Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Wednesday, August 4, 2010

LULU APIGANIA MWANAUME

Na Shakoor Jongo
Mwigizaji ‘sidanganyiki’ katika kiwanda cha filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na kundi lake wamejikuta katika matatizo makubwa baada ya kudaiwa kumvamia na kumpiga binti mmoja aliyefahamika kwa jina la Husna Maulid, mkazi wa Magomeni Kagera, Dar, chanzo kikisemekana kuwa ni mwanaume, Amani linakudondoshea.

Tukio hilo lilijiri hivi karibuni ambapo inadaiwa Lulu ‘alimtilia maguu’ Husna nyumbani kwao na kumshambulia kwa maneno kabla ya kumshushia kipigo akiwa na mashotito zake khao wa madai kuwa, ‘anatoka’ na king’asti wake aliyetajwa kwa jina moja la Kiba.



Elizabeth Michael ‘Lulu’

Awali ilidaiwa kwamba, juzikati Lulu akiwa na king’asti wake huyo maeneo ya Mlimani City, mara iliingia meseji kwenye kilongalonga cha mwanaume huyo ambapo ‘kinda’ huyo anayefanya vizuri kwenye filamu mbalimbali aliamua kung’ang’ania kuisoma na kukuta maneno ya mapenzi kutoka kwa Husna.

Ikazidi kunyetishwa na mdaku wetu kwamba, kufuatia meseji hiyo Lulu akiwa na marafiki zake walifunga safari hadi nyumbani kwa Husna na kumshushia mtiti wenye uzito wa kilo kadhaa.

Kufuatia ishu hiyo, Husna ambaye aliwahi kushiriki shindano la Miss Dar City Centre mwaka jana, aliamua kwenda kituo cha polisi cha Magomeni na kufungua jalada la kesi lenye namba MAG/RB/ 12468/10.

Husna ambaye aliwahi kushiriki shindano la Miss Dar City Centre mwaka jana

Baada ya kupata taarifa hizo, mwandishi wetu alimvutia waya Lulu na kumuuliza juu ya tukio hilo ambapo alikiri kutokea lakini akadai kuwa, walishaombana msamaha na kusameheana.

No comments:

Post a Comment