Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Saturday, January 29, 2011

Mke na mume wafumaniana kwa Sangoma -Dar


KATIKA hali isiyo ya kawaida mke na mume walifumaniana ana kwa ana kwa mganga wa kienyeji huko maeneno ya Mbagala.
Hali hiyo ilijitokeza juzi majira ya adhuhuri wakati kila mmoja akiwa amefika eneo hilo kusubiri huduma ya mtaalamu huyo.
Chanzo cha habari kilidai kuwa, mume ndiye aliyetangulia kufika eneo hilo na inadaiwa kuwa ndiye aliyetangulia kufika mahali hapo kupata huduma.

Mke huyo bila kutambua kama angemkuta mume wake hapo alifika eneo hilo akiwa na rafiki yake walifika na kutafuta mahali wakaketi huku wakiwa katika hali ya kusubiri kuingia kwa mtaalamu huyo kupata huduma.

Ndipo mume huyo aliposhindwa uvumilivu na kujitokeza na kumfata mke wake mahali alipokuwa ameketi na mke huyo alitamani kukimbia baada ya kumona mume wake mahali hapo.

Ndipo mume huyo alipoanza kumuuliza mke wake mbele ya hadhara alikuwa akisubiri nini mahali hapo.

Imedaiwa mke huyo alipatwa na kigugumizi kumuona mumewe mahali hapo ndipo alipomjibu alikuwa amemsindikiza rafiki yake alikuwa na shida, ndipo mume huyo alipoanza varangati na kuanza kuripoka na kujikuta akitoa siri iliyomfikisha mahali hapo.

Imedaiwa mume alimuuliza mkewe hivi “ umefata nini hapa wewe mwanamke? Mbona uridhiki wewe umekuja kuniroga wewe sasa leo nimekugundua”

Hata hivyo imedaiwa kuwa mwaneamdke huyo alimjibu kuaw “ hapana sijaja kukuroga, nilikuwa na shida nyingine mume wangu” lakini weote tuna makosa Mungu ametukutanisha hapa”

Mume huyo alijibu “ Mimi si unajua kuwa nina matatizo kule kazini kwangu, watu wananifanyia fitina niondolewe kile cheo ndio mana nimekuja sasa wewe unashida gani yakuja hapa.

Baada ya jibu hilo watu waliokuwa karibu na wanandoa hao wakati wa mazungumzo hayo walipata jibu kuwa baba huyo alikuwa na shida ipi iliyomleta mahali hapo.

Hivyo imedaiwa mke huyo hakuwahi kuingia kwa mtaalamu huyo baada ya mume wake kumuamrisha aondoke mahali hapo.

Chanzo hiki cha habari kilidai kuwa hata hivyo hali haikuwa shwari hata walivyofika nyumbani kwao na kitakachojiri kitaendelea kuwajia

No comments:

Post a Comment