Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Tuesday, February 1, 2011

Kashfa nyingine Mwananyamala


VICHANGA 10 wanaodaiwa kufa katika hospitali ya Mwananyamala wamekutwa wamekufukiwa katika shimo la futi moja na nusu kwa pamoja.
Vichanga hivyo vimekutwa vimezikwa maeneo ya Mwananyamala Kwa Msisiri pembezoni mwa makaburi ya Kwa Kopa na tukio hilo kuvuta watu wengi kufika neo hilo kushuhudia tukio hilo.

Vichanga hivyo vimeviringishwa katika shuka moja lenye nembo ya hospitali hiyo na kuzikwa katika shimo moja lenye urefu futi moja na nusu.
Maiti hizo zimekutwa katika eneo la Mwananyamala Msisiri, jijini Dar es Salaam, pembezoni mwa makaburi ya kwa Kopa mita chache kutoka katika hospitali hiyo.

Maiti hizo zilibainika kwenye eneo hilo na mtu mmoja aliyefahmaika wka jina la MBaga alipokuwa akifanya usafi katika eneo hilo majira ya saa 3 asubuhi na kubaini shimo hilo.
Aliona shimo ambalo lilikuwa haliajaa taka na aliposegelea ndipo aliona mkono wa kichanga kimoja na ndipo aliwaita majirani wa karibu kasha kulipoti tukio hilo kituo cha polisi Oysterbay.

Ndipo polisi walipofika eneo hilo wakafukua na kukuta maiti za watoto wachanga 10 na zilikuwa zimeshaharibika na kukatika viungo wakati wanatolewa shimoni humo.

Maiti hizo zilikuwa zimezikwa na plasta zao mikononi zilizoonyesha walikuwa wamtoka katika wodi moja hospitalini

Kufuatia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana alikutana na viongozi wa juu wa wilaya hiyo wakiwemo madaktari waandamizi kwenye ukumbi wa hospitali hiyo kuzungumzia tukio hilo mkutano uliochukua zaidi ya masaa mawili.

Hata hivyo jeshi la polisi mkoani Kinondoni wanafanuya uchunguzi wa kina kufuatia tukio hilo


Hata hivyo haijafahamika mara moja sababu ya vichanga hivyo kuzikwa kwa pamoja bila ya wazazi kujua

No comments:

Post a Comment