Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Sunday, November 7, 2010

Askari akilinda kanisa moja Baghdad


Askari akilinda kanisa moja Baghdad


Kiongozi mmoja wa wakristo nchini Iraq, Askofu Athanasios Dawood, ameiambia BBC, kuwa Wakristo nchini Iraq, hawana mtu wa kuwalinda, na hawana la kufanya ila kuondoka nchini humo.


Askofu Dawood, alisema Marekani imeshindwa kutekeleza ahadi iliyotoa kuwapatia Wairaqi demokrasi, na kwamba maisha ya Wakristo yalikuwa bora zaidi, chini ya utawala wa Saddam Hussein.





Askofu Dawood alisema hayo nchini Uingereza, wiki moja baada ya waumini zaidi ya 50, kuuwawa ndani ya kanisa mjini Baghdad, baada ya kutekwa nyara na wapiganaji wa Kiislamu.


Lakini mbunge mmoja Mkristo nchini Iraq, Yonadem Kanna alisema, Wakristo wanafaa kubaki nchini humo, kupigania haki zao.

Inakadiriwa kuna waKristo nusu milioni nchini Iraq, maelfu kwa maelfu wakiwa wamekimbia tangu Marekani na washirika wake, kuivamia Iraq mwaka wa 2003.

No comments:

Post a Comment