Dini ni mfumo wa maishani
Saturday, June 18, 2011
Frederick Chiluba amefariki
Rais wa zamani wa Zambia, Frederick Chiluba, amefariki, akiwa na umri wa miaka 68.
Bwana Chiluba amekuwa na ugonjwa moyo kwa miaka kadha.
Rais Chiluba aliiongoza Zambia kwa mwongo mzima katika miaka ya '90, na baada ya kustaafu alishtakiwa kwa sababu ya rushwa.
Frederick Chiluba alipata urais wa Zambia mwaka wa 1991, wakati Afrika inaanza kuingiia katika demokrasi ya vyama vingi.
Kabla ya hapo alikuwa kiongozi wa wafanyakazi.
Aliahidi kuleta mabadiliko lakini alipochukua uongozi Zambia ilikuwa imeshafilisika, naye aliacha rushwa kustawi.
Alipojaribu kujiongezea muhula wa tatu wa madaraka, alipingwa.
Piya alilaumiwa kuwa akipenda maisha ya anasa.
Baada ya kuondoka madarakani mwaka wa 2001, mrithi wake, Levy Mwanawasa, alimshtaki kwa shutuma za rushwa.
Baada ya kesi ya miaka 6 kuhusu ubadhirifu wa mali ya taifa, Frederick Chiluba aliambiwa hakuwa na makosa. .
Lakini katika kesi nyengine iliyofanywa katika mahakama makuu ya London, Chiluba alikutikana na hatia ya kuiba mamilioni ya dola ya fedha za serikali ya Zambia, kwa kutumia akaunti kwenye mabenki ya London.
Marekani inazungumza na Taliban
Nchini Afghanistan Rais Karzai amethibitisha kuwa Marekani na mataifa mengine yanafanya mazungumzo ya awali na Taliban.
Watu walikisia kuwa Marekani ina mawasiliano na Taliban.
Lakini hilo ndio kwanza kuthibitishwa na kiongozi.
Rais Karzai amesema mazungumzo yanafanywa na Taliban, na kwamba jeshi la mataifa ya nje, hasa Marekani yenyewe, linafanya majadiliano.
Haijulikani nani wanaiwakilisha Marekani, na kama wanazungumza ana kwa ana na Taliban, au kuna mtu kati.
Kinachozungumzwa piya hakijulikani.
Msimamo rasmi wa Taliban ni kuwa majeshi ya kimataifa lazima kwanza yaondoke nchini kabla ya kujadili amani, na itazungumza na serikali ya Afghanistan tu.
Hayo hayalingani na yale aliyosema Rais Karzai.
Haifai kutaraji suluhu ya haraka kutokana na mawasiliano ya hivi sasa.
Utabiri wa pande zote, Nato, serikali ya Afghanistan na Taliban yenyewe, ni kuwa mapigano makali yataendelea kiangazi cha mwaka huu, na pengine miaka kadha ijayo.
Makanisa ya Sudan yanalaani mapigano
Baraza la makanisa ya Sudan linasema lina wasiwasi mkubwa juu ya mauaji makubwa ya raia katika majimbo ya Abyei na Kordofan Kusini.
Katika taarifa yake, baraza hilo linasema watu wameuwawa bila ya kufikishwa mahakamani.
Majimbo hayo kwenye mpaka baina ya Sudan Kusini na Kaskazini, hivi karibuni yamekumbwa na mapigano baina ya jeshi la kaskazini, la kusini na makundi mengine.
Makanisa yameulaumu Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kuwalinda raia, na yamezilaani serikali za kaskazini na kusini Sudan, kwa kutumia nguvu kutatua hitilafu baina yao.
Mfalme anapendekeza mabadiliko Morocco
Viongozi wa wanaharakati wanaotaka mabadiliko nchini Morocco wanapanga kufanya maandamano Jumapili, ingawa Mfalme Mohammed ametangaza mabadiliko ya katiba.
Mfalme wa Morocco alisema mabadiliko anayopendekeza yatapunguza madaraka yake na kuzidisha nguvu za waziri mkuu na bunge.
