Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Tuesday, January 11, 2011

Kanisa Katoliki

Papa Benedikto XVI, askofu wa Roma na mkuu wa Kanisa Katoliki


Jina hilo linatumika hasa kumaanisha Kanisa la Kikristo linalokubali mamlaka ya Papa wa Roma kama mkuu wa Maaskofu juu yake lote.

Kanisa hilo linaamini kuwa ndani yake linadumu moja kwa moja Kanisa pekee lililoanzishwa na Yesu Kristo ambalo wanaunganishwa nalo wote wanaobatizwa katika madhehebu yoyote. Tofauti kati yao ni kwamba baadhi (Wakatoliki) wana ushirika kamili nalo, wakati wengine (hasa Waorthodoksi na Waprotestanti) wana ushirika nalo la viwango mbalimbali, kadiri wanavyokubali mafundisho, sakramenti na uongozi wake.

Neno "katoliki" linatokana na kivumishi cha Kigiriki καθολικός (katholikòs), lenye maana ya «kamili, kadiri ya utimilifu». Kwa mara ya kwanza liliandikwa na Ignas wa Antiokia kwa Wakristo wa Smirna mwanzoni mwa karne II: «Alipo Yesu Kristo ndipo lilipo Kanisa Katoliki» (Ad Smyrnaeos, 8).

Kati ya madhehebu ya Kikristo, Kanisa Katoliki linakusanya waamini 1,147,000,000, yaani nusu ya wafuasi wote wa Yesu, na 17.3 % ya binadamu wote, likiwa na asilimia kubwa ya waamini kati ya wananchi wa Amerika na Ulaya.

Kanisa Katoliki linaishi katika majimbo karibu 3,000, ambayo kwa kawaida yanaongozwa na Maaskofu wakisaidiwa na mapadri na mashemasi; kati ya hayo, mengi yanafuata mapokeo ya magharibi, lakini machache mapokeo ya mashariki. Majimbo yanagawanyika katika parokia zinazoongozwa na padri anayeitwa paroko.

Kati ya waamini wana nafasi ya pekee wamonaki na watawa wengine ambao wanaishi kwa mitindo iliyostawi katika historia ya Kanisa ili kumfuata Yesu kwa karibu zaidi katika useja mtakatifu, ufukara na utiifu



Utatu

Utatu



Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jina hilo la kiteolojia linatumika kufafanulia imani ya Wakristo wengi kwamba Mungu pekee, sahili kabisa, ni Nafsi tatu zisizotenganika kamwe: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Kwa agizo la Yesu watakaomuamini wanatakiwa kubatizwa kwa jina la hao watatu (Mathayo 28:19).

Umoja wa Nafsi hizo unatokana na asili yake pekee, yaani Baba ambaye ndani mwake anamzaa milele Mwana kama mwanga toka kwa mwanga, kama Neno au Wazo lake (Hekima), tena anamvuvia Roho Mtakatifu kama Upendo ambao unamuunganisha na Mwana na kukamilisha umoja wao.

Kimsingi ni kwamba Mungu pekee anajifahamu na kwa kujifahamu anajipenda.

Imani hiyo ilizidi kufafanuliwa hasa katika karne IV, mitaguso mikuu ya kwanza ilipochukua msimamo dhidi ya wazushi waliokanusha umungu wa Yesu na wa Roho Mtakatifu. Ilipata muundo wa kudumu katika Kanuni ya Imani ya Nisea-Kostantinopoli inayotumika hadi leo katika madhehebu mengi.

No comments:

Post a Comment