Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Wednesday, August 4, 2010

Rose Ndauka amtwanga Doreen

Nyota wa filamu ya Swahiba, Rose Ndauka anadaiwa kumwachia kichapo hevi, msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Doreen Mkude kwa kile kilichosemekana kuwa, ni umbeya uliofanywa na Mbongofleva huyo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo lilitokea hivi karibuni maeneo ya Kinondoni, jijini Dar kwenye makazi ya Doreen. Habari zinapasha kuwa, ishu kubwa ilianzia kwa mchumba wa Rose ambaye anaishi jijini Tanga kumpigia simu Rose na kumvurumishia tabia na mwenendo wake wa usiku.

“Jamaa (wa Rose) si anaishi Tanga, sasa mara nyingi amekuwa akimpigia simu Rose na kumsema ni kwanini anazurura sana usiku?” Kilisema chanzo hicho.
Doreen Mkude

Kikasema kuwa, shutuma hizo zilimfanya Rose aanze kufikiria kwa kina na kubaini kuwa, mara zote anazopigiwa simu na jamaa yake huyo, jana yake usiku alikuwa ‘kiwanja’.

Habari zinazidi kupasha kwamba, baada ya kuweka akili sawa kichwani, Rose akagundua kuwa, Doreen ambaye ni rafiki yake kipenzi toka utotoni, ndiye amekuwa akimmegea ishu kamili jamaa yake huyo.

Chanzo kikasema: “Rose bila kuchelewa, alimfungia safari Doreen mpaka kwao ambapo ‘alimshikisha’ adabu kwa kumpa kichapo huku akimwambia aache kufuatilia uchumba wake na jamaa huyo.”

Hata hivyo, kwa mujibu wa chanzo hicho, palitokea patashika za huku na kule ambapo Doreen alionekana kujitetea asishindiliwe mangumi zaidi na ‘hasimu’ wake huyo.

Habari zinasema kuwa, mbali na kipondo hicho, Doreen aliweka msimamo wake kuwa, licha ya tuhuma zilizoelekezwa kwake, lakini hata siku moja hajawahi kuwasiliana na mchumba wa Rose kwa jambo lolote lile achilia mbali umbeya huo.



Ili kuweka mambo sawa, inasemekana Doreen alimtwangia simu mama yake Rose na kumshatakia kuhusu binti yake huyo ambaye naye alimpasha mwanae kwa kumwambia anapaswa kujichunga mwenyewe zaidi kwa mwenendo na matendo badala ya kukurupukia kusingizia marafiki zake kwamba, wanamwambia maneno ya uongo mchumba wake.

Ili kuujua ukweli wa habari hizi, Amani lilianza kumsaka Doreen kwa simu yake ya mkononi ambapo alipopatikana alisema hayuko tayari kuongelea kwa undani suala hilo kwa sababu ni la kifamilia zaidi.

“Niseme nini, hayo mambo ya kifamilia zaidi bwana, achana nayo,” alisema Doreen na kukata simu.

Aidha, kwa upande wake, Rose alipobambwa hewani na kuhojiwa kuhusu ishu nzima alisema matatizo hayo yalimalizika kifamilia zaidi na si suala la kuwekwa kwenye vyombo vya habari.

No comments:

Post a Comment