Wadadisi wanataka katiba mpya iandikwe na kamati itayochaguliwa siyo wajumbe wataoteuliwa na mfalme.
Watu wengine wameyakaribisha mapendekezo hayo, na maelfu ya wananchi walitoka mababarani baada ya hotuba ya mfalme Ijumaa usiku, wakipepea bendera na kupiga honi za magari.
Obama atetea hatua ya kutuma jeshi Libya
Rais Barack Obama hahitaji idhini ya bunge la congress kuwatuma wanajeshi wa Marekani kuhusika katika operesheni za Nato nchini Libya.
White House inasema wanajeshi wa Marekani wanahusika katika majukumu madogo sana nchini Libya
Kulingana na maelezo ya ikulu ya White House, Rais Obama ana uhuru kutuma wanajeshi hao kama kiongozi wa taifa.
Lakini kulingana na sheria iliotungwa wakati wa vita vya Vietnam, rais wa Marekani lazima apate idhini ya bunge la congress kutuma wanajeshi kuhudumu katika nchi ya kigeni ikiwa muda huo utachukua zaidi siku sitini.
Wabunge nchini Marekani wanasema Rais Obama amekiuka sheria hio kwa kuwa muda wa siku sitini ulikwisha mwezi May 20.
Lakini White House imewasilisha taarifa katika bunge hilo, ikielezea kuwa jukumu la wanajeshi wa Marekani ni la kusaidia tu kikosi cha Nato.
White House imesema majukumu ya jeshi la Marekani nchini Libya sasa hivi hayajafikia kiwango ambacho kimewekwa kwenye sheria hiyo ya mwaka wa 1973 ambapo rais atalazimika kuomba idhini ya congress.
Wanjeshi wa Marekani wanasaidia kuongeza ndege za Nato mafuta na katika shughuli za kijasusi nchini Libya, kulingana na maelezo ya White House.
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa wanajeshi wa Marekani hawapo kwenye makabiliano na jeshi la Libya, kwa hivyo hawako vitani.
Kulingana na katiba ya Marekani, bunge la congress ndio lenye uwezo wa kutangaza vita.
Ifikiapo jumapili wiki hii, Marekani itakuwa imehusika kwenye harakati hizo za Nato nchini Libya kwa jumla ya siku tisini.
Juhudi zaidi kupambana na Ukimwi-UN
Mpango wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukimwi (UNAID)unasema kuwa takriban watu milioni sita na nusu katika mataifa machanga wanatumia tiba dhidi ya Ukimwi likifahamu kwamba wapo wengine milioni tisa wanaohitaji dawa bila ya kuwa na uwezo wa kupata dao hiyo.
kuepuka gharama baadaye
Suala la tiba limezuka kuwa suala nyeti tangu majaribio ya mwezi uliopita kuonyesha kuwa unapotumia dawa mapema inasaidia na vilevile kuna uwezekano wa kutoambukiza wengine.
Tiba ni muhimu
Shirika hilo linakadiria hadi watu milioni 34 wanaishi na virusi huku ni watu milioni 30 waliofariki tangu maradhi haya yagunduliwe tareh 5 juni mwaka 1981.
Ingawa kiwango cha maambukizi kinashuka, mpango wa Umoja wa Mataifa una wasiwasi juu ya kupunguwa kwa uwekezaji katika kupambana na janga la ukimwi tangu mwaka jana.
Shirika hilo limeonya kua endapo hali hiyo itaendelea hivyo basi gharama zinazotokana na maradhi hayo zitakuwa kubwa zaidi baadaye.
Onyo hili linatokea wakati viongozi wa serikali mbalimbali wanajiandaa kwa mkutano wa kujadili ukimwi wiki ijayo mjini New York.
Wagombea mtoto baada ya kupeana talaka
WALIOKUWA wanandoa kwa muda wa miaka minne mfululizo wamejikuta wakihatarisha maisha ya mtoto wao kwa kumjeruhi kwa kumgombani kama mpira wa kona huku kila mmoja akihitaji kubaki na mtoto huyo baada ya kutalakiana
Sakata hilo la kugombea mtoto lilitokea juzi maeneo ya Tabata Kimanga ambapo watalaka hao walikuwa wakigombani mtoto wa kiume aliyekuwa na umri wa miaka mitatu
Hali hiyo ilizuka tu mwanaume huyo anayefahamika kwa jina la Muhsin [36] kumpa talaka mke wake aliyefahamika kwa jina moja la Feti [28]
Sakata la kugombani mtoto huyo lilizuka wakati mwanamke huyo alipofika nyumbani kwake hapo kuchukua kilichochake akiwa na jopo la wasindikizaji ili aweze kupisha maisha mapya ya mume wake huyo
Hali ilibadilika baada ya mke huyo kuandaa nguo za mtoto huyo ili aweze kuondoka nae anakoenda na ndipo aliamsha mashetani yaliyolala ya mwanaume huyo na kumtaka amuache mtoto huyo hali iliyofanya mwanamke huyo apinge na kutaka kukimbia nae ndipo walipoanza kugombania motto kila mmoja akivuta mkono wake na kumuweka mtoto huyo katika kipindi kigumu ambapo mtoto huyo alikuwa katika hali mbaya ya kuvutwa kati ya wazazi wake hao wawili
Hali hiyo ilifanya majirani waishio karibu na nyumba hiyo kuingilia kati hata hivyo haikusaidia kitu huku kila mmoja akihitaji kuishi na mtoto huyo
Hata hivyo mwanaume huyo hakukubaliana na hali hiyo hali iliyofanya akaripoti kwa Mwenyekiti waSerikali za mtaa anapoishi na kupigia simu baadhi ya wazee wa familia wa pande zote mbili ili aweze kupata msaada juu ya sakata hilo
Imedaiwa mwanaume huyo alikuwa anagoma mtoto huyo asiondoke kwa kuwa mwanamke huyo alishatangaza kuondoka nchini hali iliyofanya mwanaume huyo kugoma mtoto huyo kuondoka na mama yake huyo
Hadi nifahamsihe inaondoka maeneno hayo majira ya saa 10 jioni iloiacha wanandoa hao wakiwa katika hali ya ututa huku kila mmoja akihitaji kuishi karibu na mtoto huyo
Dar yakithiri kwa uchafu wa mazingira
MKOA wa Dar es Salaam umekubuhu kwa uchafuzi wa mazingira hali iliyofanya wakazi waishio humo kushangaa kuitwa jiji kutokana na kero za uchafuzi wa mazingira ambao ungeweza kuzuilika kukua siku hadi siku
Dar es Salaam imekuwa iko shagala bagala katika mitaa yake ya jiji hali inayofanya kukosa hadhi ya kuitwa jiji kutokana na mazingira yake hayaridhishi machoni mwa watu
Mazingira yamekuwa hovyo kwa baadhi ya mitaa ya jiji kwa kuonekana kwa baadhi ya wakazi kushindwa kudumisha suala la usafi wa mazingira wanayowazunguka.
Jiji hilo hali huwa mbaya zaidi hasa pindi mvua zinaponyesha na wakazi hao kuacha uchafu wa vyooni, mitaro kutirrika barabarani hali inayofanya uchafunzi wa mazingira uzidi kuongezeka.
Mamlaka husika wa afya na usafi wa jiji pia wameonekana kuchangia kwa asilimia kubwa uchafuzi huo wka kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo
Hivi sasa wafanyabiashara ndogondogo wamekuwa wakijiendeshea shughuli zao mahali popote wanapojisikia na sehemu ambazo si rasmi na kufanya kuacha taka ngumu katika maeneo ya jiji na mamlaka husika kufumbia macho suala hilo na inasikitisha majalala ya kutupia taka yakiwa katikati ya barabara, kati ya nyumba na nyumba hali inayofanya uchafuzi wa mazingira na ili hali mamlaka hizo kutumia mamilioni ya fedha za walipa kodi kushughulikia taka hizo hizo
Gen.Nyamwasa atishiwa kufukuzwa
Mashirika yanayopigania haki za binadamu nchini Afrika ya kusini yamechukuwa hatua za kisheria kuitaka serikali ya nchi hiyo ibadili hadhi ya ukimbizi aliyopewa mkuu wa zamani wa majeshi ya Rwanda.
