilo linalohusika na machafuko yaliyoikumba Libya tangu katikati ya mwezi uliopita.
Majeshi ya Gaddafi yasonga mbele
Mripuko kwenye Ras LanoufWakati haya yakiripotiwa, kuna taarifa kuwa vikosi vitiifu kwa kiongozi huyo vinaendelea na mashambulizi makali dhidi ya waasi. Mashahidi wanasema wameviona vifaru vya kijeshi vikikaribia mji wa Zawiyah ulio magharibi mwa Libya.
Akizungumza na Shirika la Habari la Reuters, mpiganaji mmoja wa upande wa waasi, aliyejuilikana kwa jina la Ibrahim, amesema kwamba vifaru vya wanajeshi wa Gaddafi vimezagaa kila kona za barabara kuu na za ng'ambo za mji huo wa Zawiyah, huku akitaja kuonekana kwa miili ya watu waliouawa na vikosi hivyo.
"Mji umeharibiwa kwa mashambulizi kutoka angani. Pia kuna watunguaji wenye silaha katika kila jengo refu, na wanampiga risasi kila anayejaribu kutoka nje. Hivi sasa kuna miili mingi ya watu barabarani na hatuwezi hata kuwazika. Zawiyah imehamwa. Huoni mtu mitaani. Hata wanyama. Hata ndege." Amesema Ibrahim.
Amesema kuwa kiasi ya wapiganaji wao 60 waliotoka kwenda kupambana na wanajeshi wa Gaddafi hapo jana, umbali wa maili 12 kutoka Zawiyah, hawakuwa wamerudi hadi sasa, na hawana uhakika ikiwa wako hai ama wameshauawa.
Wachunguzi wa mambo wanasema kwamba, Libya imesimama njia panda, huku kukiwa hakuna hata upande mmoja kati ya pande znazopambana ambao una nguvu za kutosha kuushinda mwengine kwa sasa.
Kwa upande mmoja, vikosi vya Gaddafi havina uzoefu wa kupigana vita vya kukabiliana moja kwa moja, na kwa upande mwengine, waasi hawana silaha wala ujuzi wa kutosha kuweza kupambana na jeshi hadi ushindi.
Jambo hili linafanya kuwapo kwa uwezekano wa vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe, katika nchi ambayo bado utiifu kwa makabila ni mkubwa.
Hadi sasa jumuiya ya kimataifa haijakubaliana juu ya hatua za haraka kuchukuliwa kuzuia umwagikaji damu nchini Libya, huku wazo la kuiwekea nchi hiyo vikwazo vya anga likisuasua.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment