Jeshi la wanamaji la Italia limesema maharamia wamekwea na kuchukua udhibiti wa meli ya mafuta ya Italia katika bahari ya Hindi.
Meli ya Ujerumani ambayo pia imetekwa
Maharamia hao walifyatua risasi katika chombo kiitwacho Savina Caylyn, takriban kilomita 800 kutoka pwani ya Somalia.
Msemaji wa jeshi la wananamaji amesema hakuna aliyejeruhiwa miongoni mwa mabaharia 17 kutoka India na wataliano watano.
Maharama wamejipatia mamilioni ya dola
Msemaji wa jeshi la wanamaji la Umoja wa Ulaya amesema shambulio la chombo hicho limefanyika katika eneo la mashariki mwa kisiwa cha Yemen cha Socotra.
Meli hiyo imebeba shehena ya mafuta yaliyokuwa yakipelekwa katika bandari ya Pasir Gudang nchini Malaysia, limeripoti shirika la habari la Reuters
Wanajeshi wa Marekani wakiwa na maharamia
Meli ya kivita ya Italia ilikuwa ikielekea katika eneo la tukio, lakini iko umbali wa kilomita 600, na inatarajia kuchukua siku kadhaa kuwasili, limeripoti shirika la habari la Italia.
Umoja wa Ulaya umesema meli hiyo imetekwa na mashua moja ikiwa na maharamia watano
Maharamia wa Somalia
Msemaji wa jeshi la wanamaji wa Umoja wa Ulaya amesema meli hiyo "ilikuwa ikielekea magharibi," upande wa pwani ya Somalia, shirika la habari la AFP limekaririwa.
Maharamia wa Kisomali wametjipatia mamilioni ya dola katika miaka ya hivi karibuni kwa kuteka meli za mizigo katika njia inayotumiwa na meli katika pembe ya Afrika.
No comments:
Post a Comment