Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Friday, March 11, 2011

Sumatra yatoa leseni ya muda Loriondo


MAMLAKA ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini, (Sumatra), imeanza kutoa leseni za muda kwa magari ya kusafirisha abiria yaendayo kijiji cha Samunge, Loliondo, kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila.
Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia hitaji kubwa la wasafiri wanaendao kwa mchungaji huyo mstaafu.

Sumatra mkoani Arusha imechukua uamuzi huo ili kuweza kuweza kudhibiti bei stahiki ya nauli ya halali ya kuelekea huko kutokana na ongezeko la wimbi la magari yanayojitokeza kufanya ruti hiyo

Hata hivyo Sumatra haitakataza wanaojitolea kufanya ruti hizokwa kuwa suala hilo limeonekana kuwa ni la dharura .

Hivyo kufuatia hatua hiyo wamiliki wa magari yaendayo huko watalazimika kukata leseni hizo ili haki ya abiriana kanuni za usafirishaji uweze kuchukuliwa wka kuwa wamiliki hao wanajiongezea nauli watakavyo

“Hii itasaidia kupunguza nauli walizopandisha kiholela” alisema

Hata hivyo ilidaiwa kuwa katika ruti hiyo kuna jumla ya mabasi sita tu yaliyosajiliwa kihalali yanayoambulika Sumatra.

Nauli halali ya iliyopangwa na Sumatra kutoka Arusha kwenda Loliondo ni Shilingi elfu kumi na saba tu 17,000/= ya kitanzania lakini kwa hivi sasa hivi imepanda maradufu kutokana na ongezeko la abioria kuelekea huko na kufikia hadi Shilingi laki moja 100,000 hadi laki moja na nusu kutegemea na bei anayoitaka mmiliki wa gari








Pombe si Chai, Aibu! Aibu! Aibu!




KATIKA kuonyesha kuwa mmomonyoko wa maadili unashika kasi kila kukicha nchini Tanzania, wapenzi wawili jana wameonekana wakifanya mapenzi hadharani kwa kuzidiwa na pombe kupita kiasi huko maeneo ya Ilala Mchikichini jijini Dar es Salaam.
Wapenzi hao ambao walizidiwa na pombe walijikuta wakifanya mapenzi hadharani kwenye majani yaliyokuwa yameota katika moja ya njia ya maeneo hayo.

Tukio hilo lililoshangaza wapita njia waliowengi lilikuwa likifanyika majira ya saa 3 usiku eneo hilo.

Tukio hilo lilikuwa ni la aibu na la kusikitisha kwa kuonekana wapenzi hao wakiwa wamelala michangani wakiendelea na vitendo vya kimapenzi hadharani bila hata chembe ya aibu.

Kutokana na tukio hilo ambalo lilizua tafrani maeneo hayo hasa kwa wale wastaarabu baadhi ya wapita njia walionekana na mtandao huu waliokuwa wakihitaji kupita njia hiyo wakiwa na watoto wao walilazimika kukimbia huku wengine wakilazimika kubadilisha njia ili kunusuru watoto waisone tukio hilo.

Baadhi ya mashuhuda waliokuwa eneo la tukio wanaoishi maeneo hayo, waliokuwa na moyo kuwasogelea wapenzi hao walidai kuwa, wawili hao walikuwa wakionekana maeneo hayo mara kwa mara wakiwa wanaongozana kwenda kwenye vilabu zinavyouza pombe za kienyeji kwenda kupata vinywaji hivyo na walikuwa hawafahamiki walikuwa wanaishi eneo lipi.

Hata hivyo mwandishi wa habari hii hakufanikiwa kupata majina ya wawili hao, na imeona kutoweka picha kwa kuwa picha hiyo kimaadili isingeweza kutumika katika mtandao huu kutokana na kuwa kinyume na maadili ya watanzania







Ajinusurisha polisi kwa kujeruhi mke kwa wivu wa kimapenzi


KIJANA mmoja jina kapuni [34] mkazi wa Yombo amejinusurisha kituo cha polisi baada ya kumjeruhi mke wake kutokana na sababu za wivu wa kimapenzi.
Chanzo cha habari hii kilidai kuwa, kijana huyo alimjeruhi mke wake baada ya kumuhisi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwenye nyumba wao.

Ilidaiwa kuwa, jana majira ya saa 2 usiku mume huyo alikuwa akianza kumfokoe mke wake na hatma yake alijikuta kumpiga na kumjeruhi maeneo yake ya usoni kutokana na jazba na hasira ya kuhisi kuibiwa mke wake.

Ilidaiwa kuwa, mara baada ya kuona amejeruhi kijana huyo alichomoka ndani kwake na kukimbilia kituo cha polisi kilichokuwa karibu nao kuripoti tukio hilo.

Majirani waliokuwa karibu nao walikimbilia ndani humo na ndipo mwanamke huyo alibainisha kuwa alikuwa amempigwa na chupa ya soda kutokana na hasira za kuhisiwa anatoka nje ya ndoa.

Mwanamke huyo alibainisha kuwa “mume wangu ananihisi kuwa nina mahusiano na baba mwenye nyumba, kutokana na kutukuta mara kwa mara tukiongea na kuchangamkiana ndipo alikuwa akidhani kuwa ni mpenzi wangu”

Ilidaiwa kuwa mwanamke huyo alifafanua kuwa alikuwa na ukaribu na mwenye nyumba hiyo kwa kuwa alikuwa ni kabila moja na alikuwa akimuona kama kaka yake kutokana na kuongea lugha moja





Mwingine huyu hapa! Apoteza maisha kwa kuudhiwa na mke




MKAZI wa Mbezi Juu Mtoni jijini Dar es Salaam, aliyefahamika kwa jina la Shabani Kihundo (30), amekutwa amekufa akiwa chumbani kwa kuhisiwa kunywa sumu kwa kuudhiwa na mkewe katika ujumbe aliouacha chini ya kitanda.
Akitoa taarifa hiyo kwa wanahabari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,Bw. Charles Kenyela alisema kuwa, Kihundo alikutwa amekufa juzi chumbani kwake majira ya saa 7 mchana akiwa amelala kifudifudi.

Kamanda Kenyela alidai kuwa, Kihundo aliacha ujumbe uliooneshwa kuwa kulikuwa na ugomvi kati yake na mkewe ujumbe aliokutwa chini ya kitanda chake.

Kamanda Kenyela alifafanua kuwa ujumbe huo ulisomeka hivi: “Nimejiua kutokana na kutoelewana na mke wangu, nimeona nimuachie dunia name niondoke duniani nikatulize nafsi yangu japokuwa nilimpenda”

“Nimekuachia hiyo nyumba,japo kuwa ulininyima haki yangu, mimi ni mwanachama wa NSSF na kadi yangu anayo mke wangu,

“Yeye apewe milioni moja ili ziweze kumsaidia kwa sababu atakuwa na maisha magumu, nimeahca baiskeli apewe mdogo wake mke wangu pamoja, nguo na viatu”

“Pia Samweli ananidai shilingi 28,000 asante”ulimaliza ujumbe huo

Maiti imechukuliwa na kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi









Ampeleka mumewe polisi



KATIKA hali ambayo haijazoeleka katika jamii, Fatma Mussa [50] mkazi wa Gongolamboto amempeleka mumewe polisi kwa kuchoshwa na vipigo, kudhalilishwa na matusi kutoka kwa mumewe huyo.
Chanzo cha habari hii kilisema kuwa Fatma aliamua kuchukua uamuzi huo baada kuchoshwa na kadhia hiyo na kupewa ruksa na watoto wake baada ya kuchoshwa na kero hiyo.

