Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Monday, April 11, 2011

Mshirika wa Gbagbo alisema, wanajeshi wa Ufaransa wamemkamata




Mshirika wa Gbagbo alisema, wanajeshi wa Ufaransa wamemkamata kiongozi wa Ivory Coast Laurent Gbagbo kutoka kwenye makazi yake na kumkabidhi kwa upinzani.




Inaripotiwa kuwa waliingia baada ya vifaru vya Ufaransa kuingia katika makazi yake kwenye mji mkuu wa Ivory Coast, Abidjan, kufuatia mashambulio ya helikopta ya Ufaransa na Umoja wa Mataifa.



Bw Gbagbo alikataa kukabidhi madaraka kwa Alassane Ouattara, anayetambuliwa kimataifa kuwa mshindi wa urais nchini humo.

Majeshi ya Umoja wa Mataifa ya kutunza amani yanayashutumu majeshi ya Bw Gbagbo kuhatarisha maisha ya raia.



Msemaji wa Rais Toussaint Alain aliliambia shirika la habari la Reuters kutoka Paris, "Gbagbo amekamatwa na majeshi maalum ya Ufaransa nyumbani kwake na amekabidhiwa kwa wapinzani."















Serikali ya Gaddafi yakubali mpango wa amani,asema Zuma
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anasema serikali ya Libya imekubali mpango wa amani wa muungano wa Afrika ili kumaliza mapigano ya miezi miwili.

Bwana Zuma na viongozi wengine watatu wa Afrika walikutana na kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi, mjini Tripoli siku ya Jumapili

.Sasa wanaelekea katika eneo la Benghazi linalodhibitiwa na waasi mashariki mwa nchi.

Katika eneo la Ajdabiya,vikosi vinavyomuunga mkono Gaddafi vimewazidi nguvu waasi katika mapigano.




Shirika la Nato linasema ndege zake zimeshambulia vifaru 25 vya serikali katika siku ya Jumapili pekee.



Mpango wa muungano wa Afrika unatoa wito wa kusitishwa kwa mapigano mara moja, kufunguliwa njia kwa ajili ya kusafirisha misaada na mazungumzo kufanyika kati ya serikali na waasi.


"muhimu kusitisha mapigano," alisema rais Zuma,baada ya mazungumzo yaliyochukua saa kadhaa.



Mfumo ambao mchakato huo utachukua mtaelezwa baadaye katika taarifa zetu,alisema Bwana Zuma.

Mwakilishi wa upinzani aliye Uingereza,


,akizungumza na BBC amesema kuwa wataangalia kwa makini mpango huo wa muungano wa Afrika,lakini mpango wowote ulio na nia ya kumuacha Gaddafi au wanawe madarakani hautokubalika.













Tetemeko lingine la ardhi latokea Japan!


Tetemeko lingine latokea huku Japan ikiendelea kuomboleza


Tetemeko lingine kubwa la ardhi limetokea nchini Japan,

wakati nchi hiyo ilikuwa katika shughuli za kulikumbuka jana lililotokea mwezi mmoja ukiwa uliopita, tetemeko la ardhi ambalo lilisababisha tsunami, na kuliangamiza eneo la kaskazini mashariki mwa nchi.

Tetemeko la hivi karibuni lenye kipimo cha, nguvu zake hasa zilisikika zaidi kusini mwa Fukushima, ambako kinu cha nuklia kiliharibiwa sana mwezi uliopita.

Wafanyikazi katika eneo hilo waliondolewa wakati huo.

Mapema, serikali ilikuwa imetangaza kwamba itapanua eneo ambalo litafikiriwa kuwa ni hatari Fukushima, na kuwaondoa raia ili kuepuka mionzi ya nuklia.

Awali, raia walinyamaza kimya kwa kipindi cha dakika moja, katika hali ya kuwakumbuka watu 13,000 walioangamia mwezi mmoja uliopita.










Misri:Mubarak kuhojiwa juu ya mauaji

Aliyekuwa rais wa Misri Hosni Mubarak ametakiwa kufika mbele ya mwendesha mashtaka mwandamizi wa serikali kuhojiwa juu ya madai ya ufisadi na mauaji ya waandamanaji.

Tangazo hilo limejiri muda mfupi baada ya Bwana Mubarak kutoa taarifa yake ya kwanza tangu kuondolewa madarakani miezi miwili iliopita,akikanusha madai ya ufisadi.


Kiongozi huyo wa zamani amesema ana haki ya kutetea heshima yake na akakanusha kuwa na mali yoyote katika nchi za kigeni.

Watoto wa Mubarak Gamal na Alaa pia wametakiwa kufika kwa mahojiano.

Mwendesha mashtaka mwandamizi amesema taarifa ya Mubarak, haitoathiri kwa vyovyote uchunguzi huo.

Siku ya Ijumaa,eneo la Tahrir mjini Cairo lilikuwa na waandamanaji wakitaka Bwana Mubarak na jamii yake kushtakiwa kwa ufisadi.

Mtu mmoja aliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati maafisa wa usalama walipoingia kufukuza walioandamana.Walikuwa na majeraha ya risasi lakini jeshi lilikanusha kutumia risasi za moto.

Waandamanaji na wanaharakati wanaopinga ufisadi wamekuwa wakishinikiza kufanyiwa uchunguzi mali za familia ya Mubarak,zinazosemekana kuwa kati ya $1bn hadi $70bn











Besigye akamatwa Uganda


Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Uganda, Dk Kizza Bessigye, amekamatwa katika mji mkuu wa Kampala.


Besigye amewataka raia wa Uganda kupinga ongezeko la bei za bidhaa muhimu
Dk Besigye alikamatwa lna kubebwa kwa gari la polisi, alipokuwa akitembea kutoka nyumbani kuelekea kazini.





Dk Besigye alikuwa amewataka raia wa Uganda kutembea kutoka nyumbani hadi kazini, kama njia moja ya kupinga ongezeko kubwa la bei ya vyakula na mafuta.




Mwandishi wa BBC mjini Kampala anasema kuna watu wengi waliokamatwa, ikiwa ni pamoja na wanasiasa wachache wa upinzani.








Serikali ya Somalia kususia kongamano la UN





Kongamano la Umoja wa Mataifa kujadili hali ya Somalia pamoja na hatima ya serikali ya mpito ambayo kipindi chake kinamalizika mwezi Agosti mwaka huu linaanza juma hili mjini Nairobi.

Kikao hicho kinaanza huku Waziri Mkuu wa Somalia Mohammed Abdullahi

akitangaza kususia na kusisitiza kwamba masuala yote ikiwemo mashirika ya kusaidia Somalia yanafaa kuwa mjini Mogadishu.

Zaidi ya wafanyakazi elfu moja wanaotoa misaada kwa Somalia wanaendesha shughuli zao kutoka Kenya

Serikali ya mpito ya Somalia imesema itasusia mkutano ulioandaliwa na umoja wa mataifa mjini Nairobi juma hili.Waziri mkuu wa Somalia Mohammed Abdullahi anasema wanasusia mkutano huo kwa kuwa walitaka mkutano ufanyike mjini Mogadishu.


Mkutano huu umependekezwa na mjumbe maalum wa umoja wa mataifa juu ya mzozo wa Somalia Augustine Mahiga,na ulikuwa na nia wa kuleta pande zote zinazozozana nchini humo pamoja.

Serikali ya Somalia inataka mashirika yote ya umoja wa mataifa ihamishie shughuli zake nchini Somalia



''Sisi tunajua mashirika ya umoja wa mataifa yametumia pesa nyingi mamilioni ya madola hata pengine dola bilioni moja na tunataka wawe karibu na watu wanaodai wanawahudumia na pia tunataka wajionee hali ilivyo wenyewe Somalia'' alisema waziri mkuu.


Tayari baadhi ya wajumbe wameanza kuwasili mjini Nairobi tayari kwa mkutano.Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa kuanza siku ya Jumanne.

No comments:

Post a Comment