Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Monday, August 16, 2010

Staili Mpya ya Wizi Ufaransa

Staili mpya ya wizi imeibuka nchini Ufaransa ambapo wanawake vibaka huwachengua wanaume wanaotoa pesa kwenye ATM kwa kuwaonyesha matiti yao ili kuwazubaisha waweze kuwaibia.
Staili mpya ya wizi imeibuka nchini Ufaransa ambao wezi ni wanawake na wanaoingizwa mjini huwa ni wanaume.

Katika staili hii ya wizi, wanawake wawili humsogelea mwanaume anayetaka kutoa pesa toka kwenye mashine za kutolea pesa (ATM) na pindi mwanaume huyo anapoingiza pin number yake, mwanamke mmoja huyatoa matiti yake nje na kuanza kumuonyesha mwanaume huyo ili kumzubaisha wakati mwanamke wa pili hutumia fursa hiyo kutoa kiasi cha pesa anachotaka toka kwenye ATM na kisha kutimua mbio.

Katika tukio la hivi karibuni, wanawake wawili wenye umri kwenye miaka ya 20, walinaswa na kamera za ulinzi wakitumia staili hiyo kumuibia pesa mwanaume mmoja jijini Paris.

Taarifa ya polisi ilisema kuwa kamera za ulinzi zilifanikiwa kulinasa tukio hilo lakini sura za wanawake hao vibaka hazikuonekana vizuri.

Msemaji wa polisi aliwaonya wanaume kuwa wakati wanapotoa pesa toka kwenye ATM wajitahidi kuwa makini na wasizubaishwe na vishawishi au matukio yatakayotokea karibu yao

No comments:

Post a Comment