Imedaiwa kuwa mwanamke huyo alikuwa akipata kipigo, matusi ya nguoni mara kwa mara kutoka kwa mumewe huyo hali inayomfanya akose amani pindi tu mumewe anapokuwa akirudi nyumbani.

Imedaiwa kuwa Jana mume huyo alirudi nyumbani hapo akiwa na hasira tele na kujikuta akimpiga mkewe na kumjeruhi maeneo ya usoni na kupelekea kushonwa nyuzi kumi eneo la jeraha.

Imedaiwa kutokana na hali hiyo watoto waliamua kuchukua uamuzi wa kumshauri mama yao akaripoti tukio hilo kituo cha polisi kwa kuwa walishachoshwa na hali hiyo.

Imedaiwa kuwa Khalidi [30] aliongoza wadogo zake kwenda kuripoti tukio hilo kwa kuwa walichoshwa na hali ya kuteswa kwa mama yao huyo.

Hata hivyo imedaiwa kuwa baba huyo alikuwa akimuamuru mke wake huyo aondoke kwao ili aweze kuoa mke wa pili kwa kuwa mke wake alikuwa haafiki maamuzis yake hayo.
Imedaiwa kuwa Fatma alipinga maamuzi ya kuletewa mke mwenzake katika nyumba hiyo na kumshauri amtafutie nyumba nyingie awatenganishe na si kukaa mahali pamoja.

Imedaiwa kuwa mume huyo haafiki mawazo hayo na alikuwa akihitaji amlete ndani humo na kumtaka mkewe huyo aondoke kama hataweza kuishi hapo na mke mwenzake

Imedaiwa kuwa wanandoa hao walibarikiwa kuwa na watoto watatu na walitoa baraka zote kumpa mama yao kuwa akaripoti tukio hilo ili baba yao huyo aweze kuadabishwe kutokana na kuchoshwa na tabia hiyo.

Mume huyo aliyetambulika kwa jina moja la Farid [59] ni dereva wa kampuni binafsi wa magari makubwa yasafirishayo mizigo yaendayo nchi jirani.

Muda wowote kuanzia leo mume huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu shtaka hilo linalomkabili





Maandamano Syria






Polisi nchini Syria wamewatawanya kiasi cha watu 150 katikati ya Damascus hii leo, ambao walikuwa wakidai kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa askari hao walikuwa wakiwatawanya waandamanaji hao kwa kutumia virungu.

Maandamano hayo yamekuja siku moja baada ya takriban Wasyria 200 kufanya mkutano usiotarajiwa katika mji mkuu wa nchi hiyo wakidai uhuru na mageuzi ya kisiasa, licha ya sheria ya dharura iliyowekwa mwaka 1963 ikiwa bado inafanyakazi, ambayo imepiga marufuku upinzani wa aina yoyote ile.

Ukurasa wa mtandao wa Facebook ambao ulitoa wito wa mapinduzi nchini Syria dhidi rais wa nchi hiyo Bashar al-Assad katika mwaka huu wa 2011, ndio uliochochea maandamano hayo.







watu 120 wajeruhiwa Yemen






Watu 120 wamejeruhiwa magharibi mwa Yemen leo katika mapigano kati ya majeshi ya serikali na waandamanaji wanaoipinga serikali.

Majeshi ya serikali yalitumia gesi ya kutoa machozi na risasi kuwatawanya waandamanaji katika mji wa Bandari wa Al Hudaydah.

Upinzani dhidi ya Rais Ali Abdullah Saleh ambaye ameitawala nchi hiyo kwa miaka 32, uliopata msukumo kutokana na wimbi la uasi katika ulimwengu wa kiarabu, umekubwa na machafuko yaliyosababisha watu 40 kuuawa






Bahrain yaripuka tena




Siku moja baada ya kutangazwa kwa hali ya hatari na kuingia kwa majeshi ya Jumuiya ya Nchi za Ghuba nchini Bahrain, jeshi limeuvamia uwanja wa Pearl walipokusanyika waandamanaji wanaoupinga utawala wa Al Khalifa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Reuters, kiongozi wa chama cha Waislamu wa Madhehebu ya Shia bungeni, Abdel Jalil Khalil, kinachotokezea hivi sasa ni "mauaji ya kuteketeza".

