Jenerali Charles Bouchard kutoka Canada
Ndege za kivita za jeshi la muungano zilifanya mashambulio 150 zaidi dhidi ya vikosi vya jeshi la Kanali Gaddafi, ukiwemo mji wa mashariki wa Adjabiya. Mashambulio hayo yamewawezesha waasi kuudhibiti tena mji huo.
Baadhi ya ndege za kijeshi zinazoshiriki katika operesheni nchini Libya
Kuna taarifa kwamba mtoto wa kiume wa Kanali Gaddafi, Saif al-Islam ameondoka kwa siri nchini humo ikiwa ni katika kuchukua hatua za kidiplomasia kwa ajili ya kuzuia mapigano zaidi na kuidhibiti hali iliyopo sasa ya kisiasa na kijeshi ambayo inazidi kuwa mbaya.
Marekani na Jumuiya ya Kujihami ya NATO zinafikiria kuwapatia silaha wapinzani, zikisema kuwa azimio la Umoja wa Mataifa linaruhusu uwezekano huo.
NATO hatimaye pia imekubali kuchukua jukumu la kuongoza operesheni za kutekeleza marufuku ya ndege kuruka katika anga ya Libya.
Uvamizi wa anga unaofanywa na majeshi ya muungano umeshambulia eneo alipozaliwa Kanali Muammar Gaddafi huko Sirte, eneo muhimu linalolengwa na waasi lililopo upande wa magharibi.
Msemaji wa serikali ya Libya alisema raia watatu wa Libya waliuliwa kwenye bandari ya nchi hiyo.
Uvumi ambao haukuthibitishwa kuwa waasi waliudhibiti mji wa Sirte ulisababisha waasi kufyatua risasi kwa minajil ya kushangilia kwenye mji walioukhodhi wa Benghazi.
Waandishi wa kigeni Sirte walisema walisikia milipuko mikubwa kwenye mji huo huku ndege zikipita angani.
Msemaji wa waasi huko Benghazi alisema Sirte sasa ilikuwa mikononi mwa majeshi ya waasi- lakini hakujakuwa na uthibitisho binafsi kutokana na madai hayo, na waandishi wa habari wa kimataifa ndani ya mji huo walisema bado unadhibitiwa na serikali.
Wakati huo huo, Qatar ni taifa la kwanza la kiarabu kutambua uongozi wa waasi- Baraza la Taifa la Mpito- kama wawakilishi rasmi wa watu wa Libya.
No comments:
Post a Comment