Lt.Gen Kayumba Nyamwasa na Rais Kagame kulia
Wamesema kuwa serikali ilichukuwa hatua ya haraka kumpa hifadhi Luteni Generali Faustin Kayumba Nyamwasa il hali alishirikiana na Rais Paul Kagame katika kukomesha mauwaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda.
Lakini akakimbilia nchini Afrika ya kusini mwaka jana baada ya kukorofishana na Bw.Paul Kagame.
Yeye anatakikana na Uhispania pamoja na Ufaransa kwa madai ya mchango wake katika mauwaji ya kimbari ya siku 100.
Baada ya kukimbilia Afrika ya kusini aliponea chupuchupu jaribio la kumua.Serikali ya Rwanda ilikanusha madai ya kwamba ilihusika katika jaribio hilo.
Afrika ya kusini ilimwitisha balozi wake aliyekueko mjini Kigali baada ya tukio hilo.
Hukumu akiwa uhamishoni
Uhispania na Ufaransa zinamsaka Lt Gen Nyamwasa
, kwa tuhuma za kuongoza mauwaji ya Rais wa zamani wa nchi hiyo Juvenal Habyarimana, tukio lililoanzisha mauwaji ya kimbari.
Shirika lijulikanalo kama 'The Southern Africa Litigation Centre and the Consortium for Refugees and Migrant Rights' limesema kuwa haikubaliki kwa Afrika ya kusini kuruhusu mtu wa aina hiyo kupewa hadhi ya ukimbizi akiwa anashukiwa kushiriki vitendo vinavyokiuka haki za binadamu.
"sheria ya ukimbizi ina lengo la kuwalinda wanyonge, na siyo wale waliosababisha uonevu na kusababisha wengi kuingia katika hali kama hiyo, alisema Allan Wallis, wakili kwenye kituo cha Afrika kusini (The Southern Africa Litigation Centre.)
Serikali ya Rwanda nayo imekuwa ikiipa msukumo Afrika ya kusini imrejeshe Rwanda Lt Gen Nyamwasa atumikie kifungo gerezani cha miaka 24 kufuatia mahakama ya kijeshji kusikiliza na kumhukumu mnamo mwezi januari kwa tuhuma za kutishia usalama wa taifa, kukimbia jeshini bila ruhusa na uchafuzi wa jina la taifa.
Watu 800,000 waliuawa
Takriban watu wa kabila la Watutsi 800,000 pamoja na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa katika mauwaji hayo ya kimbari.
Bw.Kagame aliongoza vuguvugu la RPF ambalo lilikomesha mauwaji mnano mwaka 2000 na tangu hapo amekuwa ndiyo Rais wa nchi.
Baada ya mauwaji, aliahidi kuleta amani na utawala wa demokrasia lakini wakosoaji wanasema anaongoza utawala wa ki-imla.
Ngozi ya chura kuponya saratani
Wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Belfast wamejishindia tuzo kwa kazi waliyoifanya kuhusiana na ngozi ya chura
ambayo wamegundua inaweza kutibu zaidi ya maradhi makuu 70.
kupoza saratani
Watafiti hao walipokea tuzo yao kwenye sherehe iliyoandaliwa na Tuzo ya ubunifu kutoka taasisi ijulikanayo kama Medical Futures Innovation mjini London.
Wataalamu hao wakiongozwa na Profesa Chris Shaw wa taasisi ya Famacia ya Queens, wamegundua proteni mbili ambazo zinaweza kurekebisha kukuwa kwa mishipa ya damu.
Waligundua kuwa proteni kutoka aina ya chura ajulikanaye kwa jina la kitaalamu 'waxy monkey frog' hubana kukuwa kwa mishipa inayosambaza damu mwilini na inaweza kutumiwa kuua uvimbe unaotokana na saratani.
Profesa Shaw alisema kuwa mara nyingi uvimbe huo huweza kuchochewa kufikia kiwango fulani kabla ya kuhitaji damu zaidi ili kupevuka kuwa kivimbe ambacho husaidia kupitisha hewa ya oksijeni na lishe.
Kwa hiyo akaongezea kusema '' Ili kusitisha kukuwa kwa mishipa hii isikuwe hadi kuvimba kutafanya saratani isienee na hatimaye kuiondoa mwilini kabisa.
Hili lina uwezekano mkubwa wa kuifanya saratani yawe maradhi yasiyo uwa ila ya kuishi nayo.
Kundi hilo liligundua pia kuwa aina ya chura mkubwa ajulikanaye kama ''firebellied toad'' huzalisha proteni inayoweza kuchagiza mishipa kukuwa na inaweza kusaidia katika kutibu majeraha ya mgonjwa yapone kwa haraka zaidi.
Kevin Nolan ajiunga na West Ham
Nahodha wa Newcastle United, Kevin Nolan, amekamilisha utaratibu unaostahili na kujiunga na West Ham, ambako amepata mkataba wa miaka mitano.
Amepata mkataba kuichezea West Ham iliyoshuka daraja
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, na aliyecheza chini ya meneja Sam Allardyce katika klabu ya Bolton, amejiunga na klabu hiyo ya ligi ya Championship pasipo kujulikano kwa kiwango gani cha fedha.
"Kupata nafasi ya kushirikiana tena na Sam kwa mara nyingine tena ni jambo kubwa kwangu," alielezea Nolan katika wavuti ya West Ham.
"West Ham wameonyesha juhudi katika kunitamani na kuwa na ari ya kuhakikisha nitawachezea."
Awali mashauri na Newcastle yalikwama kutokana na kutoafikiana Nolan atapata mkataba wa miaka mingapi.
"Ninafahamu klabu kilitoa ahadi nzuri kwa Kevin, lakini hawakuelewana kuhusiana na mkataba," meneja wa klabu ya Newcastle, maarufu kwa jina Magpies, Alan Pardew, alilieleza jarida la Shields Gazette.
"Ningelipenda kumshukuru Kevin kwa juhudi zake kama mchezaji na nahodha, tangu nilipochukua mamlaka msimu uliopita.
"Alionyesha kipawa cha uongozi, na ninamtakia kila la heri West Ham. Ni klabu nzuri, na ninahakika atastawi".
Nolan, ambaye anatazamiwa kuwa nahodha katika uwanja wa Upton Park, ametoa ahadi za kuwaridhisha mashabiki wote wa West Ham walionyesha uaminifu wao kwa kumpa mkataba wa miaka mitano.
Padri Asakwa, Adaiwa Kubaka
JESHI LA POLISI mkoani Morogoro linamsaka Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Alfa.
Taarifa hizo zilitolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Adolphina Chialo
Chialo aliviambia vyombo vya habari kuwa, mwanafunzi huyo ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sasa, aliripoti tukio hilo Mei 28, mwaka huu na kudai kufanyiwa unyama huo Machi 30 mwaka huu na Padri huyo akiwa jijini Dar es Salaam.
Chialo alisema kuwa maelezo ya mwanafunzi huyo yalisema Padri huyo alimwita mwanafunzi huyo aje jijini Dar es Salaam ili aweze kumpatie fedha za masomo ya ziada ikiwa ni utaratibu wake wa kumsaidia mara kwa mara kama yatima kutokana na mwanafunzi huyo kujitangaza kuomba misaada kwa wasamaria.
Alisema mwanafunzi huyo kuwa, Padri huyo alimpigia simu mwanafunzi huyo ya kumtaka kwenda jijini Dar es Salaam akachukue fedha za kumsaidia kimasomo na mwanafunzi huyo kudai hakuonyesha shaka kwa kuwa hakufikiria kama angefanyiwa hivyo na alifunga safari na kwenda huko.
Maelezo ya mwanafunzi huyo yalidai alipofika Dar es Salaam eneo la Manzese alipomuelekeza alianza kupatwa na mashaka pale Padri alipomtaka waingie chumbani na kumwambia hawezi kumpa fedha hizo hadharani.