"Jambo hili halitokezei hata katika uwanja wa vita, seuze kwenye uwanja ambapo watu wamekusanyika kwa amani, na hili halikubaliki". Amesema Khalil.

Inaripotiwa kuwa usiku wa kuamkia leo, vikosi vya jeshi na polisi, viliuvamia uwanja wa Pearl, vikawashambulia waandamanaji waliokuwa ndani ya mahema yao na walio mitaani, vikilazimisha kulisafisha eneo hilo, ambalo limekuwa kitovu cha maandamano ya karibuni wiki tatu sasa dhidi ya utawala wa Al Khalifa.




Haijafahamika bado ikiwa wanajeshi walioshiriki kwenye operesheni hii ni pamoja na wale wa kigeni kutoka Saudi Arabia na Imaraat, lakini Khalil anasema kuwa wanajeshi na polisi wamejaa kila sehemu mitaani, wakikamata na kufyatua risasi kwa mtu yeyote anayejaribu kukaidi amri yao.

Kuna taarifa za nyumba za watu binafsi na sehemu za kufanyia shughuli za maziko kupokea mamia ya wahanga, kwani vikosi vya jeshi vinaripotiwa kuzizunguka hospitali kuzuia ama majeruhi kupelekwa huko na au madaktari kuwahudumia.

Kiasi ya watu 200 wamejeruhiwa kwa mabomu ya machozi na daktari mmoja kutoka hospitali ya Salmaniya, amekiambia kituo cha televisheni cha Al-Jazeera, kwamba hali ni ya kuvunja moyo sana.

"Wanajeshi wa Bahrain na Saudi Arabia wanafanya uhalifu dhidi ya binaadamu kwenye ardhi ya Bahrain. Kuna majeruhi wengi hapa. Huko Sitra pia majeruhi wamelala barabarani, hatujui wanaendeleaje, kwa sababu hatuwezi kufika huko. Polisi wameyazuia magari ya kuhudumia wagonjwa, maji yamefungwa, mmoja ametufia hapa hapa." Amesema daktari huyo.




Vilivyothibitishwa hadi sasa ni vifo vya watu watatu. Televisheni ya taifa ya nchi hiyo inasema kwamba, hapo jana, waandamanaji walimuua kwa kumpiga risasi mwanajeshi mmoja wa Saudi Arabia.

Jamii ya Washia nchini humo imeutaka ulimwengu wa Kiislamu na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kusaidia haraka iwezekavyo ili kuzuia mauaji zaidi.

Hapo jana, maelfu ya watu waliandamana kutoka uwanja wa Pearl kuelekea ubalozi wa Saudi Arabia kupinga kitendo cha majeshi ya nchi hiyo kuingia Bahrain.

Maandamano hayo, hata hivyo, hayakuzuiwa na polisi na yalikuwa ya amani. Nabil Rajab wa Kituo cha Haki za Binaadamu anasema, raia wa Bahrain hawapendelei hata kidogo nchi yao kuingiliwa na mataifa ya nje, hata kama ni Waarabu wenzao.

"Hali ni tete na mbaya sana. Watu wamekasirishwa na Saudi Arabia na nchi nyengine za Ghuba kuleta majeshi yao hapa, kuja kukandamiza maandamano ya amani, ambayo watu wanadai tu haki zao za kisiasa na kuheshimiwa kwa haki za binaadamu. Hili hatulikubali kabisa na tutalipinga mpaka majeshi haya yaondoke." Amesema Rajab.

Wafuasi wa upinzani wanahsi kuwa Marekani imewasaliti, kwa kuinyamazia kimya serikali ya Bahrain inapowakandamiza waandamani. Hadi sasa Marekani haijaonesha kupinga majeshi ya nchi za Ghuba kuingia Bahrain.












TEHRAN, Iran (AP) -- Iran's Foreign Ministry spokesman has denounced the deployment of a Saudi-led military force to Bahrain to prop up the monarchy in the tiny island nation against widening demonstrations by the Shiite-led opposition. Ramin Mehmanparast said on Tuesday that the "presence of foreign forces in Bahrain is unacceptable" and would only complicate the crisis in the Sunni-led kingdom. The statement is the strongest reaction from Shiite powerhouse Iran on Monday's deployment of about 1,000 troops from Saudi Arabia and other members of the Gulf Cooperation Council. Bahrain is a key U.S. ally and host of the U.S. Navy's 5th Fleet....




Gaddafi sasa abanwa na Umoja wa Mataifa







Waasi wamekaribisha uamuzi huo kwa furaha kuu mjini Benghazi
Baraza la Usalama la umoja wa Mataifa limepitisha azimio linaloidhinisha kuchukuliwa kwa hatua za kuwalinda raia nchini Libya dhidi ya mashambulizi ya wanajeshi wa Kanali Muamar Gaddafi.

Miongoni mwake ni kutenga eneo ambalo ndege hazipaswi kupaa angani.

Lakini azimio hilo limepinga matumizi ya wanajeshi wa ardhini.

Serikali ya Ufaransa imesema hatua za kijeshi dhidi ya majeshi ya Kanali Gaddafi zitaanza wakati wowote.

Wanachama kumi wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walipiga kura kuunga mkono azimio hilo lakini wengine watano ikiwemo China, Urusi na Ujerumani walisusia kura hiyo.

Matokeo ya kura hiyo yamepokewa kwa vigelegele,vifijo na ulipuaji wa fataki katika eneo linalodhibitiwa na waasi la Benghazi, Mashariki mwa Libya.

Makundi ya waasi yalipeperusha bendera zao huku wakifyatua risasi angani mara tu habari hizo zilipowafikia.

Awali Kanali Gaddafi alikuwa aliapa kuuteka mji wa Benghazi na kusema kuwa mtu ye yote atakayepinga hatua hiyo atakabiliwa vikali.








Rais Obama amwonya Gaddafi






Rais wa Marekani, Barack Obama Baada ya Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kuifunga anga ya Libya, Rais Barack Obama ameonya kuwa Marekani inaweza kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya kiongozi huyo wa Libya ikiwa hataacha kuwashambulia watu wake.

Rais Obama amesema yaliyotamkwa katika azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kuwalinda raia nchini Libya siyo masuala ya kujadiliwa. Amesema ikiwa Kanali Gaddafi hatalitekeleza azimio la Baraza la Usalama jumuiya ya kimataifa itamchukulia hatua na azimizo hilo litatekelezwa kwa njia ya nguvu za kijeshi.



Rais Obama amesema katika hotuba aliyoitoa kwa njia ya televisheni, kwamba Gaddafi lazima aache mashambulio yote.Kiongozi huyo wa Marekani amemtaka Kanali Gaddafi ayaamrishe majeshi yake ili yaache kuelekea Benghazi na ayaondoe kutoka miji ya Ajdabiya, Misrata na Az Zawiya.
Maseneta wa chama cha Republican, Marekani

Wabunge wataka mjadala rasmi

Hata hivyo, wabunge wa Marekani wamesema wanataka mjadala rasmi ufanyike na kura ipigwe juu ya kuidhinisha hatua zozote za kijeshi za kuchukuliwa dhidi ya Libya. Wabunge hao wameeleza kuwa katiba ya Marekani imelipa bunge mamlaka ya kutangaza vita na siyo Rais.

Seneta wa chama cha Republican, Richard Lugar amesema Rais hapaswi kuamua juu ya vita dhidi ya Libya bila ya wawakilishi wa wananchi kupiga kura. Lakini onyo lililotolewa na Rais Obama juu ya kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Libya limeungwa mkono mara moja na Ufaransa, Uingereza na nchi za Kiarabu.



