Dini ni mfumo wa maishani

Dini ni mfumo wa maishani

Tuesday, May 31, 2011

VIDEO - Mwanamke Alazimishwa Kuvua Nguo Zake ili Aachiwe Huru na Polisi
Polisi 15 wa nchini Mexico wamesimamishwa kazi baada ya kumlazimisha mwanamke waliyemkamata avue nguo zake na kisha acheze uchi mbele yao.
Polisi 15 wakiwemo polisi watatu wa kike wa nchini Mexico wamesimamishwa kazi baada ya video yao wakimlazimisha mwanamke waliyemkamata acheze uchi kuonyeshwa kwenye vyombo vya habari.

Mwanamke huyo alikamatwa na polisi katika mji wa Tijuana akiwa pamoja na mpenzi wake ambapo alituhumiwa kufanya wizi wa credit card na cheki za benki.

Ili aweze kuachiwa huru mwanamke huyo alilazimishwa avue nguo zake zote na kisha acheze dansi uchi mbele ya mapolisi hao 15.

Tukio hilo lilitokea mwezi machi mwaka huu lakini video ya tukio hilo iliyochukuliwa kwa kutumia simu ya mmoja wa polisi hao ilivuja na kuwafikia waandishi wa habari ambapo ilionyeshwa kwenye vyombo vya habari wiki hii.

Polisi wote 15 walioshiriki kumlazimisha mwanamke huyo acheze uchi wamesimamishwa kazi huku wakisubiri kufikishwa mahakamani kwa unyanyasaji walioufanya kwa mwanamke huyo.

Angalia VIDEO ya tukio hilo chini.

Mtoto Mwenye Vichwa Viwili Azaliwa China


Mtoto mwenye vichwa viwili aliyezaliwa nchini ChinaMtoto mwenye vichwa viwili amezaliwa nchini China na kuwa gumzo kwenye vyombo vya habari duniani.
Mtoto huyo alizaliwa katika jimbo la Sichuan akiwa na viungo vyote kamili kama watoto wengine isipokuwa alikuwa na vichwa viwili.

Kwa mujibu wa shirika la habari la China, mtoto huyo alikuwa na mabega mapana ambapo vichwa viwili vilijitokeza kwenye mabega yake.

Taarifa zaidi zilisema kuwa mtoto huyo alikuwa na mikono miwili, miguu miwili na viungo vingine vyote kamili.

Daktari aliyekuwa akiwaangalia watoto hao alisema kuwa ni vigumu sana kwa mtoto huyo kuweza kuishi muda mrefu kutokana na jinsi maumbile yake yalivyoungana.

Angalia VIDEO ya mtoto huyo chini.


VIDEO - Mtoto Mwenye Vichwa Viwili China
Aukata Uume wa Mbakaji na Kuupeleka PolisiMwanamke mmoja wa nchini Bangladeshi ameukata uume wa mwanaume aliyejaribu kumbaka na kisha kukipeleka kipande cha uume wa mwanaume huyo polisi kama ushahidi.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 40 aliukata kwa kutumia kisu uume wa mwanaume aliyejaribu kumbaka na kisha alikichukua kipande cha uume huo na kukipeleka polisi kama ushahidi.


Mwanamke huyo ambaye ni mama wa watoto watatu alishambuliwa na mwanaume huyo wakati amelala usiku wa jumamosi kwenye kibanda chake kilichopo kwenye kitongoji cha Jhalakathi nje kidogo ya mji mkuu wa Bangladeshi, Dhaka, taarifa ya polisi ilisema.

"Wakati alipojaribu kumbaka, mwanamke huyo alichukua kisu na kuukata uume wake na kisha alikifunga kipande hicho cha uume kwenye nailoni na kukipeleka kwenye kituo cha polisi kama ushahidi wa tukio hilo la ubakaji", alisema mkuu wa polisi Abul Khaer wakati akiongea na shirika la habari la AFP.

Mwanamke huyo alifungua kesi polisi akisema kuwa mwanaume aliyejaribu kumbaka ambaye naye pia ana umri wa miaka 40 ambaye pia ni baba wa watoto watano, alikuwa akimsumbua sana kwa miezi sita sasa.

Kipande cha uume wa mwanaume huyo kilihifadhiwa kwenye kituo cha polisi kama ushahidi wakati mwanaume huyo mbakaji akiwa na uume wake kibubutu alipelekwa hospitali kwa matibabu zaidi ili kunusuru maisha yake.

"Tutamtia mbaroni wakati hali yake itakapokuwa nzuri", alisema mkuu huyo wa polisi.

No comments:

Post a Comment