Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Saturday, January 29, 2011

Binti wa Miaka 14 Achapwa Bakora 100 Kwa Kuzini, Afariki


Polisi nchini Bangladesh wanawashikilia watu wanne na ikiendelea kuwatafuta watu wengine 14 waliomhukumu kwa kosa la kuzini na walioshiriki kumcharaza bakora 100 mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 14 ambaye alifariki wakati alipocharazwa bakora ya 80
Mosammet Hena alifariki hospitali jumapili baada ya kucharazwa bakora 80 kati ya 100 alizohukumiwa kucharazwa na mahakama ya kijiji kwa kutuhumiwa kuzini na binamu yake mwenye umri wa miaka 40 ambaye alikuwa na mke.

Taarifa zaidi zimesema kuwa mke wa binamu yake aliyejulikana kwa jina la Shilpi Begum ndiye aliyemfungulia mashtaka Mosammet kwenye mahakama ya kijiji kinachotumia sharia za kiislamu akisema kuwa Hena ana uhusiano wa kimapenzi na mumewe na amekuwa akiwaona wakiongea sana pamoja.

Taarifa zilizopatikana baadae zilisema kuwa Mosammet alibakwa na binamu yake huyo na baadae kutuhumiwa kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.

Mahakama hiyo ya kijiji iliwaona wote wawili wana hatia na iliwahukumu wacharazwe bakora 100 kila mmoja.

Mosammet alikamatwa na kutolewa toka nyumbani kwa wazazi wake na kucharazwa bakora 100 mbele ya wanakijiji. Wakati alipocharazwa bakora ya 80 alizimia na alifariki wakati akiwahishwa hospitali.

Bangladesh haifuati sheria za kiislamu lakini viongozi wa kijiji hicho walijiamulia wenyewe kuwahukumu watu kwa sheria za kiislamu.

Polisi wamewatia mbaroni watu watatu akiwemo Shilpi na imamu aliyetoa hukumu ya kucharazwa bakora Mosammet, ambapo wote wamemfunguliwa mashtaka ya mauaji. Polisi inawatafuta watu wengine 14 ambao walishindwa kuzuia Mosammet asicharazwe bakora 100.

Mume wa Shilpi anatafutwa na polisi baada ya kutoroka kijijini kabla ya kucharazwa bakora 100.

Mosammet alizikwa jana kwenye makaburi ya familia yake kwenye kitongoji cha Naria, Shariatpur, kusini mwa mji mkuu wa Dhaka

No comments:

Post a Comment