Wananchi wa Libya wakiwa wamenyanyua juu bendera
Libya yatangaza kusimamisha mashambulizi

Wakati huo huo, nchini Libya utawala wa Gaddafi umesema kuwa umesimamisha mashambulio, lakini pana taarifa kwamba mashambulio bado yanaendelea katika baadhi ya maeneo fulani. Juu ya hayo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton amesema jumuiya ya kimataifa haitavutiwa na kauli. Amesema kinachotakiwa ni hatua thabiti. Bibi Clinton amesema ameziona taarifa za vyombo vya habari zilizotolewa na serikali ya Libya juu ya kusimamisha mashambulio.

Lakini ameeleza kuwa hali inaendelea kubadilika kwa haraka. Hata hivyo, ametamka kuwa angelipendelea kuona hatua thabiti, lakini amesema hali bado haijawa wazi. Waziri Clinton amesema Marekani itashirikiana na washirika wake katika jumuiya ya kimataifa ili kumshinikiza Gaddafi aondoke na pia itaendelea kuyaunga mkono matakwa halali ya watu wa Libya.

Na Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Susan Rice amesema utawala wa Gaddafi unalikiuka azimio la Baraza la Usalama juu ya kusimamisha mashambulio. Balozi huyo alikuwa anajibu swali, iwapo utawala wa Gaddafi unakiuka azimio la Umoja wa Mataifa.




Mkutano kuhusu Libya kufanyika Ufaransa

Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy Habari kutoka Paris zinasema Ufaransa inaitisha kikao muhimu leo kujadili hali ya Libya, kitakachohudhuriwa pia na wawakilishi kutoka Umoja wa nchi za Kiarabu, Umoja wa Afrika, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton. Na duru za kibalozi za Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa zimeashiria kwamba hatua za kijeshi dhidi ya Libya zinakaribia sana kuchukuliwa, yumkini baada ya kikao cha mjini Paris.









Ujerumani yapinga hatua za kijeshi dhidi ya Libya






Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle. Ujerumani imepinga kwa mara nyingine matumizi ya nguvu za kijeshi dhidi ya utawala wa Gaddafi

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle kwa mara nyingine amepinga wazo la kuifunga anga ya Libya ili kuzizuia ndege za Gaddafi kuruka.

Waziri Westerwelle ameyasema hayo mjini Berlin katika tamko rasmi la serikali ya Ujerumani juu ya hali ya kisiasa nchini Libya.Waziri huyo ameusisitiza msimamo huo licha ya majeshi ya Gaddafi kusonga mbele kuelekea kwenye ngome ya waasi.

Westerwelle ameeleza kuwa Ujerumani haipaswi kuwa pande mojawapo katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Libya.Amesema Ujerumani haitaki na wala haipaswi kuwa vitani nchini Libya.Ameeleza kuwa kuchukua hatua za kijeshi ili kuifunga anga ya Libya kutaleta maswali mengi zaidi kuliko majibu.

Akifafanua msimamo wa Ujerumani juu ya nchi za Kaskazini mwa Afrika kwa jumla Waziri Westerwelle alitamka kuwa Ujerumani inataka kusaidia ili watu waweze kuona mustakabal mzuri katika nchi zao. Amesema kuchukua hatua sasa katika nchi hizo ndiyo siasa bora, ili pia kuepusha wimbi la wakimbizi.

Hata hivyo Waziri Westerwelle amesisitiza katika tamko la serikali mjini Berlin leo kwamba badala ya hatua za kijeshi, vikwazo vinapaswa kulengwa panapostahili dhidi ya utawala wa Gaddafi. Kwa hiyo amesema Ujerumani inaunga mkono hatua ya Umoja wa Mataifa ya kuimarisha shinikizo la kisiasa dhidi ya utawala wa Kanali Gaddafi.

Waziri huyo pia ameyapinga manufaa ya kiuchumi yaliyodokezwa na utawala wa Gaddafi kwa Ujerumani. Waziri Westerwelle ametamka wazi kwamba dikteta Gaddafi lazima aondoke. Amesema urafiki wenye sumu wa dikteta Gaddafi hautaubadili msimamo huo wa Ujerumani.Hapo awali Kanali Gaddafi aliusifu msimamo wa Ujerumani juu ya utawala wake, kulinganisha na ule wa nchi nyingine.

Gaddafi alisema katika mahojiano na televisheni ya RTL kwamba sasa hana imani tena na nchi za magharibi. Na kutokana na hayo tenda za biashara ya mafuta zitakwenda Urusi, China na India. Gaddafi pia amesema anaamini kuwa Ujerumani pia inaweza kuendelea kupata tenda ya biashara ya mafuta.

Juu ya harakati za kuleta mapinduzi ya kidemokrasia katika nchi za Kaskazini mwa Afrika, Waziri Westerwelle amesema Ujerumani pia inashuhudia mapambazuko ambayo ni fursa kubwa kwa nchi hizo na kwa Ujerumani kadhalika.

Waziri huyo pia amezungumzia juu ya hali ya mvutano nchini Bahrain. Ametoa mwito kwa nchi za eneo la Uarabuni wa kujizuia, na amezitaka pande za serikali na za upinzani zianzishe mazungumzo.Amesema suluhisho lazima lipatikane kutokea ndani.Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Westerwelle pia ametoa mwito wa kukomesha matumizi ya nguvu.






VIDEO - Kiama cha Japan Hakijaisha, Tsunami Jingine Kutokea Ndani ya Siku Tatu



Wakati maelfu ya watu wakihofiwa kufariki, uchumi wa Japan ukitetereka, huku miale ya nyuklia ikitishia amani zaidi, tetemeko jingine kubwa linatarajiwa kuitikisa Japan ndani ya siku tatu zijazo. Angalia PICHA na VIDEO za tetemeko la ardhi lilivyotokea na jinsi mawimbi makubwa ya Tsunami yalivyoisambaratisha miji ya Japan.
Kuna uwezekano mkubwa wa asilimia 70 tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa 7.0 litaitikisa tena Japan ndani ya siku tatu zijazo na tetemeko hilo huenda likasababisha Tsunami kutokea kwa mara nyingine.

"Kuna uwezekano wa asilimia 70, tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa 7.0 au zaidi huenda likatokea ndani ya siku tatu zijazo", alisema Takashi Yokota, mkurugenzi wa taasisi inayoshughulikia utabiri wa matetemeko ya ardhi nchini Japan.

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.0 lina uwezo wa kubomoa majengo na kusababisha kutokea kwa Tsunami, alisema Takashi.

Hadi sasa maelfu ya watu wameishafariki huku zaidi ya watu 10,000 wanahofiwa kufariki baada ya kusombwa na Tsunami katika mji wa Minami Sanrik ambao majengo yote katika mji huo yamebomolewa na Tsunami.

Hofu nyingine kubwa iliyotanda nchini Japan ni miale ya Nyuklia ambapo vitu vitatu vya nishati ya nyuklia vipo kwenye hatari ya kulipuka na kupelekea kuvuja kwa miale ya nyuklia ambayo ni hatari sana kwa maisha ya binadamu.

Uchumi wa Japan nao umepigwa kumbo kubwa sana na Tsunami ambapo Waziri Mkuu wa Japani, Naoto Kan, amesema kuwa nchi yake inakabiliwa na janga kubwa kabisa, tangu vita vya pili vya dunia.

Angalia VIDEO chini zinazoonyesha jinsi tetemeko la ardhi lilivyoingia kwenye mitaa ya Japan na kusomba somba kila kitu





VIDEO - Mawimbi ya Tsunami Yalivyoiteketeza Japan


No comments:

Post a Comment