Ilidaiwa alipofika chumbani mwanafunzi huyo Padri alifunga mlango kisha kumfanyia kitendo cha kumuingilia pasipo idhini yake na kumsihi asiseme tukio hilo kwa mtu yeyote.
Ndipo mwanafunzi huyo alitoa taarifa hiyo ili aweze kupatiwa msaada wa kisheria kwa kuwa alikuwa na wasiwasi na afya yake kwa kushindwa kuendelea kumsikiliza Padri huyo kwa maombi yake ya kumtaka asifichue tukio hilo popote kwani angelidhalilisha kanisa.
Maelfu ya watu wahama Kordofan Kusini
Mashirika ya misaada yazuiwa kuwasaidia walioathirika na vita
Zaidi ya watu elfu hamsini wamelazimika kuhama makaazi yao katika jimbo la kordofan kusini kufuatia mashambulizi ya anga kutoka jeshi la Sudan.
Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, limesema mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu pia yamezuia kuwasaidia watu walioathirika kufuatia mashambulizi hayo.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa Fatoumata Lejeune-Kaba ameelezea kuwa makundi ya wapiganaji yameweka vizuizi barabarani na yanawazuia kupeleka misaada kwa watu waliohama makaazi yao.
Na Mkuu wa kanisa la Kianglikana, Askofu Rowan Williams amesema kuwa huenda hali katika jimbo la Kordofan Kusini ikazidi kuzorota sawa na hali ilivyo katika jimbo la Darfur.
Mzozo huo unaingia siku ya kumi sasa.
Inaripotiwa kuwa mapigano yamekuwa makali kati ya vikosi vya serikali na wanajeshi wa zamani wa jeshi la Kusini.
Sudan Kusini imebakisha siku kadhaa kabla nchi hiyo kubwa barani Afrika haijagawanywa.
Mwandishi wa BBC Peter Martell aliyeko mji mkuu Juba anasema ndege za jeshi la Sudan Kaskazini zimelipua eneo la kijeshi la anga lililoko Kauda katikati ya milima ya Nuba, kwenye makazi ya makundi yanayounga Sudan Kusini likiwaita waasi.
Umoja wa mataifa unaripoti kuwa milio mikubwa ya risasi iliweza kusikika huku mapigano yakisambaa katika jimbo la Kordonfan Kusini.
Kuna wasiwasi kuwa idadi ya watu waliokufa ikaongezeka, huku wafanyakazi wa misaada na viongozi wa dini katika eneo hilo wakisema kuwa wanaolengwa ni wale wanaoaminika kuipinga serikali ya Khartoum.
Watu wanachimba mahandaki wakiogopa mashambulizi zaidi.
Awali wafanyakazi wa misaada walisema mapigano yanazidi kuongezeka katika jimbo la Nuba, ambako ni makazi ya makabila ya waafrika ambao wana uhusiano zaidi na Sudan Kusini kuliko Kaskazini inayokaliwa na waarabu wengi.
Ugiriki yaweza kushindwa kulipa madeni
George Papandreou anasheherekea mwaka wake wa 59 kwa umri, na zawadi alioipokea ni kujiuzulu kwa manaibu wawili wa mawaziri katika chama cha kisoshalisti.
Waziri mkuu wa Ugiriki
Wakati waasi hao wakimuacha mkono, Rais Karolos Papoulias ametaka pawepo na uwajibikaji ili mgogoro wa uchumi usigeuzwe kuwa medani ya kisiasa.
Hali hiyo ya sintofahamu imemtia wasiwasi kamishena wa fedha wa Umoja wa Ulaya Olli Rehn ambaye azma yake ni kuona kwamba sarafu ya Euro haitoathiriwa na mgogoro wa hivi sasa.
Amezitaka serikali za umoja huo zipuuze tofauti zao wakati huu mgumu na zikubaliane juu ya fungu la kuiokoa Ugiriki kwa mara ya pili kufikia mwezi Julai.
Huu ni mwezi muhimu kwa Ugiriki ambayo ina pesa kidogo na itaishiwa mnamo mwezi huo ikiwa haitopokea kitita cha kwanza kama ilivyoahidiwa mnamo mwezi Mei mwaka 2010.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment