Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Tuesday, April 5, 2011

Umoja wa Mataifa washambulia kambi za Gbagbo

Helikopta za Umoja wa Mataifa nchini Cote d'Ivoire zimeshambulia kambi za wanajeshi watiifu kwa Laurent Gbagbo katika mji mkuu wa nchi hiyo, Abdijan.

Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, ameidhinisha vikosi vyake kushiriki kwenye operesheni hiyo ya Umoja wa Mataifa inayokusudia kupunguza mashambulizi ya silaha kutoka makambi ya vikosi vya Gbagbo.

Umoja wa Mataifa na Ufaransa wanasema operesheni hii inadhamiria kuzuia maafa kwa raia wa nchi hiyo ya Afrika ya Magharibi inayoonekana kutumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mshauri wa Gbagbo ameyaita mashambulizi haya kuwa si halali. Gbagbo alishindwa kwenye uchaguzi wa Novemba, lakini amekataa kuondoka madarakani.

Umoja wa Ulaya unaunga mkono juhudi za Umoja wa Mataifa ambazo nazo zinawasaidia waasi. Rais wa Umoja huo, Herman Van Rompuy, amemtaka Gbagbo kundoka madarakani ili amani ipatikane.

Ujumbe huu wa Rompuy unasadifiana na kile kinachoitwa "mashambulizi ya mwisho", kutoka vikosi vya rais wa Cote d'Ivoire anayetambuliwa kimataifa, Alassane Ouattara.

Wakati huo huo, taarifa za hivi punde zinasema vikosi vya Ouattara vinashikilia makaazi rasmi ya Gbagbo, ingawa bado haijafahamika ikiwa Gbagbo mwenyewe yupo kwenye makaazi hayo ama la














Westerwelle ajiuzulu uwenyekiti wa FDP, unaibu kansela





Guido Westerwelle

Wiki moja baada ya kushindwa vibaya kwa chama cha FDP katika chaguzi za mikoa ya Baden-Württemberg na Rheinland-Pfalz, mwenyekiti wa chama hicho, Guido Westerwelle, amejiuzulu wadhifa wake na ule wa unaibu kansela.

Yumkini hakuna sababu moja tu ya kujiuzulu kwa Westerwelle, maana ukiacha maneno makali aliyokuwa akitupiwa na wenzake kwenye chama, kwa siku za karibuni amekuwa pia akishutumiwa na hata walio nje ya chama chake, kwa msimamo wa Ujerumani kujizuia kulipigia kura Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo liliruhusu uingiliaji kati kijeshi nchini Libya.









Matokeo yake ni kuwa, miaka yake kumi ya kuwa mwenyekiti wa chama hiki cha kiliberali, imemalizika kwa hotuba ya nusu dakika tu. Shinikizo kutoka ndani na nje ya chama chake, lilimfanya hapo jioni ya jana ashindwe hata kusubiri mawiyo ya leo (Jumatatu, 04.04.2011).



Kansela Angela MerkelBadala yake akaamua kuitisha mkutano wa waandishi wa habari ofisini kwake mjini Berlin, na kutangaza mwanzo wa mwisho wake kwenye siasa za uongozi wa FDP.

"Sitogombea tena nafasi ya uenyekiti kwenye uchaguzi wa chama hapo mwezi Mei. Ninaweza kuwaambia kuwa uamuzi huu kwangu ulikuwa mzito kwa upande mmoja na mwepesi kwa upande mwengine. Mzito kwa kuwa mtu ambaye amekuwa kwenye chama kwa miaka kumi kama mwenyekiti inahitaji moyo kuwacha ghafla hivi. Lakini ni mwepesi kwa kuwa sasa tuna vijana wengi walio tayari kupigania nafasi za uongozi wa chama na kuchukua uongozi wa FDP." Ndivyo alivyowaambia waandishi wa habari.

Asubuhi ya jana tu, Westerwelle alikuwa ametoka safarini katika nchini za Asia. Wakati akiwa Japan na China, huku nyumbani kulikuwa kunatokota kauli za chinichini kumtaka awachie ofisi za uenyekiti wa chama.

Hadi hapo, bado marafiki na waungaji mkono wake, kama vile kiongozi wa FDP Bungeni, Birgit Homburger, na Katibu Mkuu wa chama Christian Lindner, hawakuwa wamependezewa na wazo la kujiuzulu kwa Westerwelle, kwani kwao hakuna kiongozi mwengine ambaye anaweza kujaa kikamilifu kwenye kiti cha uenyekiti.

Alijisahau
Akiwa kama mwenyekiti wa chama, Westerwelle anaonekana na wakosoaji wake kwamba amekuwa muda mwingi kujiengea haiba yake mwenyewe huku akisahau wajibu wake kwenye chama, jambo ambalo wanaona ni sababu ya kupoteza kwenye chaguzi za Baden-Württemberg na Rheinland-Pfalz.

Matokeo kama haya yalipotokea kwenye mkoa wa Mainz, Westerwelle alisema kwamba angelipendelea kuendelea kubakia mwenyekiti wa FDP, lakini si sasa tena. Hata hivyo, Westerwelle hajapoteza yote. Bado anaendelea kushikilia nafasi zake za uwaziri wa mambo ya nje.

Hata mwenyekiti wa FDP katika mkoa wa Schleswig-Holstein, Wolfgang Kubicki, ambaye ni mpinzani mkubwa wa Westerwelle, anatambua heshima ya Waziri huyu wa mambo ya nje.

"Kama FDP, tuna mengi ya kumshukuru Guido Westerwelle. Alikichukua chama hiki kutoka chini kabisa na kukiinua juu. Anatekeleza wajibu wake wa uwaziri wa mambo ya nje kwa ufanisi licha ya matatizo mengi, na kwa hili hapana suala la kumng'oa kwenye nafasi hizo." Anasema Kubicki.

Linapokuja suala la mrithi wa kiti cha Westerwelle, kwa sasa inaonekana kuwa, macho ya chama hiki cha kiliberali yanamuelekea sana Waziri wa Afya, Phillip Rösler, kijana wa miaka 38, mzaliwa wa Vietnam, aliyelelewa na wazazi wa Kijerumani kutoka jimbo la Niedersachsen, na ambaye alianza siasa tangu akiwa daktari kwenye jeshi la Ujerumani.








Dawa ya Loriondo ni salama




HATIMAYE uchunguzi wa kisayansi uliofanywa na Serikali kuchunguza dawa inayotolewa na Mchungaji Mstaafu Ambilikile Mwaisapile [78] huko kijiji cha Samunge, Loliondo, Wilayani Ngorongoro,Mkoani Arusha, umebainisha kuwa dawa hiyo ni salama.
Taarifa hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Bw. Charys Gulllum baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo.

Gullum alisema kuwa utafiti walioufanya kuhusiana na dawa hiyo wamebaini na kuridhika kuwa dawa ya BABU haina madhara yeyote kwa mtumiaji wa dawa hiyo.

Alibainisha kuwa uchunguzi huo ulikamilika baada ya kuchukua sampuli ya dawa hiyo na kuifanyia utafiti wa kina uliochunguzwa na wataalamu waliobobea kutoka mamlaka ya hiyo.

Pia Taasisi ya Utafiti wa Dawa za Asili ya Chuo Kikuu cha Afya ya Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Mkemia Mkuu wa Serikali (CGC) na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) walibariki dawa hiyo kuwa haina madhara kwa binadamu.

Hata hivyo Gulllum alisema hatua ya awali imekamilika na hatua inayofuata ni kuchunguza ili kubaini kama kweli inatibu magonjwa aliyoorodhesha babu huyo






Westerwelle ausifu ujasiri wa Mubarak







Rais aliyeondolewa madarakani nchini Misri Hosni Mubarak Waziri wa mambo ya kigeni ya Ujerumani Guido Westerwelle ameyataka mataifa ya Kiarabu kuingia zaidi katika utaratibu zaidi wa kidemokrasia, baada ya kuangushwa utawala wa Mubarak

Ujerumani inakalia kwa mara ya kwanza kiti katika baraza la usalama la umoja wa mataifa. lakini matukio nchini Misri ambapo rais Hosni Mubarak amejiuzulu kutoka madarakani, yamefunika hatua hiyo ya Ujerumani kujiunga na baraza hilo la usalama la umoja wa mataifa. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle akiwa mjini New York kuzindua kuingia kwa Ujerumani katika baraza hilo, amekaribisha uamuzi wa rais Mubarak , baada ya wiki kadha za maandamano na kuyataka mataifa ya Kiarabu kuingia zaidi katika utaratibu wa kidemokrasia. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon ametoa wito wa kuwapo utaratibu wa amani katika hatua za mpito kuelekea demokrasia zaidi.

Si kwa kutumia hali ya utaratibu mzuri wa baraza la usalama la umoja wa mataifa , kuhusiana na majadiliano ya mada zilizopo. Ambapo wanachama 15 wa baraza hilo la umoja wa mataifa wakijadili suala la amani ya kimataifa pamoja na usalama, kunakuwa na hali ndogo ama kubwa ya mivutano katika majadiliano yao ambayo yamekwisha tayarishwa mapema , hali ambayo haikuwapo katika mitaa ya mjini Cairo , ambapo waandamanaji waliweza kuzika enzi ya utawala. Ni kwa njia ambazo si rasmi, ni kwa ujumbe mfupi wa simu za mkononi, barua pepe katika mtandao wa internet, ambazo zimeweza kukamilisha hatua ya kumlazimisha Hosni Mubarak kujiuzulu. Taarifa hizo zimemlazimisha waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle , kusitisha kwa muda kujitokeza kwake katika baraza la usalama kwa mara ya kwanza na kusema.
Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle
Tumefurahi, kwamba sasa njia iko wazi kwa mwanzo mpya wa kisiasa, kuelekea katika demokrasia na kuleta amani ndani na nje ya nchi hiyo.

Ni baina ya furaha na shauku , ambapo maneno ya waziri wa mambo ya kigeni yalikuwa yanaonesha, na usiku baada ya hotuba iliyokatisha tamaa ya Mubarak Alhamis usiku, Westerwelle alieleza wasi wasi wake kuhusu utatuzi wa amani katika mzozo huo wa Misri. Baada ya hapo ambapo ilikuwa ni hatua ya ghafla na ya mshangao, waziri Westerwelle amerejea pendekezo lake, la kuunga mkono ujenzi mpya wa mfumo mpya wa kisiasa.








Utawala wa Ujerumani uko tayari, amesema Westerwelle pembezoni mwa ushirika wao wa karibu kusaidia mabadiliko hayo ya kidemokrasia. Lakini pia shauku kuhusiana na kuondoka madarakani kwa Mubarak inaweza kuporomoka kutokana na hali jumla ambayo haieleweki kuhusiana na suala la , nani na kitugani kinakuja baada ya hapa.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-Moon ametoa wito, kama anavyosema , wa utaratibu wa uwazi na ulioratibiwa kwa njia sahihi katika kipindi hiki cha mpito, kutekeleza matarajio halali ya umma wa Misri.


Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon
Ni muhimu , kwamba haki za binadamu na uhuru wa raia vinaheshimiwe bila kuwekewa mipaka.

Amesema Ban na kuongeza.

Naupongeza uamuzi mgumu aliochukua Mubarak kwa maslahi ya umma wa Misri.

Dunia pamoja na wadau wanatoa wito upatanishi wa kweli. Ni hakika kwa Berlin sio tu imeanza ushirikiano wa kweli na Tunisia , lakini pia watakuwa na mahusiano mazuri na Misri na kutafuta washirika muhimu wa mazungumzo katika serikali pamoja na upande wa upinzani.











Ujerumani haitoiacha Afghanistan mkono! asema,Westerwelle.



Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle akiwa KunduzWaziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Guido Westerwelle amefanya ziara yake ya kwanza nchini Afghanistan tangu kuushika wadhifa huo mwaka 2009.


Kiongozi huyo amewatembelea wanajeshi wa Ujerumani wanaopiga doria kwenye eneo la kaskazini mwa Afghanistan. Wakati huo huo Waziri Westerwelle ameahidi kuusadia uongozi wa Afghanistan katika harakati zake za kuwadhibiti wanamgambo.Akiwa katika ziara yake hiyo iliyodumu kipindi cha saa tatu, Waziri wa Mambo ya Nje Guido Westerwelle na naibu Kansela wa Ujerumani waliwasifu wanajeshi hao kwa kuyahatarisha maisha yao ili kuulinda uhuru na usalama. Waziri Westerwelle anatarajiwa pia kukutana na gavana mpya wa jimbo la Kunduz, Muhammad Anwar Jegdalek, aliyechaguliwa baada ya mtangulizi wake kuuawa mwezi wa Oktoba mwaka uliopita.

Mashada ya kumbukumbu

Kiongozi huyo anatazamiwa pia kuweka shada la maua kama kumbukumbu ya wanajeshi wa Ujerumani waliouawa wakipiga doria.

Hapo jana alikutana na rais wa Afghanistan Hamid Karzai na kwa pamoja walitoa wito wa kuyaimarisha mapambano dhidi ya biashara ya madawa ya kulevya na ufisadi vilevile kuyalinda makundi madogo ya kidini.

Ziara hii inafanyika wakati ambapo Bunge la Ujerumani linasubiriwa ifikapo mwishoni mwa mwezi huu kuiamua hatma ya majukumu ya wanajeshi wake wanaopiga doria Afghanistan. Endapo bunge litaridhia, wanajeshi hao wataanza kuondoka Afghanistan ifikapo mwishoni mwa mwaka huu kama ilivyopendekezwa baada ya kuyazingatia mazingira yaliyopo. Waziri Westerwelle anaeleza kuwa,''Mwaka wa 2011 ndio utakaoiamua hatma ya suala hilo la Afghanistan kwani ndipo mchakato mzima wa kuyakabidhi majukumu ya usimamizi wa usalama utakapoanza.''




Kansela Angela Merkel alipowatembelea wanajeshi wa Ujerumani Disemba iliyopita
Afghanistan kuungwa mkono

Uamuzi huo wa bunge pia utaiidhinisha hatua ya kuiongeza idadi ya wanajeshi waliopo Afghanistan kutoka 4,415 hadi 5350. Wengi ya wanajeshi hao wanapiga doria katika eneo la Kunduz. Kwa upande wake Waziri Westerwelle alisema kuwa ana imani Bunge litayaidhinisha mapendekezo hayo. Hata hivyo alisisitiza kuwa ,'' Ujerumani kamwe haitoiacha Afghanistan katika miaka ya baada ya 2014, tutaendelea kuutimiza wajibu wetu kwani azma yetu ni kufanikiwa wala sio kuyatelekeza majukumu yetu ya kiusalama katika mapambano dhidi ya ugaidi,'' kama njia ya kupambana na ugaidi.

Vikosi vya ISAF

Waziri Westerwelle alikuwa akitokea Pakistan alikotoa wito wa ushirikiano zaidi katika vita dhidi ya ugaidi na kwamba mchango wa Pakistan una umuhimu mkubwa. Mapigano yanaripotiwa kuongezeka katika eneo la kaskazini mwa Afghanistan hasa baada ya vikosi vinavyosimamiwa na ISAF chini ya mwamvuli wa NATO kwa ushirikiano na wanajeshi wa Afghanistan wameziimarisha harakati zao za kupambana na uasi.

Ili kulithibitisha hilo hapo jana jioni wapiganaji wa Taleban walipambana na wanajeshi wa NATO na Afghanistan katika mkoa wa Dasht-e-Archi, shambulio lililowaua wapiganaji 15 na kamanda mmoja.



Ramani ya maeneo ya doria ya vikosi vya ISAF:Wanajeshi kuanza kuondoka Afghanistan mwaka huu
Vikosi hivyo vya Jumuiya ya Kujihami ya mataifa ya magharibi NATO itaanza rasmi kuyakabidhi majukumu ya usalama kwa wanajeshi wa Afghanistan mwaka huu. Mchakato huo unatarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2014.











Westerwelle ataka msimamo wa EU kuhusu Alexander Lukashenko wa Belarus.





Alexander Lukashenko wa Belarus.


Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle.Msimamo huo ni kuhusu ukandamizaji unaoendelea chini ya uongozi wa Rais Alexander Lukashenko wa Belarus.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle amesema kuwa Umoja wa Ulaya unatakiwa kutoa jibu la wazi la kisiasa juu ya ukandamizaji unaofanywa chini ya utawala wa Rais Alexander Lukashenko nchini Belarus. Matamshi hayo ni kwa mujibu wa gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung.

Westerwelle amesema Umoja wa Ulaya unatakiwa kukabiliana na uongozi wa kisiasa wa Belarus kutokana na taarifa za rushwa katika uchaguzi na ukandamizaji nchini humo.

Ujerumani imekuwa miongoni mwa wakosoaji wakali wa Belarus, wakati ambao nchi hiyo inaendelea kuwashikilia mamia ya wafuasi wa upinzani ambao walikamatwa wakati wa maandamano makubwa kupinga uchaguzi wenye utata wa Desemba 19, uliompa ushindi Lukashenko.

Siku ya Ijumaa, Belarus iliamuru kufungwa kwa ofisi ya Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya, kwenye mji mkuu wa Minsk, baada ya shirika hilo kukosoa vikali uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment