Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Friday, March 11, 2011

Mrema Atinga Kwa Babu Loriondo Kufuata Dawa za Kisukari



VIONGOZI, vigogo wa kada mbalimbali wamekuwa wakimiminika huko Ngorongoro, Loriondo kwa mchungaji Ambilikile ambaye amepachikwa jina la 'BABU' kwa lengo la kujitibia maradhi yanayowasumbua kwa muda mrefu.
Kati ya viongozi hao ni Augustine Mrema ambaye ameonekana kutinga kwa mchungaji huyo kwa lengo la kujitibia maradhi yake ya kisukari yanayomkabili kwa muda mrefu.

“Nimekuja kujitibia kisukari changu, ili nitoke na nguvu mpya ya kuwahudumia wananchi” alisema Mrema

Mrema ambaye ameshawahi kushika nyadhifa mbalimbali serikali ikiwemo kuwahi kuwa waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, na alishawahi kugombania nafasi ya Rais kwa tiketi ya NCCR, na TLP na hivi sasa ni Mwenykiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mtaa [LAAC]

Hivi karibuni serikali kupitia Wizara ya Afya ilitangaza kumsitisha mchungaji huyo maarufu kama ‘BABU’ kuacha kutoa hudma hiyo kwa kuwa dawa hiyo ilikuwa haijabarikiwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa [TFDA] pia ilikuwa haijasiliwa.

Mbali na kutolewa kwa tamko hilo kutoka serikalini watu wamekuwa wakizidi kumiminika huku wengine wakitoa malalamiko kwa serikali kuwaacha wakapate huduma hiyo kwa kuwa mchungaji huyo alishushwa na Mungu kuwahudumia Watanzania na kutoa huduma ya uponyaji.

Mchungaji huyo anaendelea kutoa huduma hiyo kijijni hapo na jana aliiomba serikali kumuandalia makazi ya kudumu ili aweze kuhudumia uma wa watanzania.

Jana zaidi ya magari 3,000 yalikuwa kwenye foleni ya kuelekea kwa Babu kwenda kunywa dawa hiyo inayotibu maradhi sugu na walioitumia wameendelea kudai kuponywa na dawa hiyo.




Mtambo wa Nyuklia walipuka tena Japan




Kumetokea mlipuko mwingine katika kinu cha kinukilia kilichoharibiwa na tetemeko la ardhi cha mji wa Fukushima. Mlipuko huo ulitifua moshi mkubwa katika eneo hilo.

Mlipuko huo wa hewa ya Hydrogen ulitokea katika mtambo wa tatu, lakini katibu wa Baraza la Mawaziri wa Japan amesema kuwa hakuna hatari ya kusababisha kuvuja kwa sumu ya kinukilia kutokana na mlipuko huo ni ndogo sana.

Msimamizi wa kiwanda hicho amesema kuwa mlipuko huo haujaharibu kifaa kinacho hifadhi mtambo huo wa kinukilia. Kiwanda hicho kinasema watu sita walijaruhiwa.

Hadi kufikia sasa watu 22 wametibiwa kutokana na madhara ya kuharibika kwa kinu hicho cha kinukilia. Awali Waziri Mkuu wa Japan, Naoto Kan, alisema kuwa kinu hicho kilichoharibiwa kutokana na uharibifu wa Ijumaa kilikuwa katika hali ya hatari.

Mlipuko wa hewa ya hydrogen ulirusha hewani paa la sehemu moja ya kiwanda mnamo Jumamosi. Mitetemeko midogomidogo imeendelea kutokea maeneo kadhaa nchini humo.












Vinu vya nyuklia kuchunguzwa Ujerumani





Kiongozi wa Ujerumani, Angela Merkel, amesema usalama wa vinu vyote vya nyuklia nchini vitachunguzwa tena baada ya maafa yaliyotokea katika vinu vya Japan.





Bi Angela Merkel


Bi Merkel aliyasema hayo baada ya kufanywa maandamano makubwa kupinga matumizi ya nyuklia.

Hii ndio isahara ya mwanzo ya jinsi matukio ya Japan yanavyoweza kubadilisha majadiliano kuhusu matumizi ya nyuklia.

Matukio ya Japan yamebadilisha mawazo nchini Ujerumani.

Tayari kuna vuguvugu linalopinga kurefusha muda wa vinu vya nishati vya nuklia vilioko hivi sasa Ujerumani.

Maandamano yaliyofanywa jana yalihudhuriwa na maelfu ya watu.

Sasa kiongozi Angela Merkel amesema, "yaliyotokea Japan yataleta mabadiliko ulimwenguni, hasa kwa sababu Japan ni nchi iliyoendelea sana."

Aliongeza kusema kuwa, usalama wa vinu vya nishati vya nyuklia vya Ujerumani utachunguzwa tena ingawa alisema anaamini kuwa vinu vya Ujerumani ni salama.

Bila ya shaka, Ujerumani ni tofauti na Japan kwa sababu mitetemeko ni nadra.

Lakini hii ndiyo ishara ya mwanzo, kuonesha namna swala la nyuklia, litavyotazamwa katika nchi nyingi





Chenji yampeleka kuzimu


KIJANA Joseph Nyabikwi [20] amefariki dunia kwa kuchomwa na kisu baada ya kumuomba chenji muuza duka alipokwenda kununua bidhaa.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea huko wilayani Sirari , Tarime baada ya mwenye duka kughadhibika na kuombwa chenji hiyo.

Imedaiwa kuwa muuza duka aliyefahamika kwa jina la Ramson Mwita [36] alimchoma kisu marehemu huyo kutokana na kitendo chake cha kumuomba chenji.

Imedaiwa kuwa, marehemu alifika dukani kwa Mwita na noti ya shilingi elfu kumi kununua bidhaa yake na baadae alimuomba chenji ili aweze kuondoka dukani hapo.

Ndipo muuza huyo alipochukua kisu na kumchoma nacho na kusababisha kupoteza uhai wake.






Majeshi ya Gaddafi yawashambulia waasi



Waasi wakiwa mjini Ajdabiya


Majeshi ya Kanali Muammar Gaddafi's yanasogea taratibu kwenye miji inayoshikiliwa na waasi nchini Libya.

Ajdabiya, mji mkuu wa mwisho kabla ya kufika eneo linalokhodhiwa na waasi la Benghazi, mashariki mwa Libya, limejikuta likishambuliwa kupitia angani.

Na huko magharibi, majeshi ya ardhini na vifaru vimekuwa vikiushambulia mji wa Zuwara.

Awali, majeshi ya waasi yalisema yaliudhibiti tena mji wa Brega, lakini serikali imepuuzilia mbali madai hayo.

Wakati huo huo, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linafikiria kutoa amri ya kupiga marufuku upitaji wa ndege kwenye anga ya Libya.

Jumuiya ya kiarabu iliunga mkono hatua hiyo siku ya Jumamosi, lakini majeshi ya umoja wa nchi za kujihami za Ulaya Nato na Marekani mpaka sasa imeonyesha wasiwasi wa kuhusisha jeshi moja kwa moja katika mgogoro huo






Mwalimu Acharaza wanafunzi kwa waya wa Umeme



SHULE ya Msingi Bunge ya jijini Dar es salam, imeingia kwenye kashfa baada ya mwalimu mmoja shuleni hapo kuwaadhibu wanafunzi kwa waya wa transfoma.
Taarifa kutoka shuleni hapo ilisema kuwa mwalimu anayefahamika kwa jina la Preygod Isaya [26] ameiingiza shule hiyo kwenye kashfa hiyo.

Mwalimu Isaya mwalimu wa hisabati darasa la sita amewapa wanafunzi wake adhabu ya kuwachapa na waya wa umeme baada ya kuona wanafunzi hao hawasikii.

Hata hivyo mwalimu huyo alifafanua kuwa aliamua kuwachapa na waya huo kwa kuona fimbo haiwatoshelezi kuwapigia wanafunzi hao kutokana na kosa lao.

Pia shule hiyo imekuwa na tuhuma ya kuwapa adhabu ya kuwarudisha wanafunzi nyumbani kutokana na kuchelewa kufika shuleni hapo.

Na zoezi hilo limedaiwa kubarikiwa na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Hadija Telela





Jeshi limeukomboa mji wa Brega, Libya







Televisheni ya Libya inasema kuwa jeshi limeukomboa mji wa Brega ulioko mashariki kutoka wale walioelezewa kuwa magenge yenye silaha.

Hali nchini Libya


Taarifa hizo hazijaweza kuthibitishwa.

Majeshi ya Gaddafi yamekuwa yakisonga mbele kwa kasi dhidi ya wapiganaji wasiokuwa na silaha wala uongozi mmoj, katika maeneo ya mashariki na magharibi mwa nchi.


Kukombolewa kwa mji mdogo wa Brega, kama ni kweli, kutathibitisha mkondo ambao umejitokeza katika siku chache zilizopita.

Jeshi la Gaddafi limeweza kugeuza mafanikio ya wapiganaji waliyoyapata wakati upinzani ulipoanza.


Wapiganaji wanasema wanarejeshwa nyuma kwa sababu nguvu zao na zile za upande wa Gaddafi hazilingani.


Wanasema wanashambuliwa na ndege na manuwari na wanataka jumuiya ya kimataifa kufanya haraka kuweka amri ya kuzuwia ndege kuruka katika anga ya Libya ili kupunguza uwezo wa serikali.

Lakini Kanali Gaddafi amelitoa maanani tishio la kuingiliwa kati.








Inavoelekea yeye na wapinzani wake wako tayari kupigana hadi mwisho.










Nigeria yahitaji tume maalumu uchaguzi


Serikali ya Nigeria imehimizwa kuanzisha tume maalumu itayochunguza na kuchukua hatua za kisheria, dhidi ya ghasia na upotovu wowote utaotokea wakati wa uchaguzi.




Ramani ya Nigeria


Wito huo umetolewa na shirika la kimataifa la kupigania haki za kibinaadamu, Human Rights Watch, na shirika la mawakili wa Nigeria.

Katika taarifa ya pamoja, mashirika hayo yamesema kwamba Nigeria inahitaji kuhakikisha kuwa fujo, vitisho na udanganyifu hautochafua uchaguzi mkuu wa mwezi ujao.

Mashirika hayo yamesema ingawa watu 50 wameuwawa katika fujo za uchaguzi tangu mwezi Novemba, hata hivyo polisi hawana uwezo na uhuru wa kuchunguza mauaji hayo na hakuna mtu aliyekamatwa.







Chadema kumfikisha Simba Mahakamani




CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] kimetangaza kumfikisha Mahakamani Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Bi. Sophia Simba kwa kuupotosha umma dhidi ya chama hicho.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa mambo ya nje na uhusiano ya kimataifa, ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Ubungo[Chadema] John Mnyika alipokuwa akizungumza ma waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mnyika alisema, watamburuza waziri huyo kutokana na kauli zake za kukishashifu chama hicho.

Mnyika alifafanua kuwa waziri huyo aliweza kudiriki kusema kuwa Chadema wanaamua kufanya fujo ya kuanzisha maandamanao ya nchi nzima kwa kuwa wamekuwa wakifadhiliwa na nchi za nje.

Alisema kutokana na kauli ya waziri huyo ni sawa na kuupotosha umma wa watanzania kwa kwua kuwa maneno hayo si kweli.

Hivyo “tumeamua kumfikisha waziri huyo ili aweze kuthibitisha kauli yake hiyo mbele ya mahakama, na hii itakuwa onyo kwa viongozi wengine wa CCM wanaoibeza na kuipaka matope chadema “ alisema

Chadema kiliandaa maandamano ya nchi nzima kushinikiza kutolipwa kwa deni la bilioni 94 kwa kampuni ya kufua umeme dowans, ongezeko la ugumu wa maisha kwa watanzania.








Mji wa Abidjan ni shuwari


Ramani ya Ivory Coast

Utulivu umerejea Abidjan siku moja baada ya mapigano makali katika kitongoji cha Abobo.



Taarifa kutoka Ivory Coast zinaeleza kuwa mji wa Abidjan ni shuwari, siku moja baada ya mapigano makali, katika kitongoji cha Abobo, kinachodhibitiwa na wafuasi wa Alassane Ouattara anayetambuliwa kimataifa kuwa rais.

Taarifa hizo zinasema kuwa watu kadha waliuwawa wakati eneo hilo liliposhambuliwa na askari wa mpinzani wa Bwana Ouattara, Laurent Gbagbo, ambaye amekataa kuacha madaraka ingawa alishindwa katika uchaguzi wa mwezi Novemba mwaka jana.

Umoja wa Mataifa ulisema, afisa wake mmoja kutoka Ghana alijeruhiwa wakati gari lake liliposhambuliwa na vijana mjini Abidjan.






Wivu wasambaratisha maisha yake



ALLY Salum [48] anayedaiwa kuwa fundi ujenzi mkazi wa Yombo Buza, amekufa baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya mkonge kutokana na kuzidiwa na wivu wa mapenzi .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime alisema kuwa marehemu huyo alikutwa amekufa juzi, majira ya saa 8.00 mchana nyumbani kwake.
Alisme Ally kabla hajachukua uamuzi wa kujinyonga aliacha ujumbe maalum uliofanya ajinyonge yeye mwenyewe.

Alisema ujumbe huo ulionyesha dhahiri kuudhiwa na mke wake baada ya kuona mabadiliko yakitabia juu yake

Ujumbe aliouacha ulisomeka , “nimeamua kujinyonga kwa hiyari yangu kutokana na mke wangu kushauriwa na mama Salehe kutoka nje ya ndoa, hivyo namuachia ukumboi aendelee na hizo starehe zake, ila naomba mke wangu asibughudhiwe.

“Mali nilizochuma naye zibaki mikononi mwake, asinyang’anywe na mtu yeyote wala ndugu yangu yoyote, napenda kuwajulisha nilikuwa na mke mwingine mdogo yupo maeneo ya Kimbiji Kigamboni, Sanda yangu nilishaandaa siku nyingi ipo kwenye sanduku,” ulieleza ujumbe huo.

Polisi wanaendelea na upelelezi huku maiti imehifadhiwa hospitali yaTemeke.

Katika tukio jingine, MTOTO wa kike [1] ameokotwa akiwa hai na wapita njia huko maeneo ya Yombo Vituka jijini Dar es Salaam.

Mtoto huyo alitupwa na mtu asiyejulikana na wasamalia wema waliopita eneo hilo walimuona na kumuokotwa nakumkuta akiwa hai

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Bw. David Misime, ilisema kuwa mtoto huyo aliokotwa juzi majira ya saa 2.15 usiku.

Alisema mtoto huyo alikutwa akiwa amefungwa na kufunikwa na kitenge na kulazwa katika njia hiyo.

Taarifa ilipoifikia polisi mtoto huyo amechukuliwa na amehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke kwa uangalizi zaidi.





Sudan Kusini yashuku njama



Serikali ya Sudan Kusini imetangaza kuwa inasimamisha mazungumzo na Sudan Kaskazini na imemshutumu Rais Bashir kuwa anapanga njama ya kuipindua serikali ya kusini kabla ya uhuru, mwezi Julai.


Pagan Amun, kulia


Afisa mwandamizi, Pagan Amun, alisema Rais Bashir anasimamia njama inayotekelezwa na idara ya ujasusi ya jeshi.

Pia alisema serikali ya Sudan Kusini, inachunguza njia nyingine ya kusafirisha mafuta, badala ya kupitia Sudan Kaskazini kama ilivyo hivi sasa.

Tamko hilo lilitolewa baada ya ripoti za shambulio, lilofanywa alfajiri dhidi ya mji wa Malakal, linalofikiriwa kufanywa na wafuasi wa afisa aliyeasi wa Sudan Kusini, George Athor.

No comments:

Post a Comment