Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Friday, August 13, 2010

Waislamu Duniani Waanza Mfungo wa Ramadhan


Waislamu duniani leo wanaanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan huku wengine wakitarajiwa kuanza kufunga kesho alhamisi.
Waislamu wanauanza mwezi wa tisa wa kalenda ya kiislamu ambao hujulikana zaidi kama mwezi wa Ramadhan kwa kujizuia kula na kunywa kuanzia alfajiri jua linapochomoza hadi jioni jua linapozama. Kufunga ni mojawapo ya nguzo tano za Uislamu.

Kuanza na kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan hutegemea na kuandama kwa mwezi lakini kumekuwa na mgongano juu ya njia za kugundua kuandama kwa mwezi. Baadhi ya nchi hutaka mwezi lazima uonekane kwa macho na hukataa kutambua kuandama kwa mwezi kwa kutumia njia za kisayansi.

Nchini Saudi Arabia, televisheni ya taifa ya Al-Ekhbariyah ilitangaza kuwa baraza linalohusika na kuthibitisha kuandama kwa mwezi limetoa taarifa kuwa jumatano ndio mwanzo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Nchi za Qatar, UAE, Bahrain, Kuwait, Misri, Syria, Lebanon, Yemen nazo zimetangaza kuwa mwezi wa Ramadhan unaanza leo jumatano.

Baraza la Waislamu la Jordan lilitangaza kuwa mwezi haujaonekana nchini humo lakini kwakuwa umeonekana nchi za jirani basi na wao wataanza kufunga leo jumatano.

Hata hivyo nchi ya Oman imetangaza kuwa wao wataanza kufunga alhamisi kwakuwa hawajauona mwezi nchi humo.

NIFAHAMISHE.COM inawatakia waislamu wote duniani mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

No comments:

Post a Comment